Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,377
- 8,075
MTIHANI MKUBWA....
Bibi yetu mpenzi (pichani katikati), amezaliwa kabla ya vita ya kwanza ya Dunia. Jana Alhamisi saa 10 jioni
alimzika kijana wake muhimu hapa Kiabakari-Musoma, huyu ni Mzee Silyvester Korogo (Born on 1932 akiwa mtoto wa nne wa bibi). Wakati picha hii inapigwa jana nilikuwa nazungumza na bibi na swali kubwa aliloniuliza ni...
BIBI; "Kisika...(jina alilonipa utotoni)...namuulizia mwanangu Malima, anaendeleaje?" (Yani, bibi anamuulizia kijana wake mwingine wa kipekee na peke yake aliye hai baada ya kifo cha Mzee Korogo. Ananiuliz kwa sababu iliamriwa asijulishwe kuwa vijana wake wote wamefariki kwa mpigo).
MIMI; "...kama ulivyojulishwa, Uncle Malima alienda Musoma Mjini na amelazwa akitibiwa KISUKARI ambacho hapa Kiabakari hakitibiwi kwani hakuna daktari".
BIBI; "...sasa anaendeleaje huko hospitali?",
MIMI; "...tukitoka kumzika Mzee Korogo mimi na wenzangu tutakwenda Musoma Mjini kumjulia hali".
BIBI; "...ukitoka Musoma uje unieleze hali yake",
MIMI; "...ntafanya hivyo bibi"
BIBI; "....na umwambie aje kunisalimia haraka"
MIMI; "...kwaheri bibi"..
Baada ya Mazungumzo yetu, Padre Wojciech Adam Kościelniak aliongoza ibada fupi nyumbani kwa marehemu kisha tukaelekea kwenye makaburi ya Kanisa Katoliki na kumzika mjomba wetu mpendwa.
Usiku wa kuamkia leo, watoto wa pekee wa bibi waliobakia (MAMA LUCY na MAMA JANE) wakaniita na kunikumbusha mazungumzo yangu na bibi, wakanambia sasa kukikucha kesho (yaani leo Ijumaa), mpelekee bibi yako mrejesho wa hali ya mgonjwa mliyeahidiana, mjulishe amefariki asubuhi. Huu ni MTIHANI MKUBWA kabisa kukabidhiwa na watu wazima and I am speechless! Hii kazi ntaifanyaje?
Kijana wa bibi aliyekuwa amebaki badala ya Mzee Korogo ni huyo Uncle MALIMA tu (aliyestaafu Jeshi mwaka Juzi), Malima amefariki ghafla siku moja baada ya kifo cha kaka yake. Bibi amesafiri na kufika msibani bila kujulishwa kuna msiba juu ya msiba.
Niwaelezeapo jambo hili bibi anajua ana kijana mmoja hai na kuwa amemzika mmoja jana. Kumbe ukweli ni kinyume kabisa, bibi amepoteza vijana wote ndani ya siku mbili na leo lazima aambiwe ukweli mchungu. Hii kazi niliyopewa sijaipenda kabisa!
Mtatiro J,
Kiabakari, Musoma.