Mtifuano wa Ubunge Jimbo la Ukerewe

Mtifuano wa Ubunge Jimbo la Ukerewe

Yaika Yaika

Member
Joined
Jan 6, 2015
Posts
7
Reaction score
2
Ndugu wanajanmvi!

Kwa wiki kadhaa kumekuwa na habari za kuwepo kwa mgogoro katika ya Mbunge wa Ukerewe Salvatory Naluyaga Machemri na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ukerewe na Diwani wa Kata ya Bukiko, Joseph Mkundi. Kwa wasiofahamu hili wanaweza kudhani kuwa mgogoro huu umeanza baada ya issue ya Rehema kumpeleke Machemli mahakamani. Kimsingi mgogoro huu ni wa muda mrefu japo umekua kwa kasi (kufika kwenye media) mara baada ya Katibu Mukhutasi wa Mbunge kumfikisha bosi wake mahakamani kwa madai ya kumdai mshahara. Katika thread iliyohusu kesi ya Machemli na PS wake kuweka hapa jukwaani nilisema kuwa sula hili ni zaidi ya tunavyoliona. Nilisema kuwa nyuma ya kesi hii wapo wanaotamani kugombea ubunge kupitia Chadema.

Niilwataja Malima, Mkundi na Machemli nikihaidi kuingia msituni ili niwajuze yanayoendelea Ukerewe. Nimetoka Msituni….naomba usikivu wenu. Ukweli ni kwamba Ukerewe ni ngome ya Chadema na hata CCM ifanye vipi ni vigumu kulichukua jimbo hili. Katika uchaguzi wa serikali za mitaa Chadema walipata viti 47 kati ya 76, CCM 26 na CUF 3. Watu wa Ukerewe bado wana imani na Chadema, ila wametoa condition moja kuwa, kama Machemli atarejeshwa kugombea basi wajiandae kushindwa. Machemli anajua ukweli huu na hata watia nia wengine. Ukweli huu ndio umeibua mtifuano unaoendelea kwa sasa.

Wako watu wengi wanaotajwa kutaka ubunge. Hata hivyo majina yanayotajwa sana ni Joseph Mkundi (Mwenyekiti wa Halmashari), Martin Malima (Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa) na Machemli. Wengine japo hawatajwi sana ni, Simon Mutobeshya Mabagara (huyu alienguliwa kugombea 2010 kwa madai ya kuwa mamruki wa Mongela, akapewa nafasi Machemli) na jamaa mmoja anayeitwa Mnaku. Naomba nitoe wasifu kidogo wanaotajwa kuutaka ubunge,udhaifu wao na nguvu yao. Salvatory Naluyaga Machemli Huyu ndiye Mbunge wa sasa wa Jimbo la Ukerewe. Hafahamiki sana kama wabunge wengine wa Chadema. Ni mara chache sana kumsikia akiongea bungeni.

Alikuwa kipenzi cha wana-ukerewe, lakini kadri muda unavyokwenda amekuwa akipoteza mvuto. Ni mara chace sana kumuona akifanya mikutano. Kwa kipindi chake cha miaka minne hajaweza kufika katika Kata zote za jimbo. Wananchi wamekuwa vwakimsikia kwenye ‘bomba'. Uwepo wa Halmashauri ya Ukerewe kumesaidia kutunza heshima ya Mbunge kwa kiasi fulani. Kero nyingi za wananchi zimekuwa zikitekelezwa na halmashauri, hasa baada ya kugundua udhaifu wa mbunge. Mwenendo wa kijamii wa mbunge umekuwa hauwafurahishi wengi. Madeni anayodaiwa katika hotel na nyumba za kulala wageni yamekuwa yakikwaza chama. Tabia ya Mbunge ya kupenda ngono na kiasi cha kutolewa katika vyombo vya habari kumewakwaza wengi. Madai ya kupelekwa na PS wake mahakamni kwa issue ya mshahara kumewakwaza wengi pia.

Hata hivyo wanachadema Ukerewe watarajie madai mengi na tuhuma nyingi dhidi ya mbunge wao. Pia Machemri amekuwa haaminiki na Chama Taifa. Tabia yake ya kusaini kitabu cha maudhurio bungeni na baadae kukacha vikao kimekuwa kikiwakwaza viongozi wa Chama Taifa. Machemli anafahamu kuwa jina lake halitarejeshwa hata kama atashinda kura za maoni.

Kabla ya Ukawa, watu walio karibu nae waliwahi kudokeza kuwa alikuwa anfikiria kwenda NCCR kama asingepitishwa na Chama. Kama ni kweli alikuwa na wazo hilo, basi litakwama kutokana na makubaliano na Ukawa. Kwa hali ilivyo Machemli yuko kwenye wakati Mungu. Ndani ya chama Wilaya mchango wa Machemli haujaonekana. Mwonekano wa nje na ndani wa Ofisi ya Chama haoneshi kama Jimbo na Halmashauri viko chini ya Chadema. Mpaka sasa chama hakina hata kiwanja na kina madeni mengi kutokana na kukopa pesa na vyumba vya hotel kwa ajili ya viongozi wa Kitaifa ambao wamekuwa wakifika Ukerewe.

Kwa wanachama hali nako ni tete. Inafikia hatua wanachama kukataa kuchangia gharama za ugeni kwa madai kuwa yuko Mbunge na Mwenyekiti wa Halmashauri. Taarifa kutoka vyanzo vinavyoaminika ni kuwa Ofisi ya Wilaya ilifungwa wiki mbili zilizopita kwa kudaiwa pango. Lawama kubwa zinakwenda kwa Machemli na Mkundi kwa kuonekana kukitekeleza chama. Kwa mwaka uliopita Chama kimepokea wageni wawili wa Kitaifa (Halima Mdee na Salum Mwalim). Ziara hizi zote zimekiachia chama madeni. Huyo ndio Machemli. Joseph Mkundi Ni moja ya viongozi wanaoheshimika katika Chama. Ni motto wa Kada wa Chama cha Mapinduzi ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Ukerewe, Silyvery Mataba. Uongozi wake katika halmashauri umeonesha tofauti kubwa katika ya CDM na CCM.

Amekuwa akisifiwa kwa usikivu hali ambayo imemjengea heshima kwa watu. Hata hivyo heshima ya Mkundi imekuwa ikishuka kadri muda unavyosogea. Hali hii imejitokeza hasa baada ya kutajwa kutaka ubunge. Kutaka kwake ubunge kumeligawa Baraza la Madiwan makundi Mawili/ Matatu.Kundi la moja ni lile linalomuunga mkono yeye na kusadikiwa kumuandalia mazingira ya kugombea ubunge. Katika kundi hili yupo Diwani wa Bwisya (Dismas), Diwani wa Ngoma (Meado), Diwani wa Bukongo (Costa), Diwani wa Bukindo (Toto) na Diwani wa CCM Kataya Nansio (Lamadhani Mazige –Shehe). Mkundi amaekuwa kiwateua madiwani hawa kushiriki semina mbali mbali ndani na nje ya wilaya. Na wengi wao amewateua kuwa kwenye kamati ya Fedha. Kundi la pili linajumuisha madiwani wanaosadikiwa kuwa upande wa Machemli.

Hata hivyo inasadikiwa wengine wanamuunga mkono Malima. Hata hivyo watu waliokaribu na Malima wanadai kuwa Malima hawezi kuwa na kundi katika Baraza la Madiwani kwa kuwa huwa hakutani nao mara kwa mara (Malima anaishi Dar es Salaam). Malima anahusishwa na kundi hili kutokana na uwepo wa Diwani wa Nyamanga, Magesa Simon. Katika kundi hili ambalo ndilo kubwa yuko Diwani wa Ilangara ( jina sijalipata, ila ni mwana mama), Diwani wa Nduruma (White), Diwani wa Namirembe (Matome), Diwani wa Igara (Jose-Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri), Diwani wa Kagunguri (Misana), Diwani wa Bwiro (Leba), Madiwani watano wa Viti Maalumu na Diwani wa Nyamanga (Magesa). Kundi hili ndilo lenye watu wenye ushawishi mkubwa. Na katika uchaguzi wa Makamo Mwenyekiti na wenyeviti wa Kamati walifanikiwa kuwashindisha wagombea katika kundi hili huku wale waliokuwa wakipigiwa upatu na mwenyekiti wakishindwa.

Kundi hili limekuwa likilalamika kutengwa na Mwenyekiti Halmashauri. Mgogoro katika halmashauri ya wilaya ulifikia hatua ya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mwenyekiti. Hali hii ilipelekea Mwenyekiti kuita Kikao cha maridhiano. Hata hivyo kikao hicho hakikusaidia chochote, kwani hali bado ni tete. Katika Uchaguzi wa ndani ya chama ziliibuka tuhuma kuwa Mkundi alitumia rushwa kutaka wagombea wake wapite. Katika uchaguzi huo Mkundi alikuwa anawapigia kampeni Diwani wa Bwisya (Dismas) ambaye alikua anagombea uenyekiti, Paul Mfumu aliye kuwa anatetea ukatibu na Chaurembo aliyekuwa anagombea Wenezi wa Wilaya.

Kati ya hawa wote ni Chaurembo pekee ndie aliyeshinda. Hata hivyo Chaurembo inasemekana kukosa ushawishi. Katika nafasi ya Uenezi alikuwa anagombea pia Diwani wa Nyamanga (Magesa) ambaye Mkundi anadaiwa kutumia nguvu zake zote ili ashinde kwa kuhofia kuwa angemsaidia Malima katika harakati za ubunge.

Mkundi pia amekuwa akihusishwa na CCM. Amekuwa karibu sana Diwani wa Nansio (CCM) Lamadhani Mazige (Shehe) na amemteua kuwa mjumbe wa kamati ya Finance. Shehe amakuwa akimnadi Mkundi kwenye ubunge. Hali hii imekuwa ikizua maswali mengi miongoni mwa wanachadema. Ofisi ya wilaya mpaka sasa haina Ofisi ya kudumu wala kiwanja. Halmashauri ya Wilaya imewahi kugawa viwanja.

Mkundi adaiwa kushindwa kusimamia upatikanaji wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa chama. Mgawanyiko ndani ya halmashauri, ukaribu wake na CCM, tuhuma za rushwa na kushindwa kukisaidia chama kuwa na eneo lake la ofisi/ kiwanja ni kati ya vitu ambavyo vimechangia kumporomosha mkundi kisiasa. Pia Mkundi anadaiwa kutokuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa Chama Wilaya. Anadaiwa kuna wakati amekuwa akikataa kuchangia fedha kwa ajili ya kazi za chama hasa anapokuwa anafuatwa na viomgozi anaoona hawako upande wake.

Tegemeo pekee la Mkundi ni Mzee Slyvester Masinde. Mzee huyu ni moja kati waanzilishi wa Chadema na anadaiwa kuwa na ushawishi mkubwa kwa viongozi wa Chama Taifa. Hata hivyo kushindwa kuchaguliwa tena kwa Mzee Masinde kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chadema kunaweza kuwa kumemuathiri Mkundi kwa namna fulani. Kwa kutokuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, Mzee Masinde anakuwa sio mjumbe wa Kamati kuu. Martin Malima Jina la Malima lilianza kuvuma katika siasa za Ukerewe wakati wa uchaguzi ndani ya chama, japo katika kisiwa cha Ukara (anakotoka) alikuwa akifahamika sana. Hata wakati wa kampeni wapinzani wake waliogopa kumshambulia kwa kuogopa kupoteza kura za Ukara, isipokuwa kundi la Mkundi.

Iikumbukwe kuwa Malima na Mkundi wote wanatoka kisiwa cha Ukara. Katika uchaguzi ndani ya chama Malima aligombea nafasi mbili. Ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya. Katika nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Malima alimshinda kwa kura nyingi Diwani wa Bukongo (Costa) ambaye yuko kundi la Mkundi na katika Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya Malima aliongoza kwa kura nyingi huku akifuatiwa na Wilbourd Machemli (Kaka yake na Machemli) na wagombea wengine akiwemo mzee mmoja kutoka kata ya Mkundi. Kwa tafsiri nyingine Malima alikuwa anagombea na Machemli na Mkundi ambao walimwekea watu. Hata hivyo ushindi wa Malima haukuwa mrahisi. Licha ya Mwenyekiti wa Halmashauri na kundi lake kumuundia tuhuma kua ni Afisa Usalama wa Taifa ambae ametumwa kuvuruga chama Ukerewe Malima alifanikiwa kushinda. Malima amekuwa akifanya siasa za kiungwana.

Licha ya Mwenyekiti wa Halmashauri kumuundia tuhuma mbali mbali na kutuma baadhi ya wanachama kuzunguka kwenye Kata kueneza propaganda za kumuhusisha Zitto Kabwe na Usalama lakini yeye ameendelea kuwa imara zaidi. Hata hivyo wachunguzi wa mambo wanasema kuwa Malima huwezi kumuhusisha na Zitto kwa kuwa amekuwa akimponda Zitto kataika mitandao ya kijamii na magazeti waziwazi. Amekuwa ni mtu wa kujichanganya kwa watu wa rika na jinsia zote. Amekuwa na misimamo ya wazi katika kile anachoamini na amekuwa mjanja sana kutugeuza hoja za uongo dhidi yake kuwa mtaji wake wa kisiasa. Wachunguzi wa siasa za Ukerewe wanasema kuwa wanachadema wengi wanataka mtu jamii ya Malima. Aina yake ya siasa zisizokuwa na makundi na kutochafua wengine zimekuwa zikiwavutia wengi.Malima amekuwa mjanja sana anapoulizwa kama anataka ubunge, japo mwenendo wake wa kisiasa na kijamii unaonesha hivyo.

Pia inasemekana kuwa Malima ana uwezo wa kujieleza na mvuto wa kisiasa zaidi kuliko Mkundi. Pia amekuwa na uungwaji mkubwa sana miongoni mwa vinaja. Yawezekana ni kulingana na ukweli huo ndio maana Red Brigade ilivyozinduliwa rasmi Ukerewe mwaka jana Macheli na Mkundi waliwahi haraka kuwaweka vijana wao. Kamanda wa Red Bregedi, Tito Mangwesi ni Mfuasi Mtiifu wa Machemli na Matroni ni Mfuasi Mtiifu wa Mkundi. Red Brigade hutumiwa na chama kufanya upelelezi na kuandika taarifa za siri kuhusu chama na wanachama. Watia nia huwatumia baadhi ya viongozi wa Red Brigade kuandika taarifa za uongo dhidi ya washindani wao wa kisiasa.

Licha ya Mkundi na Machemli kuikamata Red Brigade, lakini Malima haonekani kushituka sana. Amekuwa karibu na vijana ambao wako kwenye Red Brigade. Waliokaribu nae wanasema wanadai kuwa Malima amekuwa na ukaribu baadhi ya viongozi wa Cahdema Taifa na wajumbe wa Kamati Kuu. Inadaiwa kuwa ujio wa Halima Mdee Salum Mwalim nikutokana na ushawishi wa Malima. Ukaribu huu na viongozi wa Taifa utamsaidia Malima kama Red Brigade ya Ukerewe itatumika kumuundia tuhuma za uongo. Unaweza kujiuliza kama hali ndio hii, kwa nini wanaogombana ni Machemli na Mkundi? Issue ya Machemli na PS wake: Kama nilivyotangulia kusema, Machemli kudaiwa ni kitu cha kawaida na matukio kama haya kumhusu Mbunge yamekuwa ya kawaida sana.

Ni kweli PS anamdai Mbunge, ila swali kujiuliza ni kwa nini wakati huu ndio aibuke kwenda mahakamani? Na kwa nini Mkundi anahusishwa na kuwa nyuma ya PS? Kwa tabia ya Mkundi ya kuogopa ushindani wa kisiasa na kuwaundia wenzake tuhuma na hata kutumia pesa kutimiza matakwa yake ya kisiasa, si ajabu kwake (Mkundi) kuwa katika mchezo huu wenye lengo la kuendelea kummaliza Machemli kisiasa. Ukweli ni huu: Kwanza; Mkundi na Malima wanatoka Ukara. Mkundi anamuona Malima kama tishio kwake. Anahisi kuwa atamnyang'anya kura. Kimsingi huu ndio ukweli, Malima anaushawishi mkubwa kuliko Mkundi. Mkundi hawezi kuthubutu kumsema Malima vibaya Ukara. Pia anahofia kuongeza uhasama na Diwani wa Nyamanga. Diwani wa Nyamanga ana ushawishi mkubwa kisiwani Ukara na ndani ya ile kundi linalohusishwa na Machemli na Mkundi. Machemli pia analifahamu hilo,anahofu kukosana watu wa Ukara kama atampiga vita Malima.

Pili; kwa kuwa Malima anaushawishi kubwa Ukara tegemeo kubwa la Mkundi na Machemli ni Kisiwa kilkubwa cha Ukerewe. Mkundi anapomkimbia Malima Ukara na kuja Kisiwa Kikubwa, hasa tarafa ya Irangala, Machemli anaona kama anaingiliwa. Katika siasa za Ukerewe tarafa za Irangala (anakotoka Machemli) na Ukara ndizo huamua mshindi. Na ndio maana Mkakati wa Mkundi wa kumchafua Malima aliegemea zaidi tarafa ya Irangala. Tatu; inaonekana Machemli na Mkumndi hawana washauri wazuri wa kisiasa.

Haifahamiki Machemli mshauri wake nani? Awali mshauri wake Mkuu alikuwa Katibu wake, lakini inasemekana kuwa Machemli hapatani hata na Katibu wake, anamtuhumu kuwa yuko upande wa Malima. Washauri wa Mkundi ni Diwani wa Ngoma (Meado), ambaye hata hivyo hana ushawishi mkubwa na ni kati ya madiwani ambao CDM inaweza kupoteza kata kama atarejeshwa. Mwingine ni Diwani wa Bwisya (Dismas) ambaye pia uadilifu wake unatia shaka, na hali yake kisiasa katika Kata yake sio nzuri. Wengine ni Diwani wa Bukongo (Costa), Diwani wa Bukindo na aliyekuwa Katibu wa Chama Wilaya (Paul Mfumu).

Pia Mkundi ameonekana mara kwa mara akifanya vikao na kundi la wanachama walijiuzuru uongozi kwa kupinga maamuzi ya Kamati Kuu kumwengua Mutobeshya na kumpitishwa Machemli. Wanachama hawa walifungiwa na chama kujihusisha na shughuli za chama kwa kipindi cha miaka mitano. Watu hawa wote wanadaiwa kutokuwa na ushawishi mkubwa ndani chama.

Hitimisho langu Mgogoro uliopo kati ya Machemli na Mkundi unamufaisha zaidi Malima. Chama hakitakuwa tayari kumpitisha mgombea mwenye Makundi ili kuepuka yakiyotokea Tarime (Heche VS Waitara). Changamoto kubwa aliyonayo Malima hasa katika kipindi hiki ni umbali. Inasemekana Malima anaishi Dar es Salaam. Hii inaweza kumuwia vigumu kwake kupata muda wa kufika Ukerewe kufanya shughuli za kichama.

tutaonana tena.

yaikayaika@yahoo.com
 
Ukweli CHADEMA wakitaka kupoteza kiti cha Ukerewe wamrudishe Machemli. Aje yeyote yule CDM lakini siyo Machemli, kijana kaboronga vilivyo. Ovyo kabisa na ndiye amepunguza ushindi wa CDM kwenye serikali za mitaa. Uongozi ni pamoja na kujiheshimu. Kunywa mipombe na kujiko*******, kupigwa mipicha uchi na wanawake ni moja ya sababu za kumkataa. Kuhusu maendeleo hayo ndo usiseme, hoooooooi kabisa.
 
Baada ya maelezo hayo marefu, tunaomba sasa utuletee Cvs za
  1. Salvatory Machemli
  2. Joseph Mkundi
  3. Martin Malima
 
Ukweli CHADEMA wakitaka kupoteza kiti cha Ukerewe wamrudishe Machemli. Aje yeyote yule CDM lakini siyo Machemli, kijana kaboronga vilivyo. Ovyo kabisa na ndiye amepunguza ushindi wa CDM kwenye serikali za mitaa. Uongozi ni pamoja na kujiheshimu. Kunywa mipombe na kujiko*******, kupigwa mipicha uchi na wanawake ni moja ya sababu za kumkataa. Kuhusu maendeleo hayo ndo usiseme, hoooooooi kabisa.

Uliyoyasema ni kweli mkuu

Nakumbuka Ukerewe ni ngome ya CDM, kwenye Uchaguzi wa 2010 Dr. Slaa alipata kura nyingi kuliko Jakaya Kikwete.

Kama jimbo la Ukerewe litarudi CCM basi itakuwa ni uzembe wa CDM hasa Taifa, ktk kuchagua mtu wa kumsimamisha.
 
Mtu pekee wa kuwakomboa wana ukerewe ni mama Mongela, tabu yote hii imetokana na fitina za msekwa. Bila mongela kurudi jimboni kura za chuki zitaendelea na watu wa ajabu ajabu watachaguliwa.
 
Wana Ukerewe wawe na huruma kwa Machemuli wamrudishe,vinginevyo totoz zake zitammwaga.
 
Yule jamaa amepoteza haiba yake, na kuendelea kumuweka na kumrudisha agombee kutapoteza jombo...

The guy is cazy...
 
Yani ka uliyepost hii habari ni mwanachama wa chadema uko wrong sana,,,uwezi kuweka migogoro ya chama hadharani kama hivi adui watajua mapema wapi pa kuanzia ila ka sio mwanachadema sawa,,,,
 
Umepigia kweli kampeni Malima na umejitahidi sana kuonyesha udhaifu wa Mkundi!
 
Hapa naona umekuja na majungu ili kumpigia debe huyo Malima, watu kama nyie ndio mlisababisha Tarime kupotea. Hebu jiulize kama Mwenyekiti wa halmashauri na mbunge wamechemsha, kwanini CHADEMA washinde serikali za mitaa? Mmeshaona CHADEMA inakubalika hapo basi mnadhani mafanikio hayo yamekuja by chance na mnaanza kuutaka ubunge kwa majungu. Tueleze huyo Malima kakisaidiaje chama mpaka umpigie debe kiasi hicho. Ujenzi wa ofisi za chama sio lazima mtu mmoja awajibike. Kama wengine wameshindwa kuijenga huyo Malima kwanini hakuchukua nafasi hiyo kujitolea kuijenga?
 
Hivi kumbe kama Dr masau asingetangulia mbele za haki kwa hali hii wananchi wa nasio wangemuomba angombee Ubunge huwenda angewaletea maendeleo.
 
Ndugu wanajanmvi!

Kwa wiki kadhaa kumekuwa na habari za kuwepo kwa mgogoro katika ya Mbunge wa Ukerewe Salvatory Naluyaga Machemri na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ukerewe na Diwani wa Kata ya Bukiko, Joseph Mkundi. Kwa wasiofahamu hili wanaweza kudhani kuwa mgogoro huu umeanza baada ya issue ya Rehema kumpeleke Machemli mahakamani. Kimsingi mgogoro huu ni wa muda mrefu japo umekua kwa kasi (kufika kwenye media) mara baada ya Katibu Mukhutasi wa Mbunge kumfikisha bosi wake mahakamani kwa madai ya kumdai mshahara. Katika thread iliyohusu kesi ya Machemli na PS wake kuweka hapa jukwaani nilisema kuwa sula hili ni zaidi ya tunavyoliona. Nilisema kuwa nyuma ya kesi hii wapo wanaotamani kugombea ubunge kupitia Chadema.

Niilwataja Malima, Mkundi na Machemli nikihaidi kuingia msituni ili niwajuze yanayoendelea Ukerewe. Nimetoka Msituni….naomba usikivu wenu. Ukweli ni kwamba Ukerewe ni ngome ya Chadema na hata CCM ifanye vipi ni vigumu kulichukua jimbo hili. Katika uchaguzi wa serikali za mitaa Chadema walipata viti 47 kati ya 76, CCM 26 na CUF 3. Watu wa Ukerewe bado wana imani na Chadema, ila wametoa condition moja kuwa, kama Machemli atarejeshwa kugombea basi wajiandae kushindwa. Machemli anajua ukweli huu na hata watia nia wengine. Ukweli huu ndio umeibua mtifuano unaoendelea kwa sasa.

Wako watu wengi wanaotajwa kutaka ubunge. Hata hivyo majina yanayotajwa sana ni Joseph Mkundi (Mwenyekiti wa Halmashari), Martin Malima (Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa) na Machemli. Wengine japo hawatajwi sana ni, Simon Mutobeshya Mabagara (huyu alienguliwa kugombea 2010 kwa madai ya kuwa mamruki wa Mongela, akapewa nafasi Machemli) na jamaa mmoja anayeitwa Mnaku. Naomba nitoe wasifu kidogo wanaotajwa kuutaka ubunge,udhaifu wao na nguvu yao. Salvatory Naluyaga Machemli Huyu ndiye Mbunge wa sasa wa Jimbo la Ukerewe. Hafahamiki sana kama wabunge wengine wa Chadema. Ni mara chache sana kumsikia akiongea bungeni.

Alikuwa kipenzi cha wana-ukerewe, lakini kadri muda unavyokwenda amekuwa akipoteza mvuto. Ni mara chace sana kumuona akifanya mikutano. Kwa kipindi chake cha miaka minne hajaweza kufika katika Kata zote za jimbo. Wananchi wamekuwa vwakimsikia kwenye ‘bomba'. Uwepo wa Halmashauri ya Ukerewe kumesaidia kutunza heshima ya Mbunge kwa kiasi fulani. Kero nyingi za wananchi zimekuwa zikitekelezwa na halmashauri, hasa baada ya kugundua udhaifu wa mbunge. Mwenendo wa kijamii wa mbunge umekuwa hauwafurahishi wengi. Madeni anayodaiwa katika hotel na nyumba za kulala wageni yamekuwa yakikwaza chama. Tabia ya Mbunge ya kupenda ngono na kiasi cha kutolewa katika vyombo vya habari kumewakwaza wengi. Madai ya kupelekwa na PS wake mahakamni kwa issue ya mshahara kumewakwaza wengi pia.

Hata hivyo wanachadema Ukerewe watarajie madai mengi na tuhuma nyingi dhidi ya mbunge wao. Pia Machemri amekuwa haaminiki na Chama Taifa. Tabia yake ya kusaini kitabu cha maudhurio bungeni na baadae kukacha vikao kimekuwa kikiwakwaza viongozi wa Chama Taifa. Machemli anafahamu kuwa jina lake halitarejeshwa hata kama atashinda kura za maoni.

Kabla ya Ukawa, watu walio karibu nae waliwahi kudokeza kuwa alikuwa anfikiria kwenda NCCR kama asingepitishwa na Chama. Kama ni kweli alikuwa na wazo hilo, basi litakwama kutokana na makubaliano na Ukawa. Kwa hali ilivyo Machemli yuko kwenye wakati Mungu. Ndani ya chama Wilaya mchango wa Machemli haujaonekana. Mwonekano wa nje na ndani wa Ofisi ya Chama haoneshi kama Jimbo na Halmashauri viko chini ya Chadema. Mpaka sasa chama hakina hata kiwanja na kina madeni mengi kutokana na kukopa pesa na vyumba vya hotel kwa ajili ya viongozi wa Kitaifa ambao wamekuwa wakifika Ukerewe.

Kwa wanachama hali nako ni tete. Inafikia hatua wanachama kukataa kuchangia gharama za ugeni kwa madai kuwa yuko Mbunge na Mwenyekiti wa Halmashauri. Taarifa kutoka vyanzo vinavyoaminika ni kuwa Ofisi ya Wilaya ilifungwa wiki mbili zilizopita kwa kudaiwa pango. Lawama kubwa zinakwenda kwa Machemli na Mkundi kwa kuonekana kukitekeleza chama. Kwa mwaka uliopita Chama kimepokea wageni wawili wa Kitaifa (Halima Mdee na Salum Mwalim). Ziara hizi zote zimekiachia chama madeni. Huyo ndio Machemli. Joseph Mkundi Ni moja ya viongozi wanaoheshimika katika Chama. Ni motto wa Kada wa Chama cha Mapinduzi ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Ukerewe, Silyvery Mataba. Uongozi wake katika halmashauri umeonesha tofauti kubwa katika ya CDM na CCM.

Amekuwa akisifiwa kwa usikivu hali ambayo imemjengea heshima kwa watu. Hata hivyo heshima ya Mkundi imekuwa ikishuka kadri muda unavyosogea. Hali hii imejitokeza hasa baada ya kutajwa kutaka ubunge. Kutaka kwake ubunge kumeligawa Baraza la Madiwan makundi Mawili/ Matatu.Kundi la moja ni lile linalomuunga mkono yeye na kusadikiwa kumuandalia mazingira ya kugombea ubunge. Katika kundi hili yupo Diwani wa Bwisya (Dismas), Diwani wa Ngoma (Meado), Diwani wa Bukongo (Costa), Diwani wa Bukindo (Toto) na Diwani wa CCM Kataya Nansio (Lamadhani Mazige –Shehe). Mkundi amaekuwa kiwateua madiwani hawa kushiriki semina mbali mbali ndani na nje ya wilaya. Na wengi wao amewateua kuwa kwenye kamati ya Fedha. Kundi la pili linajumuisha madiwani wanaosadikiwa kuwa upande wa Machemli.

Hata hivyo inasadikiwa wengine wanamuunga mkono Malima. Hata hivyo watu waliokaribu na Malima wanadai kuwa Malima hawezi kuwa na kundi katika Baraza la Madiwani kwa kuwa huwa hakutani nao mara kwa mara (Malima anaishi Dar es Salaam). Malima anahusishwa na kundi hili kutokana na uwepo wa Diwani wa Nyamanga, Magesa Simon. Katika kundi hili ambalo ndilo kubwa yuko Diwani wa Ilangara ( jina sijalipata, ila ni mwana mama), Diwani wa Nduruma (White), Diwani wa Namirembe (Matome), Diwani wa Igara (Jose-Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri), Diwani wa Kagunguri (Misana), Diwani wa Bwiro (Leba), Madiwani watano wa Viti Maalumu na Diwani wa Nyamanga (Magesa). Kundi hili ndilo lenye watu wenye ushawishi mkubwa. Na katika uchaguzi wa Makamo Mwenyekiti na wenyeviti wa Kamati walifanikiwa kuwashindisha wagombea katika kundi hili huku wale waliokuwa wakipigiwa upatu na mwenyekiti wakishindwa.

Kundi hili limekuwa likilalamika kutengwa na Mwenyekiti Halmashauri. Mgogoro katika halmashauri ya wilaya ulifikia hatua ya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mwenyekiti. Hali hii ilipelekea Mwenyekiti kuita Kikao cha maridhiano. Hata hivyo kikao hicho hakikusaidia chochote, kwani hali bado ni tete. Katika Uchaguzi wa ndani ya chama ziliibuka tuhuma kuwa Mkundi alitumia rushwa kutaka wagombea wake wapite. Katika uchaguzi huo Mkundi alikuwa anawapigia kampeni Diwani wa Bwisya (Dismas) ambaye alikua anagombea uenyekiti, Paul Mfumu aliye kuwa anatetea ukatibu na Chaurembo aliyekuwa anagombea Wenezi wa Wilaya.

Kati ya hawa wote ni Chaurembo pekee ndie aliyeshinda. Hata hivyo Chaurembo inasemekana kukosa ushawishi. Katika nafasi ya Uenezi alikuwa anagombea pia Diwani wa Nyamanga (Magesa) ambaye Mkundi anadaiwa kutumia nguvu zake zote ili ashinde kwa kuhofia kuwa angemsaidia Malima katika harakati za ubunge.

Mkundi pia amekuwa akihusishwa na CCM. Amekuwa karibu sana Diwani wa Nansio (CCM) Lamadhani Mazige (Shehe) na amemteua kuwa mjumbe wa kamati ya Finance. Shehe amakuwa akimnadi Mkundi kwenye ubunge. Hali hii imekuwa ikizua maswali mengi miongoni mwa wanachadema. Ofisi ya wilaya mpaka sasa haina Ofisi ya kudumu wala kiwanja. Halmashauri ya Wilaya imewahi kugawa viwanja.

Mkundi adaiwa kushindwa kusimamia upatikanaji wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa chama. Mgawanyiko ndani ya halmashauri, ukaribu wake na CCM, tuhuma za rushwa na kushindwa kukisaidia chama kuwa na eneo lake la ofisi/ kiwanja ni kati ya vitu ambavyo vimechangia kumporomosha mkundi kisiasa. Pia Mkundi anadaiwa kutokuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa Chama Wilaya. Anadaiwa kuna wakati amekuwa akikataa kuchangia fedha kwa ajili ya kazi za chama hasa anapokuwa anafuatwa na viomgozi anaoona hawako upande wake.

Tegemeo pekee la Mkundi ni Mzee Slyvester Masinde. Mzee huyu ni moja kati waanzilishi wa Chadema na anadaiwa kuwa na ushawishi mkubwa kwa viongozi wa Chama Taifa. Hata hivyo kushindwa kuchaguliwa tena kwa Mzee Masinde kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chadema kunaweza kuwa kumemuathiri Mkundi kwa namna fulani. Kwa kutokuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, Mzee Masinde anakuwa sio mjumbe wa Kamati kuu. Martin Malima Jina la Malima lilianza kuvuma katika siasa za Ukerewe wakati wa uchaguzi ndani ya chama, japo katika kisiwa cha Ukara (anakotoka) alikuwa akifahamika sana. Hata wakati wa kampeni wapinzani wake waliogopa kumshambulia kwa kuogopa kupoteza kura za Ukara, isipokuwa kundi la Mkundi.

Iikumbukwe kuwa Malima na Mkundi wote wanatoka kisiwa cha Ukara. Katika uchaguzi ndani ya chama Malima aligombea nafasi mbili. Ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya. Katika nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Malima alimshinda kwa kura nyingi Diwani wa Bukongo (Costa) ambaye yuko kundi la Mkundi na katika Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya Malima aliongoza kwa kura nyingi huku akifuatiwa na Wilbourd Machemli (Kaka yake na Machemli) na wagombea wengine akiwemo mzee mmoja kutoka kata ya Mkundi. Kwa tafsiri nyingine Malima alikuwa anagombea na Machemli na Mkundi ambao walimwekea watu. Hata hivyo ushindi wa Malima haukuwa mrahisi. Licha ya Mwenyekiti wa Halmashauri na kundi lake kumuundia tuhuma kua ni Afisa Usalama wa Taifa ambae ametumwa kuvuruga chama Ukerewe Malima alifanikiwa kushinda. Malima amekuwa akifanya siasa za kiungwana.

Licha ya Mwenyekiti wa Halmashauri kumuundia tuhuma mbali mbali na kutuma baadhi ya wanachama kuzunguka kwenye Kata kueneza propaganda za kumuhusisha Zitto Kabwe na Usalama lakini yeye ameendelea kuwa imara zaidi. Hata hivyo wachunguzi wa mambo wanasema kuwa Malima huwezi kumuhusisha na Zitto kwa kuwa amekuwa akimponda Zitto kataika mitandao ya kijamii na magazeti waziwazi. Amekuwa ni mtu wa kujichanganya kwa watu wa rika na jinsia zote. Amekuwa na misimamo ya wazi katika kile anachoamini na amekuwa mjanja sana kutugeuza hoja za uongo dhidi yake kuwa mtaji wake wa kisiasa. Wachunguzi wa siasa za Ukerewe wanasema kuwa wanachadema wengi wanataka mtu jamii ya Malima. Aina yake ya siasa zisizokuwa na makundi na kutochafua wengine zimekuwa zikiwavutia wengi.Malima amekuwa mjanja sana anapoulizwa kama anataka ubunge, japo mwenendo wake wa kisiasa na kijamii unaonesha hivyo.

Pia inasemekana kuwa Malima ana uwezo wa kujieleza na mvuto wa kisiasa zaidi kuliko Mkundi. Pia amekuwa na uungwaji mkubwa sana miongoni mwa vinaja. Yawezekana ni kulingana na ukweli huo ndio maana Red Brigade ilivyozinduliwa rasmi Ukerewe mwaka jana Macheli na Mkundi waliwahi haraka kuwaweka vijana wao. Kamanda wa Red Bregedi, Tito Mangwesi ni Mfuasi Mtiifu wa Machemli na Matroni ni Mfuasi Mtiifu wa Mkundi. Red Brigade hutumiwa na chama kufanya upelelezi na kuandika taarifa za siri kuhusu chama na wanachama. Watia nia huwatumia baadhi ya viongozi wa Red Brigade kuandika taarifa za uongo dhidi ya washindani wao wa kisiasa.

Licha ya Mkundi na Machemli kuikamata Red Brigade, lakini Malima haonekani kushituka sana. Amekuwa karibu na vijana ambao wako kwenye Red Brigade. Waliokaribu nae wanasema wanadai kuwa Malima amekuwa na ukaribu baadhi ya viongozi wa Cahdema Taifa na wajumbe wa Kamati Kuu. Inadaiwa kuwa ujio wa Halima Mdee Salum Mwalim nikutokana na ushawishi wa Malima. Ukaribu huu na viongozi wa Taifa utamsaidia Malima kama Red Brigade ya Ukerewe itatumika kumuundia tuhuma za uongo. Unaweza kujiuliza kama hali ndio hii, kwa nini wanaogombana ni Machemli na Mkundi? Issue ya Machemli na PS wake: Kama nilivyotangulia kusema, Machemli kudaiwa ni kitu cha kawaida na matukio kama haya kumhusu Mbunge yamekuwa ya kawaida sana.

Ni kweli PS anamdai Mbunge, ila swali kujiuliza ni kwa nini wakati huu ndio aibuke kwenda mahakamani? Na kwa nini Mkundi anahusishwa na kuwa nyuma ya PS? Kwa tabia ya Mkundi ya kuogopa ushindani wa kisiasa na kuwaundia wenzake tuhuma na hata kutumia pesa kutimiza matakwa yake ya kisiasa, si ajabu kwake (Mkundi) kuwa katika mchezo huu wenye lengo la kuendelea kummaliza Machemli kisiasa. Ukweli ni huu: Kwanza; Mkundi na Malima wanatoka Ukara. Mkundi anamuona Malima kama tishio kwake. Anahisi kuwa atamnyang'anya kura. Kimsingi huu ndio ukweli, Malima anaushawishi mkubwa kuliko Mkundi. Mkundi hawezi kuthubutu kumsema Malima vibaya Ukara. Pia anahofia kuongeza uhasama na Diwani wa Nyamanga. Diwani wa Nyamanga ana ushawishi mkubwa kisiwani Ukara na ndani ya ile kundi linalohusishwa na Machemli na Mkundi. Machemli pia analifahamu hilo,anahofu kukosana watu wa Ukara kama atampiga vita Malima.

Pili; kwa kuwa Malima anaushawishi kubwa Ukara tegemeo kubwa la Mkundi na Machemli ni Kisiwa kilkubwa cha Ukerewe. Mkundi anapomkimbia Malima Ukara na kuja Kisiwa Kikubwa, hasa tarafa ya Irangala, Machemli anaona kama anaingiliwa. Katika siasa za Ukerewe tarafa za Irangala (anakotoka Machemli) na Ukara ndizo huamua mshindi. Na ndio maana Mkakati wa Mkundi wa kumchafua Malima aliegemea zaidi tarafa ya Irangala. Tatu; inaonekana Machemli na Mkumndi hawana washauri wazuri wa kisiasa.

Haifahamiki Machemli mshauri wake nani? Awali mshauri wake Mkuu alikuwa Katibu wake, lakini inasemekana kuwa Machemli hapatani hata na Katibu wake, anamtuhumu kuwa yuko upande wa Malima. Washauri wa Mkundi ni Diwani wa Ngoma (Meado), ambaye hata hivyo hana ushawishi mkubwa na ni kati ya madiwani ambao CDM inaweza kupoteza kata kama atarejeshwa. Mwingine ni Diwani wa Bwisya (Dismas) ambaye pia uadilifu wake unatia shaka, na hali yake kisiasa katika Kata yake sio nzuri. Wengine ni Diwani wa Bukongo (Costa), Diwani wa Bukindo na aliyekuwa Katibu wa Chama Wilaya (Paul Mfumu).

Pia Mkundi ameonekana mara kwa mara akifanya vikao na kundi la wanachama walijiuzuru uongozi kwa kupinga maamuzi ya Kamati Kuu kumwengua Mutobeshya na kumpitishwa Machemli. Wanachama hawa walifungiwa na chama kujihusisha na shughuli za chama kwa kipindi cha miaka mitano. Watu hawa wote wanadaiwa kutokuwa na ushawishi mkubwa ndani chama.

Hitimisho langu Mgogoro uliopo kati ya Machemli na Mkundi unamufaisha zaidi Malima. Chama hakitakuwa tayari kumpitisha mgombea mwenye Makundi ili kuepuka yakiyotokea Tarime (Heche VS Waitara). Changamoto kubwa aliyonayo Malima hasa katika kipindi hiki ni umbali. Inasemekana Malima anaishi Dar es Salaam. Hii inaweza kumuwia vigumu kwake kupata muda wa kufika Ukerewe kufanya shughuli za kichama.

tutaonana tena.

yaikayaika@yahoo.com

Hii habari ni ya Kupika,,,,na Mpikaji hajui kupika....angalia nilipoweka BOLD
 
CHADEMA inao utaratibu wake kikatiba wa kuwapata wagombea, wala hapa si mahali pake kuelezea kurasa zako, yafikishe huko huko kwenye vikao husika vya chama ukweli utapatikana huko,
 
Badala ya kujenga chama mnaleta migogoro. Piga chini wote
 
Hii habari ni ya Kupika,,,,na Mpikaji hajui kupika....angalia nilipoweka BOLD
nadhani hapo litakuwa ni typing error tu. kama sikosei alikuwa anamaanisha mwita na chacha (former MP) na sio henche.
 
Watu wa Ukerewe bhana yaani mnapata mafanikio kwenye chaguzi serikali za mitaa badala ya kuamua kimya kimya mnaanza kupiga kelele. Vigezo vyenu vimekaaje
 
machemli hana sifa ya kuendelea kuwa mbunge , hajitambui wala haeleweki, chadema wakitaka kupoteza hilo jimbo wamrudishe machemli,
Mr makundi anafaa sana kuteuliwa na chadema kugombea, na naamini akiteuliwa atashinda
 
Back
Top Bottom