Mtili wandu
JF-Expert Member
- Dec 15, 2012
- 9,293
- 12,874
Aisee haya keshooooo
Sijasoma ila nimesikitika sana.14 August 2012: DUMILA; MOROGORO
Nilikuwa nimetimiza wiki mbili ndani ya Dumila, mji mdogo unaounda kata za wilaya ya Kilosa.
Kilosa ni moja kati ya wilaya zinazounganisha Mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania. Harakati zangu za kupambana kufubaza makali ya ugumu wa maisha, ndizo zilizonifikisha hapo.
Kwa zaidi ya wiki mbili, nilikuwa nikizunguka toka kijiji kimoja hadi kingine, nikikusanya mazao ya chakula. Hii ilikuwa biashara niliyojikita kwa zaidi ya miaka miwili tangu nilipoachana na ajira rasmi.
Nilinunua nafaka toka kwa wakulima wadogo vijijini na kuyahifadhi kwa muda katika ghala ndogo iliyopo Dumila. Baadaye niliyasafirisha mpaka jijini Dar es salaam, nilipoyauza kwa bei ya juu kidogo na kupata faida iliyonisaidia kusogeza siku.
Katika safari hizo, nilikutana na simulizi ya kusisimua kutoka kwa msichana wa miaka kumi na sita katika kijiji kimoja nilichotembelea. Msichana huyo aliishi na watoto wawili wa kiume wenye asili ya Kiholanzi katika mazingira duni ya kijiji kiitwacho Matale.
Kilichonishangaza zaidi ni namna walivyoonekana kuwa na uhusiano wa karibu; waliishi kama mapacha watatu, wakiwa na mshikamano wa kushangaza kila walipopita.
Maswali mengi yalinijia kichwani; Ilikuwaje msichana huyu akaishi na watoto wa kizungu katika kijiji cha ndani kama hiki? Wazazi wa wavulana hao walikuwa wapi? Uhusiano wao ulitokana na nini?
Nilipowadadisi wenyeji, nilipata fununu kwamba wavulana hao walikuwa raia wa Uholanzi lakini msichana alikuwa Mtanzania, mzaliwa wa Dumila. Hata hivyo katika hali ya kushangaza, hakuna aliyefahamu kwa hakika chanzo cha uhusiano wao wala sababu iliyopelekea waishi pamoja.
Kwa asili yangu ya udadisi, sikuweza kuondoka kijijini hapo bila kufahamu ukweli. Nilihisi kuna siri nzito nyuma ya maisha ya msichana huyo na hao watoto wawili.
Kama mtu ambaye daima hunyemelea simulizi zisizo za kawaida, sikuweza kuondoka bila kutanzua fumbo hili. Lakini haikuwa kazi rahisi. Msichana huyo alikuwa mkimya na mgumu kumzoea. Ilibidi nivute subira, nikitafuta jinsi ya kujenga mazoea na uaminifu kwake.
Hatimaye baada ya juhudi na uvumilivu, alikubali kunieleza historia yake. Tulipata wasaa adimu wa kufanya mazungumzo kwa siri. Ndipo akafunguka kuhusu historia nzima ya maisha yake na jinsi alivyokutakana na hao watoto.
Simulizi yake iliniacha katika taharuki nzito. Nilijikuta nikiamini kwa dhati, kuwa dunia hii imebeba mambo mazito, yanayostaajabisha na kutisha kuliko unavyoweza kudhani.
Endelea kufuatilia.....
Sijasoma ila nimesikitika sa14 August 2012: DUMILA; MOROGORO

CHAI HAIJAIVA KANYWE MWENYEWE.14 August 2012: DUMILA; MOROGORO

Kunywa tu hivyo hivyo ukiwa wa motoUrojo si urojo chai si chai
Hii Chai ina hadi vitunguu,hoho, binaries nyembamba mixer na ubuyu. Kwa kifupi hainyweki hata ujikaze vipi.14 August 2012: DUMILA; MOROGORO

SURA YA KWANZA:View attachment 3295431
Alikuwa msichana mdogo, mwenye sura nzuri na haiba ya upole lakini iliyobeba matumaini ya siku za usoni.
Salome aliishi na bibi yake katika mji mdogo wa Dumila katika hali ya ufukara na upweke mkubwa. Hata mtaa walioishi uliakisi umaskini na hali duni ya familia nyingi. Ulikuwa mtaa wenye vumbi jingi, nyumba chakavu zilizoinamisha paa, na watoto wengi waliovaa nguo kuukuu kiasi cha kufifisha haiba yao ya utoto.
Bibi yake ambaye pia aliitwa Salome, alikuwa kila kitu maishani mwake. Msichana huyu hakuwahi kumjua mama yake mzazi, kwani mama yake alitoweka Dumila zamani sana na kwenda kuishi jijini Dar es salaam.
Salome alipokuwa mdogo zaidi, aliwahi kumuuliza bibi yake kuhusu mama yake. “Bibi, kwani mama yangu yuko wapi? Mbona huwa haji kutuona?” Lakini bibi huyo alimjibu kwa sauti ya upole, “Baadhi ya mambo huwezi kuyaelewa mjukuu wangu. Tumuachie tu Mungu.”
Salome ni mfano wa watoto wengi waliotelekezwa kwa bibi zao baada ya kuzaliwa na mama ambaye hakuwa tayari kubeba mzigo wa malezi.
Mama yake alifahamika kwa jina la Sauda; mwanamke aliyezaliwa na tunu ya urembo wa kupendeza, lakini aliyekosa hekima na maono ya kujiongoza kimaisha. Urembo wake haukuwa baraka, bali mkosi uliozidi kumzamisha katika tope la maangamizi.
Sauda alikulia katika familia yenye mapungufu. Hakuwahi kumjua baba yake, na malezi ya upande mmoja kutoka kwa mama asiye na nguvu wala mamlaka ya kumwekea mipaka, yalichangia mno kupotoka kwake. Ulimwengu ulianza kumbadilisha pale tu alipoanza kubaleghe. Uzuri wake ukageuka kuwa silaha iliyomkabili yeye mwenyewe.
Na kwa kukosa mwongozo thabiti alijikuta akiyumbishwa na tamaa za dunia. Ndiyo maana haikushangaza majirani pale aliponasa ujauzito akiwa na umri wa miaka kumi na tano tu.
Walioamini kuwa hilo lingempa funzo walijidanganya. Miezi michache baada ya kujifungua, Sauda alimtoroka mama yake akimuacha na jukumu la kulea mjukuu asiye na baba.
Jina la baba wa mtoto huyo lilibaki kuwa kitendawili, huku wanaume watatu wakizua mzozo uliowavunjia heshima. Mmoja akiwa dereva wa malori, mwingine mfanyabiashara maarufu wa duka la jumla, na wa tatu alikuwa askari polisi kijana.
Hofu ya kugonganisha wanaume hao, ilimkimbiza Dumila na kwenda kujificha mjini Morogoro. Na akiwa huko, maisha yalimuonyesha njia mbaya zaidi.
Akiwa amejaribu kazi ya ubaamedi mara mbili, aliuona mshahara wa shilingi elfu sabini kwa mwezi kama mzaha; kwani aliweza kupata kiasi hicho cha pesa kwa kulala na wanaume wawili au watatu kwa usiku mmoja.
Ndoto yake ilikuwa moja tu: kufika kwenye nchi ya ahadi kwa urahisi, bila kupitia mawimbi ya maisha.
Baada ya mwaka mmoja wa hekaheka, uzuri wake ulififia, wanaume wakamkwepa na kuelekeza macho yao kwa wasichana wapya waliotafuta nafasi katika biashara hiyo chafu. Kwa kujiona hana soko, Sauda akakimbilia Dar es Salaam – jiji la anasa na tafrija zisizokoma.
Na kweli, jiji halikumkatisha tamaa. Lilimkumbatia kwa mikono miwili na ndani ya muda mfupi akawa kipenzi cha wanaume wenye pesa, ingawa kila fedha iliyopita mikononi mwake ilipitiliza kwenye vipodozi, mavazi na nywele za bei mbaya, akihakikisha uzuri wake hauchuji tena. Hakuwaza kingine nje ya urembo wake na starehe.
Usiku ukawa uwanja wake wa maisha. Ukienda kwenye baa yoyote maarufu jijini Dar es Salaam, ilikuwa lazima umkute Sauda. Alibadili wanaume kama mtu anavyobadilisha mavazi, mpaka siku alipojikuta amenasa ujauzito mwingine, bila kujua nani hasa aliyehusika.
Safari hii alitumia ujanja. Alimtwisha mzigo huo kijana mmoja mtulivu aliyekuwa afisa ugavi katika shirika moja la umma. Kijana huyo asiye na uzoefu na hila za wanawake kama Sauda, alimkubali na kuishi naye kama mke.
Lakini wahenga walisema: “Kunguru hafugiki.” Miaka miwili ya fumanizi, fedheha, na ufuska wa kutisha ilitosha kumfanya mumewe achoke. Alipogundua uozo wake kimaadili na historia ya kutatanisha nyuma yake, kijana huyo alimfukuza Sauda kama mbwa.
Sauda aliomboleza kwa siku mbili tu, lakini ya tatu ilimkuta akiwa mkavu, amesharudi kwenye maisha yake ya zamani. Shoga yake alimpa hifadhi katika chumba cha kupanga huko Tandale kwa Mtogole. Mwezi mmoja baadaye, mtoto wake mchanga alifariki dunia kwa maradhi ya nimonia, kutokana na malezi duni na mazingira machafu.
Baada ya pigo hilo, Sauda alifanya ukahaba kwa namna ya kutisha, kana kwamba alikuwa akijiadhibu mwenyewe. Mwenye elfu kumi twende, elfu tano haachi. Alipopata mimba Mwananyamala, alienda kuichoropoa Temeke. Ulevi uliokithiri na matumizi ya mihadarati vilimtoa kabisa kwenye reli ya maisha.
Mimba yake ya tano—ukiachilia mbali zile nne alizozitoa awali—ndiyo iliyoondoka na uhai wake. Alienda kuitoa kwa daktari mmoja aliyesifika kwa huduma hiyo haramu huko Mburahati.
Masaa machache baada ya kumaliza zoezi hilo, mwili wake ulianza kuvuja damu isiyozuilika. Daktari huyo akihofia kuhusishwa na kifo chake, alimtelekeza.
Taratibu Sauda alizidi kulegea, macho yakabadilika rangi, na mwishowe alikata kauli. Hadithi ya maisha yake iliishia hapo.
Safari Ya Matumani:
Huko Dumila, Bi Salome aliendelea kulea kijukuu chake kwa upendo wa dhati, licha ya dhiki na ugumu wa maisha. Alimpa jina la Salome, akilitunza jina lake mwenyewe kwa heshima. Naye Salome mdogo akaendelea kukua, akistawi si tu katika kimo, bali pia hekima na maadili.
Shughuli za kilimo alizotegemea, hazikumwezesha bibi huyu kufanya makubwa zaidi ya kumudu chakula na gharama ndogo ndogo za maisha. Ndiyo maana mjukuu wake alipomaliza darasa la saba, Bi Salome hakuwa na uwezo wa kugharamia elimu yake ya sekondari. Safari yake ya kutafuta elimu ikawa imefikia ukingoni. Akaungana na bibi yake kupambana na maisha yasiyo na huruma.
Siku moja, bibi huyo alipata kazi ya usimamizi wa nyumba katika familia ya mfanyabiashara maarufu Dumila, Mzee Saidi Ali Omar, aliyekuwa na asili ya kiarabu.
Mzee Saidi akiwa na miaka 65, alikuwa mtu wa kuheshimika Dumila kwa sababu ya ukarimu na uungwana wake. Alimchukua Bi Salome na mjukuu wake kama sehemu ya familia yake, akiwapa ujira mzuri pamoja na msaada wa mara kwa mara uliowapunguzia baadhi ya changamoto za maisha. Wakawa wakifanya kazi kutwa na kurudi nyumbani kwao jioni.
Kwa ujira wa shilingi elfu themanini kwa mwezi, na marupurupu ya nyongeza kila mara, Bi Salome alijihisi kama mtu mwenye bahati ya mtende, kupata chemchemi jangwani. Nyuso zao zikapata nuru kwa matumaini ya kesho iliyo bora.
Miaka ilivyopita, Ali, mtoto mkubwa wa Mzee Saidi, alipata taarifa kuhusu nafasi ya kazi za ndani kutoka kwa mkulima mmoja mkubwa wa miti, mzungu mwenye asili ya Uholanzi, aliyekuwa akiishi peke yake katikati ya mashamba yake makubwa.
Ali alikuwa amefahamiana na mzungu huyo kupitia biashara zao, hivyo aliamua kumwombea Salome nafasi hiyo akijua jinsi hali yao ilivyokuwa duni.
Jioni hiyo baada ya kazi za mchana kuchwa, Ali alimfuata Bi Salome na kumweleza kuhusu nafasi hiyo adhimu. Bi Salome hakuwa na shaka yoyote, alipokea habari hiyo kwa moyo wa shukrani na furaha isiyofichika. Waliporejea nyumbani, aliharakisha kumpasha habari hiyo Salome.
“Salome mjukuu wangu, inavyoonesha Mwenyezi Mungu ameamua kutufungulia milango yote ya heri na baraka.” Alitamka kwa utulivu akijaribu kuficha furaha iliyoujaza moyo wake.
“Habari gani hiyo bibi? Niambie tafadhali!” Salome alisisimka kwa shauku kubwa.
Bibi alimkazia macho kwa upendo, kisha akamwambia kwa sauti iliyojaa msisimko, “Leo tulipomaliza kazi, kaka yako Ali aliniita kando. Unajua aliniambia nini? Kuna kazi amekutafutia!”
Salome akamtazama bibi yake kwa macho yenye shauku kubwa, “Kazi gani hiyo, bibi?” Sauti yake ilibeba matumaini na shauku kwa wakati mmoja.
“Kuna tajiri mmoja ana mashamba makubwa ya miti karibu na kijiji cha Matale. Mtu huyo ni mzungu na amekuwa akihitaji msaidizi wa kazi za ndani. Mshahara kwa mwezi ni laki mbili na nusu, Salome!”
“Bibi! Umesema laki mbili na nusu? Sio kweli!” Salome alipatwa na mchecheto.
“Ndio, mjukuu wangu. Ali mwenyewe amethibitisha...” Bi Salome alisisitiza huku akimtazama mjukuu wake kwa macho yaliyong’aa kwa furaha.
Salome akajishika kifuani kwa kihoro na mikono inayotetemeka, asiamini macho wala masikio yake. Machozi ya furaha yakawatoka wote wawili, wakiwa kwenye hali ya kukumbatiana.
Joto la shauku na furaha lilivyopoa, wakapiga magoti sakafuni na kuinua mikono yao juu. Wakafanya dua ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu.
Bi Salome hakuwahi kukata tamaa katika kumwomba Mungu ili amlinde mjukuu wake dhidi ya shimo lililomzamisha mama yake. Na leo kwa mara ya kwanza, alihisi kwamba Mungu amesikia kilio chake. Kwa elimu duni iliyogotea darasa la saba, nani angeamini kuwa Salome angepata kazi yenye ujira mkubwa kama huo? Aliwaza hayo kwa furaha na uchungu kwa wakati mmoja.
Kwa hakika huo ulikuwa usiku wa kipekee, na tukio hilo wakalihesabu kama muujiza mkubwa kwao. Na kweli ulikuwa muujiza, maana ajira hiyo ilikuwa lango la historia mpya na kumbukumbu zisizosahaulika!
Maandalizi ya safari yalifanyika kwa haraka, na siku tatu baadaye, Ali alikuwa tayari kumchukua Salome kwenda kumkabidhi kwa mwajiri wake mpya.
Siku hiyo kabla ya kuanza safari, Bi Salome alimsogeza kando mjukuu wake na kumpa nasaha za mwisho. Akimtazama kwa macho yaliyobeba mchanganyiko wa hisia za furaha na huzuni, alishusha pumzi nzito kabla ya kuzungumza.
“Moyo wangu una furaha upande mmoja na huzuni upande mwingine,” alianza kusema kwa sauti ya upole.
“Nina amani kwamba umepata kazi hii, lakini najisikia unyonge usio na kifani kwa sababu ya kutengana nawe, mjukuu wangu. Umekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu tangu siku ulipozaliwa. Leo hii unaondoka, na sijui lini tena nitaweza kukuona…” Alinyamaza kwa muda, akameza funda la mate, kisha akaendelea.
“Lakini maisha ndivyo yalivyo. Wakati mwingine ni lazima mtengane ili mambo mengine yaendelee.”
Akampa Salome mkono wake uliodhoofika na kumsisitizia kwa sauti ya upendo:
“Salome, hali yetu unaijua fika—maisha yetu si rahisi hata kidogo. Ukiwa huko, tafadhali zingatia sana kilichokupeleka. Nakusihi ufanye kazi kwa bidii na uaminifu; uwe mnyenyekevu kwa kila mtu utakayekutana naye. Mwenyezi Mungu akuepushe na shari za dunia hii na akufanyie wepesi. Nakutakia kila la heri, mjukuu wangu.”
Maneno hayo yalimchoma Salome moyoni. Akamsogelea bibi yake na kumkumbatia kwa nguvu, macho yake yakiwa yamejaa machozi.
“Bibi yangu…” alishusha pumzi kwa uchungu. “Nakuahidi, sitakuangusha. Nitafanya kila kitu kama ulivyonifundisha siku zote.”
Bi Salome akamgeukia Ali Bin Saidi, na kumshukuru kwa mara nyingine. Upendo na ukarimu usio na masharti wa kijana huyo, ulimuachia moyoni deni lisilolipika. Akaishia kumwombea dua na kuwatakia safari njema.
Ali aliwasha pikipiki yake kubwa ya kijapani aina ya Honda XLR 250; ikatoa muungurumo mzito. Ilikuwa yapata saa mbili asubuhi.
Salome alipanda kwa tahadhari juu ya pikipiki hiyo ndefu iliyomzidi kimo, akajibana kwa uangalifu huku akishikilia mfuko wake wa nailoni. Ndani yake kulikuwa na nguo chache pamoja na vitu vidogo vya thamani kwake. Safari ya kuelekea shambani ikaanza.
Bi Salome hakurudi ndani mpaka alipohakikisha pikipiki ile imepotea kwenye upeo wa macho yake. Moyo wake ukawa mzito ghafla, hisia za uchungu zikamwelemea.
Hakuwahi kutengana na Salome tangu kuzaliwa kwake, na sasa alimwona akitoweka mbele yake bila kujua mazingira ya huko aendako. Sura yake ikasinyaa ghafla, akaonekana mzee kuliko umri wa miaka sitini na mbili aliyokuwa nayo. Alirudi ndani kiunyonge akiwa na mzigo mzito wa mawazo.
Ali aliacha barabara kubwa ya Morogoro na kuingia upande wa kushoto, akishika barabara iendayo Turiani. Chombo kikapata moto, mlio wa pikipiki ukabadilika na kuunguruma kwa sauti kali zaidi.
Upepo ulimpiga Salome usoni kutokana na mwendo kasi wa pikipiki. Akafumba macho yake na kuinua juu sura yake ili kuruhusu upepo umpige zaidi. Upepo huo uliamsha hisia fulani ya ajabu ambayo hakuwahi kuipata kabla. Ni kama ulikuwa ukifuta huzuni na kumuondolea mikosi yote iliyowahi kumuandama zamani. Akapata hisia za mtu aliyeshusha mzigo mzito mabegani na kubakiwa na faraja isiyoelezeka nafsini.
Baada ya mwendo wa takribani dakika hamsini, Ali alipunguza mwendo na kuashiria taa ya upande wa kushoto. Kisha akaiacha barabara ya lami inayokwenda Turiani na kushika njia ya vumbi kuelekea kijiji cha Matale. Mbele kidogo, wakakutana na njia pacha. Njia moja ilielekea kijijini, lakini wao wakashika upande wa kushoto, wakiingia ndani zaidi kuelekea mashamba ya mwekezaji yule.
Polepole, wakaanza kuzama kwenye msitu mzito, wenye miti mikubwa iliyoshikana kiasi cha kuzuia mwanga wa jua. Giza hafifu likatawala, likitengeneza kivuli kizito kati yao.
“Huyu mzungu analipa vizuri sana, Salome.” Sauti ya Ali ilikatiza ukimya, ikimwondoa Salome kutoka kwenye dimbwi la mawazo. “Kama utaweza kwenda naye sawa na akakuamini, nina hakika atakusaidia.”
“Sawa kaka.” Salome aliitika kwa udhaifu huku macho yake yakiangaza kwa hofu pande zote za msitu huo.
Walisafiri mwendo mrefu katikati ya msitu wenye utulivu na ukimya wa kushangaza bila kukutana na kiumbe cha aina yoyote. Sauti pekee iliyotibua ukimya ni muungurumo wa pikipiki waliyopanda. Hali hiyo ikaibua maswali mazito katika kichwa kidogo cha msichana huyu.
Hatimaye safari iliyoonekana haina mwisho, ikaishia mbele ya nyumba kubwa iliyozingirwa kwa uzio wa mabanzi. Walivuka geti lisilo na mlinzi na kusimama katikati ya uwanja wa nyumba hiyo. Baada ya kuzima injini ya pikipiki, Ali na Salome wakapokelewa na kimya kizito.
“Hapa ni wapi?” Swali likamtoka Salome.
“Hapa ndiyo mwisho wa safari yetu. Lakini nahisi kama mwenyeji wetu hayupo, maana huu ukimya...halafu silioni gari lake!” Ali alijibu macho yake yakiangaza huku na kule.
Ghafla ile shauku na ari ya kazi mpya vikayeyuka kabisa katika nafsi ya Salome. Ukimya na upweke wa nyumba hii ulimvunja moyo. Lakini hali ya ukiwa uliofunika mandhari yote ulimtisha zaidi.
Alipata hisia za nguvu kwamba kuna kitu hakikuwa sawa katika mazingira ya nyumba hiyo. Kila kona ya nyumba hiyo ilimpokea kwa ukimya wa kaburi na hali ya maombolezo. Nafsi yake ikamezwa na kivuli cha hofu.
Trekta chakavu aina ya Velmet lilionekana upande wa kulia wa geti. Pembeni yake kuliwa na majembe mawili ya plau yaliyoliwa na kutu. Nyuma ya trekta, kulikuwa na trela iliyoegeshwa juu ya jiwe kubwa, kama vile imesahaulika kwa miaka.
Wakazidi kusonga taratibu kuelekea mlango wa mbele wa nyumba, Salome akizidi kustaajabu jinsi mazingira yalivyokuwa machafu. Ilimuwia vigumu kuamini kama paliishi watu timamu ndani ya nyumba hiyo. Nyasi zilistawi kila pahala na kubashiri uwezekano usio na shaka wa kuwepo nyoka na wadudu hatarishi kwenye makazi hayo. Wanaishije?
Wakiwa wamekaribia mlangoni tayari kwa kubisha hodi, ghafla wakagutushwa na macho makali ya mbwa aliyekuwa akiwakodolea muda wote tangu walivyotua miguu yao juu ya ardhi hiyo.
Mbwa huyu alikuwa ndani ya banda lililojengwa mbali karibu na uzio. Namna alivyowachungulia bila kubweka kupitia upenyo mdogo baina ya bati na mbao zilizosuka banda hilo, ni kama aliwaruhusu wamalize kufanya walichotaka.
“Aisee… Umemuona yule mbwa? Sijawahi kuona mbwa kama yule!” Ali alihamaki. Hata kama angejikaza kiume katu asingeweza kuficha hofu iliyojipambanua wazi machoni mwake. Salome aliishia kuguna na kujibanza kando yake kwa hatua za mnyato.
Kwa hadhari na hamaniko Ali akabisha hodi. Ukimya uliokuwepo ukatibuliwa na mwangwi ulioleta taswira halisi ya mahame ya kale. Hapakuwepo dalili ya mtu.
Baada ya kupiga hodi ya tatu, aliibuka mwanaume anayenyata kama kivuli kutokea nyuma ya nyumba akiwa amevalia sare za zisizotambulika. Akawakaribia taratibu, mikono kaiweka nyuma na kuwatazama kwa udadisi.
“Habari zenu!” Sauti yake ilikuwa kavu.
“Njema mkuu, Asalaam aleikum!” Ali aliitika.
“Na wewe pia.” Alijibu.
“Shikamoo!” Salome akaamkia.
“Asante.” Akajibu kwa ufupi bila kuonesha hisia. “Niwasaidie nini?”
Ali alinyamza kwa muda kabla ya kumjibu lolote. Ni kama alikuwa akitathmini utimamu wa mtu huyo na uwezekano wa kuafikiana bila kuzua rabsha.
“Nilikuwa na miadi na Mr Badwell, tulikubaliana kukutana hapa katika majira haya.” Ali alimweleza kwa utulivu.
“Mzee Badwell hakuniambia lolote kuhusu ujio wenu!” Mlinzi mwenye makunyanzi usoni na madevu yenye mvi alijibu kwa jeuri.
“Basi naomba umjuze kuwa tumefika. Ukimtajia Ali Omar ataelewa…”
“Mzee alitoka tangu alfajiri. Ninachofahamu ni kwamba atarudi, lakini hakuniambia kama kungekuwa na ugeni wa aina yoyote leo. Kama una hakika mna miadi naye, basi mnaweza kusubiri.”
Kulikuwepo kitu cha kukereketa katika haiba, sauti na matamshi ya mlinzi huyu, ambaye hakukosa miaka hamsini na tano kwa kumkadiria. Dharau. Aliongea kwa dharau na majivuno. Aliashiria kuwa mtu mkorofi anayehusudu shari kuliko hata chakula.
Kwa muda Ali alijikuta akitabasamu, lakini lilikuwa tabasamu la mfadhaiko na mvunjiko wa moyo.
“Sasa mbona hakunijulisha mapema? Angenijuza kuwa atatoka ningemsubiri Dumila.” Ali alilalamika.
“Hauelewi maana ya dharura kijana? Nimekwambia mzee alipata safari ya dharura, vinginevyo si ungemkuta hapa? Au?” Mlinzi alijibu kwa ukali.
Sasa anamkaripia nani? Kwani ugomvi? Salome alikwazika.
Ali, kijana mstaarabu mwenye uzoefu wa kuishi na watu tofuati, hakupata tabu kupambanua silika ya mlinzi huyo. Akajiepusha na mtego wa malumbano dhidi yake.
“Nimekuelewa mzee wangu, hakuna kilichoharibika. Nitawasiliana na Mr Badwell moja kwa moja kwa simu yangu ya mkononi. Ni bahati mbaya tu eneo hili halina mtandao….” Alisema huku akitazama kioo cha simu yake.
“Ila sasa, itabidi huyu msichana abaki hapa kwasababu tulikubaliana hivyo tangu jana. Binafsi nina majukumu mengine natakiwa kurudi Dumila.”
“Ni sawa pia!” Mlinzi alijibu kwa mkato huku akitawanya mikono yake hewani.
Pakapita ukimya mfupi.
“Salome!” Ali alimgeukia msichana.
“Abee!”
“Itabidi nikuache hapa lakini usiwe na hofu yoyote. Kila kitu kitakaa sawa ingawa imekuwa bahati mbaya tumepishana na huyu bwana mkubwa. Azma yangu ilikuwa nikukabidhi kwake mimi mwenyewe, lakini kwa kuwa taarifa za ujio wako anazo, hakuna kilichoharibika.” Alinyamza kwa kitambo kifupi.
“Naelewa mwanzoni haya mazingira yatakusumbua kwasababu ya ugeni, lakini ukishayazoea utaona kila kitu kinaenda sawa. Jambo la msingi kwako ni kuendelea kujituma katika kazi na kujifunza kwa uaminifu yale yote utakayoelekezwa.”
Maneno hayo yakaibua donge la uchungu. Salome akahisi huzuni kubwa moyoni na kujikuta akitokwa machozi. Alihisi kama Ali amemleta kifungoni. Nafsi yake ilitamani warudi wote Dumila lakini akakosa ujasiri wa kutamka hayo. Angewezaje kumvunja moyo kirahisi, mtu aliyehangaika kumtafutia ajira yenye ujira kuntu?
Basi Salome alitingisha kichwa kumkubalia, akiwa ameng’ata kwa nguvu midomo yake akijizuia kulia. Ali akahisi huzuni kubwa juu yake. Akamkaribia na kumkumbatia kwa sekunde kadhaa, kitendo kilichotoboa kijaruba cha machozi ya msichana huyo.
“Usilie mdogo wangu, nitakuwa nakuja kukutembelea mara kwa mara. Pia nitajitahidi nimlete bibi mapema iwezekanavyo, aje kukusalimia na kuona mazingira unayofanyia kazi.” Salome alitikisa kichwa machozi yakiendelea kumbubujika.
Wakiwa wamekumbatiana, macho ya Salome yaligongana na yule mlinzi ambaye kwa sasa alisimama nyuma ya Ali. Baada ya kugonganisha macho yao, mlinzi alijishika kiunoni na kutingisha kichwa kama anayemsikitikia. Lakini macho na mdomo wake uliobetuliwa upande mmoja, ulifichua kebehi ya wazi.
Baada ya kutengana, Ali alichomoa noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi Salome. “Hii itakusaidia kwa chochote.”
Baada ya hapo akageukia pikipiki yake, akaisogelea na kuitia moto. Akampungia mkono kwa mara ya mwisho kabla ya kukwea juu yake. Aliiondoa pikipiki taratibu na kutoweka mbele yao.
Salome alihisi kama dunia imemuacha peke yake. Alitamani kupiga kelele kwa nguvu ili Ali arudi kumchukua, lakini hakuweza. Akaendelea kukodolea macho upande huo, akisikiliza mlio wa pikipiki kwa jinsi ulivyofifia taratibu mpaka ulivyotoweka kabisa.
“Utasimama hapa nje mpaka saa ngapi?” Sauti ya mlinzi ilimzindua. Sasa wakiwa wamebaki wawili tu, Salome hakuwa na budi ila kutii kila alichoamriwa na mwenyeji wake.
Mlinzi akamuongoza hadi ndani ya jumba hilo lililojaa upweke. Akamfuata kwa nyuma mithili ya kondoo aliyefikishwa machinjioni.
“Utakaa hapo kumsubiri mzee.” Kauli yake ilisindikizwa na ishara ya kidole kuelekea kwenye kiti kidogo cha mbao kilichoegeshwa kando ya masofa ya kuvutia.
Salome alikiendea kiti hicho na kujikunyata juu yake mfano wa kifaranga kilicholoana kwa mvua. Mfuko uliobeba nguo zake ukaendelea kubaki juu ya mapaja yake.
Mlinzi alimtazama kwa muda bila kutia neno, halafu ghafla akatoka nje pasipo kuaga. Sauti ya msuguano wa kitasa na funguo ndiyo uliomgutua Salome, kwamba mlinzi alikuwa akifunga mlango kwa nje. Msichana akaduwaa, macho yake yakielekea mlangoni kwa mshangao. Mbona ananifungia ndani?
Tukutane saa moja kamili jioni.....
Urojo si urojo chai si chai
Nimejikaza kuinywa imenishinda tuwaachie wenyewe aseeHii Chai ina hadi vitunguu,hoho, binaries nyembamba mixer na ubuyu. Kwa kifupi hainyweki hata ujikaze vipi.
PoleNimejikaza kuinywa imenishinda tuwaachie wenyewe asee
Usijali lazima iisheMkuu malizia
DuuuuuuMachozi ni kimiminika kama yalivyo maji....imekuwaje kama hicho kilichotoka kwenye mti kiwe machozi badala ya maji?
Unamaanisha hii ni chai mkuu?
Tena ya motooo.Unamaanisha hii ni chai mkuu?