Mtihani rahisi kupata 100% ni huu hapa

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Maswali rahisi kwa TANESCO au TUICO – TANESCO.

Nini tafsiri ya kina ya Tamko la Viongozi wao wa TUICO:--

1. Kusema kuwa wao hawatalipa Dowans isipokuwa Dowans ilipwe na Serikali: Je serikali ikiilipa Dowans wao hawataumia au kuguswa na hayo malipo (directly or indirectly) kwa vyovyote?

2. Kumwonya Mh. Magufuli juu ya bomoa bomoa itakayowagusa. Kwamba hawatoki mpaka Waziri ametoka katika jengo lao. Je hii ndiyo busara ya kudeal na issues seriously.

3. Kudai warejeshewe mali zao zikiwemo majengo mfano Makao makuu ya wizara yenye dhamana kwa shughuli zao n.k yaliyochukuliwa au taifishwa na Serikali. Hivi wao wanapewa au walipewa mali na nani, ili naye aanze kudai kurejeshewa?

4. Kuuliza kuwa, ni kwa nini Wananchi hawaelezwi mchanganuo wa bill za umeme za TANESCO ilihali humo ndani zipo kodi ya VAT (18%), EWURA (1%) na REA (3%). Je ni wajibu wa nani kueleza wananchi hayo? Wao (TANESCO) kweli hawahusiki?

Haya nyote mmepata 100% kama nilivyowaahidi!
 
Back
Top Bottom