Mtikila ashinda tena kesi ya mgombea huru; Afungua upya Mahakama ya Afrika Mashariki

Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
751
65
Rev. Mtikila ameshinda tena kesi yake ya mgombea huru. Hivyo kwa mujibu wa hukumu hiyo, sasa hivi ni ruksa kwa mgombea wa Urais na Ubunge kutoteuliwa na chama chochote, na bunge limepewa agizo la kutengeneza sheria itakayoruhusu mgombea huru.
 
Hukumu kama hiyo ilitolewa 1994! na serikali haikutii amri halali ya mahakama. Kwanini serikali itarajiwe kutii amri hivi sasa!!! ??
 
Hakimu au Jaji anapotoa hukumu yenye amri ya kutekeleza kitu lazima awe makini sana. Lazima toe deadline ya kutekeleza amri hiyo, na ajue ni nani atakamatwa (kwa kufungwa pingu) na kuletwa kwake kama hiyo deadline itapita bila amri kutekelezwa.

Sasa Jaji anapoamuru bunge lirekebishe sheria, bila hata kutoa deadline, kuna dosari mbili kubwa. Mosi, Jaji ataamuru nani akamatwe na kuletwa kwake kujibu shtaka la kupuuza mahakama kama Bunge halitarekebisha hiyo sheria? Pili, kama hakuweka deadline, basi hata ipite miaka mingapi, bado tunaweza tukasema bunge linasubiri lipate fursa ya kutekeleza amri, halijapuuza mahakama.

Hayo yote ni tisa. Kumi ni kwamba mahakimu na majaji wetu hawana ubavu wa kuikoromea serikali. Sidhani kama uteuzi wao na promotion zinafanywa kwa namna inaoruhusu wawe independent. Sidhani kama tuna kamati huru ya kushughulikia uteuzi na promotion za mahakimu na majaji.

Sijasoma hiyo hukumu inayozungumziwa hapa. Hatahivyo, sitegemei kwamba itazaa matunda yaliyokusudiwa.

Augustine Moshi
 
Mtikila ni agent wa CCM, demokraisa ya nchi haiwezi kushinda na viongozi wanaojifanya upinzani kumbe ni vibaraka, waliopandikizwa na chama tawala, na kama kuna apologists wake aeleze wakati ule alipokwama London na US ilikuwaje serikali ya CCM ikamlipia kuanzia hotel mpaka kurudi nyumbani?

Watu kama Mtikila they belong to prison kwa kudanganya wananchi, for what? The man is always ni jela sasa huu udouble-agent unamsaidia nini kama CCM wananweza kumuweka jela anytime?

Cha muhimu hapa ni the rule of law na the whole process iliyofikisha mahakama kutoa huo uamuzi, lakini as far as Mtikila hapana huyo ni rat tena a big one! Hawa ndio vibaraka ambao kazi yao ni kupanga mstari kwa mzee JM na Kingunge ili wale halafu wanakwenda kudanganya wananchi!
 
mwanasiasa, sheria yetu ni ya ajabu.. hata kama mahakama inasema sheria fulani ni kinyume na katiba, sheria hiyo haikomi kuwa na nguvu hadi Bunge liibadilishe sheria hiyo au kipengele husika. Hivyo basi, kama ukitokea uchaguzi kesho, hakuna mgombewa huru atakayeruhusiwa!!!! hilo ndilo lililokuwa tatizo la hukumu ya awali 1994.

Hata hivyo jopo la majaji wa sasa wameamua kuiweka serikali kwenye kona. Ukitokea uchaguzi kesho, na serikali haijaweka utaratibu wa kuruhusu wagombea binafsi basi Mtikila anaweza kwenda mahakamani na kusimamisha uchaguzi huo!! So unless, serikali ikate rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa na hukumu ibadilishwe, basi wagomba huru watakuwepo... kwani bila ya kufanya hivyo hakuna uchaguzi utakaoweza kufanyika!!!
 
BUNGE la Jumuiya ya Afrika Mashariki limeingia katika mtihani mwingine, baada ya Mchungaji Christopher Mtikila, kuweka pingamizi la kuapishwa kwa wabunge wa Bunge hilo kwa madai ya kukiuka Ibara za 50 na 51 ya Mkataba wa Jumuiya hiyo.

Bunge hilo lilikwama kuapishwa mwishoni mwa mwaka uliopita, baada ya Serikali ya Kenya kushitakiwa katika Mahakama ya Jumuiya hiyo, kwa madai ya kukiuka Mkataba huo, ambapo Serikali ya Kenya ilipigwa mwereka na kukwamisha Bunge hilo kuapishwa hivyo kukata rufaa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Bw. Mtikila alisema baada ya waliokuwa wabunge wa Bunge hilo, Dkt. Harrison Mwakembe na Bi. Beatrice Shekilango kuwa wabunge wa Bunge la Tanzania na kuwachagua Dkt. Norman Sigala na Bi. Hilda Kibacha, ilitakiwa kuchagua wabunge saba tu, ili kukamilisha idadi ya wabunge tisa.

Alisema kwa mujibu wa Mkataba huo, mbunge anatakiwa kuwa madarakani kwa miaka mitano, hivyo kuwaengua wabunge waliochaguliwa Machi mwaka jana ni kosa, kwani kwa mujibu wa Mkataba, sasa wabunge kutoka Tanzania ni 11 kutokana na wabunge waliochaguliwa awali kutochaguliwa kisheria.

“Dkt. Sigala na Bi. Kibacha kwa mujibu wa Mkataba ni wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, ukiongeza wabunge tisa waliochaguliwa baadaye jumla Tanzania ina wabunge 11 jambo ambalo ni kinyume na mkataba huo…tumepinga hilo katika Mahakama hiyo kwa kesi namba 2 ya mwaka huu,”alisema Bw. Mtikila.

Alisema pamoja na kutaka wabunge hao wawili watambuliwe, pia uchaguzi wa wabunge wengine haukua sahihi, kwani kwa mujibu wa Mkataba, wabunge wanatakiwa kutoka vyama vya siasa vya kiraia na jumuiya za kijinsia, jambo ambalo halikufuatwa, hivyo ujumla wabunge hao hawakuchaguliwa kihalali na wachaguliwe upya kwa utaratibu uliowekwa na Mkataba huo.

“Lengo ni kuishikisha adabu CCM iache ukiritimba wa kuamua kufanya mambo yao wanavyotaka na si inavyotakiwa…kila Mkataba wa Jumuiya hiyo upo wazi, hivyo hakuna sababu ya kufanya mambo nje ya utaratibu huo kesi yetu iko chini ya Kampuni ya Audax & Company Advocates,” aliongeza Bw. Mtikila.

Kesi ya kuwazuia wabunge wa Kenya kuapishwa baada ya Serikali kushindwa katika kesi hiyo na kukata rufaa, ilifikia mwisho juzi ambapo hukumu yake inatarajiwa kutolewa Jumanne ijayo.

Akizungumzia juu ya maoni yanayoendelea kuhusiana na kuanzishwa kwa Shirikisho, Bw. Mtikila alisema ni kinyume cha Katiba ya Tanzania na chama chake DP kinajiandaa kuweka pingamizi mahakamani kuhusiana na suala hilo.

Alisema nchi ni ya wananchi na hakuna kiongozi mwenye mamlaka na nchi hii, hivyo kila Mtanzania ana uhuru wa kushiriki kujiunga katika Jumuiya hiyo na Shirikisho kwa ujumla

Chanzo:-
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=2228
 
mpigakura safi sana kutuletea makala ya gazeti especially sisi ambao hatupati,live.napongeza juhudi za mh mtikila mpiganaji ambaye mara zote yuko mbele kutetea haki.

natoa ombi kama kunA MTU ana mawasiliano na rev mtikila amlete huku kama mbowe ,tunataka hichi kijiwe kiwe na mawazo mbalimbali,na historia ya mtikila inajulikana ni ya kiupambanaji..

mwanakijiji naomba pia kama unaweza kumpata huyu mtanganyika umhoji,ahsante saana!!!
 
Hi Philemon**
Hii hapa contact zake(MTIKILA).

Contact Address Mchikichini Ilala P.O Box 63102 DSM
Tel:0741 -430516; 0741 - 625349
 
Safi sana Mtikila .Wasomi wetu wa sheria na ma PhD yao wamelala kimya kama vile hawako .Halafu anakuja mjinga anasema Mtikila anatumiwa na Mengi Je Mengi anataka nini EAC ?Watu bwana !
 
Atayesema mtikila ni kibaraka/katumwa na mwingine zaidi ya watanzania basi itabidi tum.....
 
Mtikila ni shujaa, ilitakiwa aungwe mkono na Watanzania wengine kama hao
wasomi wa sheria japo kwa chini chini na sisi wengine wote kumpa nyenzo mbalimbali za kumsaidia kuwa na data za uhakika.

Kweli Mtikila akaribishwe Jamboforums.
 
Mtikila Hoyeeeee...........!

Ningemshauri kama ikiwezekana ashauriwe pia kupinga uanzishwaji mzima wa EAC/EAF. Msabaha na team yake wapangiwe kazi nyingine, kwani wanatafuna kodi yetu pasipo ridhaa yetu. Kwamba watanzania hatutaki FULLSTOP!
 
Mimi nasubiri kwa hamu kesi ya kuvunjwa katiba ya wale viongozi waliogoma kurudisha fomu za kutangaza mali na madeni yao.
 
Naamini kabisa hii forum inaweza kuwa sehemu muhimu ya kuwapa moyo watu ambao wako mstari wa mbele kupigania haki na maslahi ya watanzania bila kujali itikadi ya vyama vyao. Watu wachache mfano wa Mtikila ambao wamekuwa wakipigwa vita vya propaganda na Serikali na Chama cha CCM na hivyo kuonekana watu wasiofaa katika jamii ya Tanzania.Wengi wamevunjika moyo na kukaa kimya baada ya jamii kukubaliana na propaganda za CCM na serikali yake.
Ni wazi kuwa sehemu kubwa ya Watanzania tupo gizani. CCM na serikali yake wanapenda tuendelee katika hali hiyo.Pale inapotokea mtu au Chama cha siasa au organization yeyote inayotaka kuwaweka Watanzania katika nuru inakuwa ADUI ya serikali na CCM. Tusikubali kuingia katika mtego huo.
 
mwanakijiji please mpe mwanamapinduzi ,mtikila air time umeshawahi kusikiliza kanda zake za mwanzo wa miaka ya 90,ndio moja wa viongozi wa mwanzo kubebwa pale mlimani ana historia ndefu..namba zake kazitoa MPIGA KURA hapo juu...

bado natoa wito akaribishwe forum...tutakuwa na dream team..
 
Mchungaji Mtikila kufungua kesi kusimamisha uchaguzi Tunduru

Na Mathew Kwembe © Mwananchi Communications Ltd

Mwenyekiti wa DP Mchungaji Christopher Mtikila leo anafungua kesi Mahakama kuu kusimamisha uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Tunduru. Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za chama hicho mchungaji Mtikila alisema hatua hiyo inafuatia kitendo cha Tume ya Taifa ya uchaguzi kukaidi uamuzi wa mahakama kuu wa kuruhusu wagombea binafsi. Alisema chama hicho kitawasilisha kesi hiyo mahakama kuu leo ili kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo pamoja na ule wa madiwani wa kata 14 ambao nao umepangwa kufanyika hivi karibuni.

Mchungaji Mtikila aliongeza kuwa tamko la Mwenyekiti wa Uchaguzi la kuendesha uchaguzi huo bila wagombea binafsi kwasababu Mwanasheria mkuu wa serikali atakata rufaa halina msingi kwa kuwa uamuzi wa mahakama kuu una uzito toka siku ile iliposomwa hukumu. “Tunakwenda kuzuia uchaguzi huo usifanyike kwa kuwa tunaona wazi kuwa hapa kuna kudharau Mahakama kwa hiyo tutaidhibiti tume ili isiendeshe uchaguzi huo,” alisisitiza Mwenyekiti huyo wa DP. Kwa mujibu wa Mtikila, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilipewa kipindi cha mwaka mmoja iwe imeandaa utaratibu wa ushiriki wa wagombea binafsi, lakini imeshindwa kufanya hivyo kwa madai kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali anajiandaa kukata rufaa kupinga uamuzi wa kuruhusu wagombea hao.

Pia Mchungaji Mtikila alisema kuwa kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo ni kinyume kwa kuwa hakukuwa na uandikishwaji upya wa wapiga kura. Alisema toka mwaka 2004 zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura, vijana waliokuwa na umri wa miaka 15 hadi 17 ambao wakati ule hawakuruhusiwa hivi sasa wamefikia umri wa miaka 18 na si haki wao kutoshiriki uchaguzi huo. “Wale waliokuwa na miaka 15 mwaka 2004 leo hii wana miaka 18, kadhalika wale waliokuwa na miaka 16 leo wana miaka 19, na waliokuwa na miaka 17 leo wana miaka 20 na hawa ndiyo walio wengi tunashangaa Jaji Lewis Makame anaposema hakuna kuchapisha daftari lingine hilo ni batili,” alisema Mtikila.
 
Nimezungumza na mwanasiasa ambaye ni mtetezi mkubwa wa Katiba yetu Mch. Christopher Mtikila juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea Tanzania na hususan juu ya suala la wagombea huru. Mchungaji Mtikila bado ana moto ule ule aliokuwa nao kwa zaidi ya miaka 20 sasa!!! Mchungaji Mtikila anazungumzia suala la Kadhi, uhuru wa vyama vya kisiasa, makosa ya CCM, na haja ya Katiba Mpya. Pia anazungumzia madai yaliyoandikwa na mojawapo ya vyombo vya habari vya Tanzania kuwa amempiga mlinzi wa ofisi ya Msajili wa vyama vya kisiasa hapo jana. Zaidi ya yote anaelezea "gabachori" ni nani katika Tanzania ya leo? Ameahidi kuungana nasi siku si nyingi hapa kwani ana mengi ya kusema.

Matangazo yatarushwa kesho kwenye KLH News Exclusive

http://mwanakijiji.podomatic.com
 
anatuahidi nini endapo tutamchagua kuwa raisi wa TANZANIA?
na je anaonaje suala la hawa wagombea wa vyama vya upinzani kutobadilika toka 1995 walipoanza kugombania uraisi bila mafanikio na wao kudai kuwa wanaibiwa KURA??sasa tuendelea kuwaacha na kuendelea kuibiwa kura au wasigombanie huo uraisi nini maoni yake kuhusu haya?
 
Back
Top Bottom