sasa kumbe umeshajua tatizo liko wapi, hata sisi tulipohitimi a-level na kukaa mtaani muda mrefu bila ajira tulibuni ajira ya kufundisha tuisheni kwenye vituo vya mitaani, sasa huo mkwara wake sio wa kitoto, wanafunzi wakifunga shule zao wakifika tu kwanza unawapiga mkwara wewe nani, ulisomea wapi na ufaulu wako ulikuwaje katika somo husika, basi wakitoka hapo siku ya pili wanakuja na wenzao maisha yakasonga mbele.
Sababu ya pili. Ni vigumu sana kwa mtahiniwa binafsi kufaulu kama hajui ni kwanini alifeli. Mtahiniwa binafsi anayejua kosa lake ni rahisi kutolirudia na huyo ana nafasi kubwa ya kufaulu mtihani.
Sababu ya tatu. Watahiniwa wengi unaowaona mitaani wakihangaika na kufanya mitihani kama pc, hufanya hivyo kutokana na shinikizo la familia au wazazi ambao wanajua umuhimu wa elimu, vinginevyo vijana wa siku hizi kama ingekuwa ndani ya uwezo wao wangependa waende kwenye kusomea kazi moja kwa moja veta.
Sababu ya nne. Haiwezekani mtu aliyeshindwa kufaulu ndani ya mfumo rasmi huku akiwa huru na kazi yake ni moja tu kusoma na bado akafeli halafu unatarajia afaulu wakati ameshaanza maisha ya mtaani huku ameanza kazi na demu anamtegemea yeye na bado starehe inamsubiria yeye bila kufungungwa fungwa na mtu.