Mtera washtukia matusi ya mbunge wao

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Danson Kaijage, Mtera
WANANCHI wa kijiji cha Igunguli, kata ya Loje, wilayani Chamwino, mkoani Dodoma, wamemshukia mbunge wa jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kwa kushindwa kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ya kuwania ubunge mwaka 2010 badala yake amekuwa akitumia muda mwingi kutukana.


Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti kijijini hapo, walisema kuwa mbunge huyo badala ya kutekeleza masuala muhimu amekuwa hodari wa kutukana majukwaani na kufanya ziara mbalimbali za kisiasa nje ya jimbo lake wakati wananchi wake wanakabiliwa na matatizo mengi.

Emanuel John alisema tangu mbunge huyo achaguliwe hajawahi kufika kijijini hapo licha ya kuwaahidi kuwafanyia mambo mengi ya maendeleo.


Alisema kuwa ili kuonyesha ni jinsi gani Lusinde hayuko karibu na wananchi aliahidi kumsomesha mtoto ambaye alifiwa na baba yake na kubakiwa na mama ambaye hana uwezo lakini mpaka sasa hajafanya lolote juu ya mtoto huyo.


"Wakati wa kampeni Lusinde aliahidi kuwasaidia watoto yatima pamoja na wasiojiweza lakini cha kushangaza mpaka sasa hajatimiza jambo hata moja," alisema John.


"Mbaya zaidi ni pale ambapo anapotakiwa kufanya mikutano amekuwa akikwepa hata leo (jana) alitakiwa kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Igunguli lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea na nasikia ameuahirisha," alisema John.


Alisisitiza kuwa imekuwa aibu kwa mbunge huyo kushindwa kutekeleza ahadi ya mtoto ambaye hana baba na mama yake ni mgonjwa lakini alipofuatwa nyumbani kwake alitoa shilingi 5,000.


Wananchi wengine ambao ni makada wa CCM ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema inasikitisha kuona kuwa mbunge huyo amekuwa akizunguka mikoani kutumia majukwaa kutukana badala ya kukaa jimboni kwake kutimiza ahadi ambazo alizitoa wakati wa kipindi cha kampeini mwaka 2010.


Mmoja wao ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini alisema mbunge huyo kwa sasa hawafai kwa jambo lolote na ni bora wangechagua vyama vya upinzani.


"Hapa Mtera hatuna mbunge, angalia leo tulishajipanga kumpokea mbunge wetu kwa ajili ya kumpa kero zetu lakini hakujali na sasa tumepata taarifa kuwa hatakuja katika mkutano wa hadhara.


Alipotafutwa mbunge huyo kwa njia ya simu kujibu malalamiko hayo hakuweza kupatikana badala yake alipatikana katibu wake aitwaye Patrick Nyambua ambaye alikiri bosi wake kutakiwa kufanya mkutano jana katika kijiji cha Igunga lakini kutokana na mwingiliano wa ratiba hakuweza kufanya mkutano huo.


"Siyo kweli kuwa mbunge amekimbia mkutano, bali kilichotokea ni kuwa amepata ratiba ya kwenda Mtwara hivyo isingekuwa rahisi kufanya mkutano huo," alisema katibu wa mbunge.

Kuhusu kutekeleza ahadi za mbunge huyo katibu wake alisema kuwa utekelezaji au kutokutekeleza ni jukumu la mbunge mwenyewe.
 
Ina Maana CCM wakimuweka William Malecela na yoyote wa Chadema Mtera Chadema kitashida

Nilimuona Malecela kwenye East Africa Bungeni hawezi kujenga Hoja hata kidogo
 
kama na dodoma vijijini wameanza kuamka basi M4C imefanikiwa

cdm kazeni buti na kampeni ya vua gamba(ufisadi) vaa gwanda(haki na uwajibikaji) kwani saa ya ukombozi imekaribia
 
Unajua kuna watu wa ajabu sana hapa duniani. Hivi kule ndio kwao na kinachomfanya asiwe na mipango madhubuti ya maendeleo ya kwao ni nini? Huwa sipati jibu nikiwaona watu kama huyu. Mpaka wananchi wampige mawe ndo ataelewa, wakati ni jambo dogo sana.
 
Wasipokaa sawa atawatukana hata wanaomhoji kuhusu ahadi zake. Walinywe tu kwakuwa walilikoroga wenyewe kwa kapelo, khanga, chumvi na ubwabwa wa siku 1.
 
Wasipokaa sawa atawatukana hata wanaomhoji kuhusu ahadi zake. Walinywe tu kwakuwa walilikoroga wenyewe kwa kapelo, khanga, chumvi na ubwabwa wa siku 1.

Komeo, watalinywa sana tuu mpaka 2015 wako hoi vitumbo ndiiii!!!!!
 
Wabunge wa CCM 30 = 1 CDM, sio huyo tu tuna wengi vilaza kwa kutaja wachache Nyambari Nyangine, Komba, Rage, Nkamia. Pia wabunge wa CUF 50= 1 CDM kwani huwa sioni wanafanya nini bungeni zaidi ya kulialia tu.
 
Ina Maana CCM wakimuweka William Malecela na yoyote wa Chadema Mtera Chadema kitashida

Nilimuona Malecela kwenye East Africa Bungeni hawezi kujenga Hoja hata kidogo

Watoto waliozaliwa na Silver spoon huwa wanahitaji muda mwingi sana kuwa wanasiasa wazuri, kwani wengi wao huwa out of touch na matatizo ya kawaida ya wapiga kura, ukimuuliza maana ya kulala njaa atakuona kana kwamba unatania vile. Ila mimi bado ninaamini kabisa kuwa Willy ni mwanasiasa mzuri na mwenye uchungu na nchi hivyo tumpatie muda wa kujifunza siasa za majukwaani.
 
Wabunge wa CCM 30 = 1 CDM, sio huyo tu tuna wengi vilaza kwa kutaja wachache Nyambari Nyangine, Komba, Rage, Nkamia. Pia wabunge wa CUF 50= 1 CDM kwani huwa sioni wanafanya nini bungeni zaidi ya kulialia tu.

teh teh, Wabunge wa CUF bungen jumla wapo 32, hiyo hesabu yako umewanyonga kk!
 
kudadadek waliingia choo cha walimu.
kudadadeki walifikir alikuwa anasema kweli?
kudadadeki atawachana mchana kweupe.
kudadadeki ni yupi mliyemchagua akawaletea maendeleo tokea uhuru?
 
ndio muelewe kwamba mlimchagua popompo kabisa fanyeni mabadiliko
CDM ipo kwa ajili yenu walalahoi acheni kufurahia kofia,tisheti,na kanga amkeni
wenzenu huku Iringa ni maendeleo kwenda mbele na mbunge wetu anafanya mikutano kila kata kujua kero za watu na huyo ni jembe PETER MSIGWA
 
Livinstone Lusinde ndiye Mbunge wetu wa Mtera ww huwezi tusemea wapiga kura wake tunamgguutaji na tutampa, hatukubaliani na kuigawa nchi kimajimbo au nchi ya MERU jitengeni tu tuacheni na Amani yetu ya Iringa mtayajua sasa kwani Lusinde naye allitokea upinzani aliyaona
 
Back
Top Bottom