Mtikila aibua mapya tume ya katiba

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,244
attachment.php


MAKUNDI maalumu jana yaliendelea kutoa maoni yao kwenye mchakato wa Katiba Mpya, huku DP kikipendekeza Rais aapishwe baada ya siku 90 tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.

Mbali na maoni hayo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila, makundi mengine; wakulima, wafugaji, wanahabari na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) nayo yalijitokeza kutoa moyoni.

Mtikila alisema kipindi hicho cha siku 90 kitatoa fursa kwa watu wanaotaka kuwasilisha pingamizi dhidi ya ushindi wa Rais mteule kufanya hivyo, kabla ya kuapishwa.

Alisema pingamizi linaweza kufanyiwa kazi kwa kipindi hicho cha miezi mitatu ili kuhakikisha kuwa taifa linapata kiongozi halali mwenye ridhaa ya wananchi.

“Pia tunataka kinga ya Rais ikome pale anapomaliza muda wake wa uongozi, kama alifanya makosa yoyote ya jinai aweze kushtakiwa ili kujenga nidhamu ya uongozi katika ofisi ya umma. Utaratibu wa kumwondoa madarakani uimarishwe asisubiriwe hadi amalize muda wake wa uongozi.”

Alisema kuwa Katiba ya nchi inapaswa kuwa mali ya wananchi wenyewe ili watawala wasijihusishe katika kuwaundia wananchi Katiba kama ilivyo kwa mchakato unaoendelea sasa wa kupata Katiba Mpya.

“Kumekuwa na hoja ya kuwapo kwa Serikali ya Tanganyika, hilo ni jambo muhimu na watu kutoka Tanganyika ni lazima wawe na Serikali yao ndani ya mipaka ya ardhi yao kupitia Katiba Mpya,” alisisitiza Mchungaji Mtikila.

Aliongeza kuwa nafasi za wabunge wa viti maalumu bungeni ziondolewe ili viti hivyo vishindaniwe kidemokrasia.Alisema wanawake wanatakiwa waelimishwe na kupikwa ili wahimili ushindani katika medani za kisiasa. Alisema kuwa taifa linahitaji viongozi bora na siyo kustarehesha jinsia.
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1357877461399.jpg
    uploadfromtaptalk1357877461399.jpg
    37.4 KB · Views: 476
Huyu pamoja na weakness zake nyingi lakini amekuwa na mchango Mkubwa sana hapa Tanzania ukifananisha na wanasiasa wengi wakubwa, kwa mfano mambo ya Visa kwenda Zanzibar yeye ni mmoja wa wapambanaji wakubwa waliokomosha huo upuuzi.
 
Well said,hilo la mambo ya upendeleo linapaswa kufutwa mara moja watapendelewa mpaka lini na hii ndio inazidi kuwafanya wajione kama wao ni wa kupendelewa siku zote tunapaswa kuandaa mazingira ili kuwa na ushindani wa usawa sio upendeleo.
 
Mtikila ni think tank. Anatazama mbele sana na haropoki akiwa na hakika na jambo analiamini na anashikilia hayumbi. Hongera sana baba mchungaji
 
Mawazo mazuri. Na hilo la rais kuapishwa baada ya siku 90 ni wazo zuri, haraka ya kuapisha mtu baada tu ya matokeo kutangazwa ni woga na kunyima watu kuhoji uhalali wa kura zilizohesabiwa. Safi Mtikila.
 
Mtikila ni jembe nakumbuka aliingia kwenye sherehe za uhuru wa tanganyika na bendera ya tanganyika wakamkamata bila kusahau ile kesi ya mgombea binafsi leo ccm wanataka mgombea binafsi.
 
safi mchungaj mtikila. eti mtu asishtakiwe! hamna kitu kama hicho. mtu akitoka kwenye urais awe anaweza kushtakiwa. lasivyo watu watakuwa wanatoana roho kugombea kwenda ikulu kwani watajua wakifika pale watageuka miungu watu wenye uwezo wa kuua zaid, kuiba kwa kufuru na hakutokuwa na wa kuwafanya kitu that time na baadae. mtu hajawah kuwa malaika. hii itasaidia kumweka rais kwenye mstari. safi mchungaj
 
Mawazo mazuri. Na hilo la rais kuapishwa baada ya siku 90 ni wazo zuri, haraka ya kuapisha mtu baada tu ya matokeo kutangazwa ni woga na kunyima watu kuhoji uhalali wa kura zilizohesabiwa. Safi Mtikila.

Namkubari sana Mch. Mtikira, namuunga mkono 500%
 
Naunga mkono hoja zote na hasa hili la kuondoa kinga baada ya urais kumalizika. Hii itawafanya wahusika kuwa na adabu wawapo madarakani!
 
Back
Top Bottom