Mtei: Sokoine angewachapa viboko viongozi wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtei: Sokoine angewachapa viboko viongozi wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Na Hemed Kivuyo,Arusha

  MUASISI na mwenyekiti wa kwanza wa Chadema, Edwin Mtei amesema kuwa kama waziri mkuu wa zamani, marehemu Edward Sokoine angekuwepo na kuona hali ilivyo ndani ya CCM na serikali yake, angewaadhibu baadhi ya viongozi kwa viboko.

  Mtei alisema hayo katika mahojiano na gazeti hili nyumbani kwake eneo la Chama, Tengeru mkoani Arusha.

  Alisema kuwa ndani ya CCM kuna baadhi ya viongozi wameweka maslahi binafsi mbele na kukiuka miiko ya uongozi kiasi cha kuwaibia wananchi na kujilimbikizia mali na hivyo kuwa matajiri wa kupindukia kwa njia isiyo sahihi.

  Alisema kuwa ndani ya serikali na CCM kuna wafanyabiashara wakubwa ambao wana nguvu na ambao huamua wanachokitaka bila ya kuzingatia misingi na kanuni ya kukiongoza chama hicho, kitu ambacho Mtei alisema kilikuwa kikipingwa na Mwalimu Nyerere pamoja na Sokoine.

  Aliongeza kuwa vitendo vya ufisadi vinavyofanyika hivi sasa ni matokeo ya baadhi ya viongozi ndani ya serikali kuweka mbele maslahi yao binafsi na kwenda kinyume na maadili ya uongozi.

  ''Vitendo vya ufisadi vinavyofanyika hivi sasa ni matokeo ya viongozi wa CCM kukiuka maadili ya uongozi na ni vyema chama hiki kikaondolewa madarakani kutokana na kadhia hiyo,'' alisema Mtei.

  Alisema kutokana na mambo hayo, kama Sokoine angekuwa hai angewaadhibu viongozi hao kwa viboko na baadaye kupelekwa katika mkondo wa sheria na hatimaye viongozi hao kukoma kufanya vitendo hivyo. Sokoine alifariki mwaka 1984 kwa ajali ya gari wakati akitokea Dodoma kwenye kikao cha Bunge. Kabla ya kifo chake alisimama kidete kupambana na wahujumu uchumi, ambao baadhi walilazimika kukimbia nchi na wengine kutelekeza biashara zao
   
Loading...