MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,432
Wakuu,
Nahisi wengi hawajafuatilia kwa karibu "vita" inayoendelea kwenye makanisa ya kiroho. Hivi karibuni Askofu Kakobe, Mtume Fenenard (yule wa Agape) na Askofu Gamanywa waliunda umoja wao na kuuita Jukwaa la kumuhubiri Kristo na siku ya uzinduzi waliponda mno huduma za sasa hasa manabii ikiwemo kuuzwa kwa mafuta na maji ya upako.
Kakobe alifikia hatua kuitaka serikali kukusanya kodi kwa manabii wanaouza maji na mafuta ya upako maana ni biashara kabisa na kinyume cha maandiko
Nimefatilia matamko ya hilo jukwaa la kumuhubiri Kristo nikaona video ambayo walikuwa wakifafanua kusudi la jukwaa hilo na pia waliweka sauti za watu walioibuka kuwajibu na kujibu hoja zao (nenda YouTube utakuta mengi zaidi).
Leo nimeona limeitishwa kongamano la huduma zote tano likiongozwa na akina Askofu Gwajima, Mwingira na wahudhuriaji wengi akiwemo akina Mwamposa n.k
Hili kongamano lilishasemwa kuandaliwa kuwajibu akina Kakobe ( ukisikiliza majibu ya akina Kakobe) na kweli limefanyika.
Ni dhahiri kuna mgawanyiko mkubwa, si kawaida kuona mtu kama Askofu Gwajima akiwa kinyume na mtu anayemwita baba yake kiroho yaani Kakobe.
Kwanza kama Roho ni yule yule hawezi kufunulia watu wake mafunuo yanayopingana. Huku kupingana ni dalili dhahiri ya kazi ya yule mwovu.
Mimi ni Mkatoliki na sipo hapa kupinga imani za wengine zaidi nawaombea umoja kama jinsi kila misa lazima tuombee umoja wa kanisa. Umoja wa Kanisa ni moja ya sala ambayo Kristo aliombea kanisa lake.
Maandiko yanasema nyinyi ni chumvi na chumvi ikiishiwa utamu itakolezwa na nini? Kama mnashindwa kuambiana ukweli kama Paulo alivyomkosoa Petro wazi nani awasuluhishe? Kiburi cha kiroho?
Itakuwa aibu mtapokuja kusuluhishwa na wanasiasa, tumieni umoja wenu rasmi unaotambuliwa na serikali kuainisha ukweli juu ya huduma zenye utata na mueleze ukweli ili watu wataoamua kwenda huko waende wakijua kweli.
Hizi link zitawasaidia wanaotaka kufatilia zaidi huu mtifuano mkali.