Mti wa maajabu unavyoanguka

Mti wa maajabu unavyoanguka

mapenzi hasara

Senior Member
Joined
Feb 28, 2020
Posts
102
Reaction score
275
Nami nikaona mti mkubwa Sana unaotoa nuru upande mmoja na upande mwingine wa mti kuna Giza totoro.

Nami nikaona wamiliki wa mti huu wakiwaonesha wanakijiji upande mmoja wa nuru na kuwaficha upande mwingine wa Giza.

Nami nikaona upande wa Nuru wa mti ukizidiwa na Giza kuanza kutanda katika kijiji husika.

Wanakijiji wanapojaribu kuukata ule mti wanatishwa na wamiliki, Kwa kuwaua na kuwashtaki Kwa kuwapa kesi zisizowahusu.

Nikaona Giza likitanda na hatimae upande wa mwanga ukapotea mara wanakijiji wakihangaika kupata mwanga Kwa miaka kadhaa bila mafanikio huku maamuzi yote yakifanywa bila kushirikishwa wanakijiji.

Nikaona wanakijiji wako kimya wakiwa wamefunga midomo wamekaa katika Giza totoro, wanakijiji wamekosa tumaini nalo limepotea kabisa wakiwa wanalia mbele za Mungu juu Giza katika kijiji.

Nami nikaona wingu likifunguka mwanga mkali kutoka mawinguni ukilipiga ule mti mkubwa utoao kiza kinene, nao mwanga ukalishinda kiza na kukausha kabisa ule.

Nami nikaona mti ukikauka wamiliki wakikimbia na kukana umiliki wa mti ule, nikaona mti ukiondoka taraibu baada ya kumaishwa na mwanga kutoka mawinguni.

Mwisho nikaona wanakijiji wanavyofurahia kuondoka kwa ule mti na kuna kwa mwanga.
 
Chadema wamua kuja na nitoke vipi ya kilozi
Kukosa ajenda kazi kwelikweli
 
Tanzania amani daima,
natumai hakutakuwa na upizani wa vya vyama tena na tutarudisha mfumo wa chama kimoja
 
Back
Top Bottom