Mtihani wa kwanza anga za kimataifa kwa Rais ni mwezi August mwaka huu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,858
Mwaka huu mwezi wa nane mjini Gabarone kutakuwa na mkutano wa "Organ of Peace and Security wa SADC" ambapo Bongoland ndio itakuwa nchi mwenyekiti na ni lazima Mkuu wa Kaya awepo kwani mwenyekiti wa kikao hicho daima ni lazima awe mtu mwenye wazifa wa Ukuu wa Kaya na atakuwa ni Mkuu wa Kaya wa nchi ambayo inashikilia kiti hicho cha uenyekiti.

Tusubirini mwezi wa nane sio mbali tutapata majibu ya maswali yote ambayo tumekuwa tukijiuliza kuhusu huyu Mh.hasa kwenye anga za kimataifa.

NB:MKutano huo pia unaweza kufanyikia hapa Bongoland iwapo mwenyekiti ataamua kuwaita wenzake hapa.
 
Mtoa mada wewe ni Mtanzania? Mbona kiswahili chako kimepinda sana!? Au elimu yako na wewe ni hapa na pale nini!?
 
Tatizo liko wapi? Atakabidhiwa huo uenyekiti "in absentia". Watu wanapiga hadi ma-PhD na hawahudhurii mahafali yet wanatunukiwa shahada zao in absentia ndio itakuwa huo uenyekiti.
 
Hyo NB Ishatoa jibu kamili.... sina haja ya kujiuliza tena
 
Hata hivyo binam mimi nina mashaka pia na uwezo wa mama hasa kwenye engo kama hizo za kimataifa. Unakumbua hii ya juzi hapa S.A mstaafu alienda kumpa sapoti mama?
Huyu mama si ndiyo yule alisema tunayo madini ya chuma na tunaweza kuchimba miaka 700 wakati wa kampeni?
Sasa ukichanganya na huyu wa Kuwait kweli mambo ni gongana
 
Natamani siku moja mkuu wa kaya azungumze kiswahili katika international meeting yoyote ile kwani ni lugha nzuri na ina wakalimani kwann tujitese na lugha za watu?
 
Kama shida ni lugha ya Malkia, ataongea lugha yetu. Hii lugha yetu inatumika katika mikutano ya AU na wakalimani wapo. Rais wa China alikuja hapa na aliongea kichina, sioni ajabu Mkuu wangu wa Kaya akiongea Lugha yetu adhimu katika kikao cha kimataifa kwani atakuwa anaienzi lugha yetu. Kiswahili Oyeee!
Kwani tatizo ni lugha mbona hata speech ya kiswahili yenyewe ni mbovu kupindukia-inambidi ajifunze namna ya kutoa speech kama kiongozi wa nchi sio speech kama anagombana
 
Acheni kuwahusudu mafedhuli waliokwapua rasilimali zetu na bado nnawagwaya,mwacheni magu afanye yake.tulishafika icu msiturudishe huko,diplomasia ndio iliowafikishas libya walipo.
 
Hivi kweli kuna watu wanaamini kuwa Raisi hasafir kwenda nje ya mipaka ya nchi yetu sababu ya Lugha??? Hii ni hoja mufilisi
 
Hata hivyo binam mimi nina mashaka pia na uwezo wa mama hasa kwenye engo kama hizo za kimataifa. Unakumbua hii ya juzi hapa S.A mstaafu alienda kumpa sapoti mama?
Naaam Mpwa
Askari wa Mwamvuli ilibidi ai intervene
 
Mmmh kuna mtu aliniambia kuna kingilishi cha kisiasa na kingine cha kisayansi! Akasema ukibobea kingilishi cha kisayansi basi si rahisi kuzungumza cha kisiasa! Eti wajameni kuna ukweli hapo?
 
Mh raisi azungumze lugha yetu ya taifa yaani Kiswahili.Bila shaka wakalimani wapo na mambo yatakuwa safi tu.
 
Hivi kwa mfano siku mbili kabla ya mkutano aka jisingizia ugonjwa na kulazwa pale Kikwete C. Institute itakuwaje? Hawezi kuteua mwakilishi?
Maana heri nusu shari kukiko shari kamili
Yeye ni Rais mzee!!! Hana haja ya kusingizia. Ataamua tu kwenda au kutokwenda. Marais wasiosafiri dunia hii ni wengi. Sijasikia hata safari za rais wa North Korea.
 
Mwaka huu mwezi wa nane mjini Gabarone kutakuwa na mkutano wa "Organ of Peace and Security wa SADC" ambapo Bongoland ndio itakuwa nchi mwenyekiti na ni lazima Mkuu wa Kaya awepo kwani mwenyekiti wa kikao hicho daima ni lazima awe mtu mwenye wazifa wa Ukuu wa Kaya na atakuwa ni Mkuu wa Kaya wa nchi ambayo inashikilia kiti hicho cha uenyekiti.

Tusubirini mwezi wa nane sio mbali tutapata majibu ya maswali yote ambayo tumekuwa tukijiuliza kuhusu huyu Mh.hasa kwenye anga za kimataifa.

NB:MKutano huo pia unaweza kufanyikia hapa Bongoland iwapo mwenyekiti ataamua kuwaita wenzake hapa.
Miezi minane atakuwa kesha patapata angalau
 
Back
Top Bottom