kulunalila
Member
- Dec 1, 2011
- 43
- 6
Wewe malima/yaikayaika acha sisa za kitto ndugu yangu, jipange mshindane kwa hoja.
Mtu pekee wa kuwakomboa wana ukerewe ni mama Mongela, tabu yote hii imetokana na fitina za msekwa. Bila mongela kurudi jimboni kura za chuki zitaendelea na watu wa ajabu ajabu watachaguliwa.
Baada ya maelezo hayo marefu, tunaomba sasa utuletee Cvs za
- Salvatory Machemli
- Joseph Mkundi
- Martin Malima
Ndugu wana JamiiForum wenzangu!
Katika jukwaa hili uliwekwa uzi wenje kichwa cha habari "Mtifuano wa Ubunge Jimbo la Ukerewe". Katika ‘uzi' huo mwandishi aliyejitambulisha kwa jina la "Yaika Yaika" ameeleza maoni na mtazamo wake juu ya aliowaita watia nia. Katika orodha yake amemtaja Martin Malima, ambaye ndie mimi. Kwanza kabisa naomba niweke wazi kuwa mimi hua ni muumini wa uhuru wa kutoa na kupokea maoni, hata kama maoni mengine yataniumiza. Yaika Yaika ametoa maoni yake, na ninakiri kuwa maoni yake yameniumiza, na yamewaumiza wengine pia. Kwa mtazamo wa harakaraka msomaji anaweza kusema kuwa taarifa hiyo inanijenga, na hivyo kunihusisha. Kwa bahati mbaya kikundi cha watu wachache mjini Nasio- Ukerewe wanaamini hivyo, na wameanzisha mradi wa kuchapa taarifa hii na kuisambaza kwa wanachama. Watu hawa wanakwenda mbali na kuwashawishi wakubaliane na hisia zao kuwa mimi ndiye niliye andaa taarifa hiyo. Baadhi ya waliopokea taarifa hizi wamezipuuza na wengine wameumizwa na taarifa hizi na wamenitaarifu kuumizwa kwao. Naomba kutumia fursa hii kuwapongeza wote waliopuuza taarifa hizi, na nawapa pole wale wote walioumizwa na taarifa hizi za kizushi. Naomba ieleweke wazi kuwa sijatangaza kugombea Ubunge katika jimbo lolote lile ndani ya Tanganyika na hivyo sina haja ya kumchafua mtu yeyote. Na hata kama ikitokea nikatangaza kugombea ubunge sitarajii kumchafua mtu yeyote. Mimi sio mwanasiasa wa ‘level' hiyo. Mpaka sasa hakuna mtia nia yeyote wa ubunge katika Jimbo la Ukerewe isipo kuwa Mbunge wa sasa Salvatory Machemli. Ninachofahamu ni uwepo wa hofu kwa kikundi cha wanasiasa dhaifu ambazo msingi wake ni hisia. Kikundi hiki cha wanasiasa dhaifu walianza kutengeneza mkakati wa kuwashughulikia wale wote wanaowahisi wana sifa za kugombea ubunge kushinda yule wanayehisi anafaa, kabla na baada ya uchaguzi ndani ya chama. Bila shaka makala ya Yaika Yaika ni moja ya mkakati huo au ni utambulisho wa ujio wa kikundi kingine au ni mkakati wa ma-ccm kukigawa chama. Matukio ya kuandika vitu ili aonekane ni fulani kaandika au kutumia majina ya watu wengine au kutoa taarifa zenye utata kwa kutumia majina ya bandia au kuwazushia wengine, ni kawaida kwa wanasiasa dhaifu. Naomba nitoe rai, kwa wale wanaojiita wanasiasa, wajitahidi kuishi maisha ya kisiasa. Wapambane kwa hoja na sio kuchafua wengine. Tutumie majukwaa rasmi kueleza mawazo yetu na tusifiche majina yetu halisi. Aidha, kwa vile ‘intelejensia' ya chama imekua naamini watamnasa Yaika Yaika na mawakala wake. Nawatakia kazi njema za kuijenga Tanganyika yetu kwa mstakabali wa Tanzania. Ndimi,
Martin Majula Malima
Naye anautaka ubunge!Ahsante kwa taarifa yako siku nyingine unapoandika taarifa kama hii jaribu kuweka paragraph bwana mkubwa.
Ahsante kwa taarifa yako siku nyingine unapoandika taarifa kama hii jaribu kuweka paragraph bwana mkubwa.
Watu wa Ukerewe bhana yaani mnapata mafanikio kwenye chaguzi serikali za mitaa badala ya kuamua kimya kimya mnaanza kupiga kelele. Vigezo vyenu vimekaaje