Mtego wa Rais kwa CAG

…kama wewe mwenyewe haujiamini ni vigumu sana kuwaamini wengine…
 
Ina maana serikali haijui Taifa linanufaikaje na madini?? Kwanini asipitie mikataba ama kuipeleka bungeni ili ipitiwe upya? Je hayo madini hayo bado yapo huko ardhini ama yanakaribia kuisha kama sio kuisha kabisa?? Miaka yote walikuwa wapi?? Nashauri akitoka hapo apitie na mikataba ya gesi..
 
Magu anaakili na ndo maana ni raisi mwenye Maono anatambua wazi kuna Udanganyifu Unaweza Ukafanyika kwenye Hiyo kazi aliyopewa Uhuru Ukizidi kipimo ni Utumwa.
 
Ingelikuwa mm ndio prof assad ningejiuzulu, kuonyesha kwamba hata mm sina imani naye.
 
Hujajibu suala la Magufuli kuingilia sehemuambazo hatakiwi kuingilia.

Rais anatakiwa sio tu kufanya vitu vizuri (kusaidia hospitali ipate vitanda ni kitu kizuri) lakini pia anatakiwa kufanya vitu vizuri kwa njia nzuri (kuliamrisha bunge kusaidia hospitali kunakiuka misingi ya separation of powers, na hivyo si kitu kizuri).

Magufuli hana weledi wa kujua hilo, ama hajali.

Kaingilia ovyo ovyo kote huko nilikokutaja, kama nchi haina misingi ya uongozi.

Hilo haliteteeki.
 

Wewe unajuwa zaidi ya wabunge wote?
 
CAG naye ni binadamu, na hii issue ni nyeti. Huko nyuma tuliona Ma CAG wakishambuliwa bungeni kwa kupindisha ukweli.

Kwa kuunda timu kadhaa, Rais anataka tu kujiridhisha na ukweli ..! Nafikiri ni strategy nzuri kwa kiongozi yeyote.
Sasa ikiwa ripoti zitatofautiana; ataiamini ripoti ipi na ataiamini kwa kutumia vigezo gani?!! Kama miongoni mwa wale atakaowatuma; anamuamini mmoja wapo; kwanini hiyo kazi asimpe huyo huyo?!!!

The problem with your president ni kwamba, anajifanya ni yeye tu na Bashite wake ndio sio mafisadi wakati ukweli ni kwamba; hata yeye nae ni fisadi tu sawa na wenzake!!!! Na ndio maana akifanya ufisadi anaenda kuuficha jeshini ili watu wasihoji!!!
 
Kwa binadamu alivyo safari moja huanzisha nyingine ukishajenga mazoea ya kutoamini watendaji wako kiasi hicho basi utakapoletewa kazi ya hao invisible team itafika mahali nao hutawaamini utaunda invisible na invisible na ni invisible............hadi uchanganyikiwe lakini yote hayo tisa waliosaini hiyo mikataba si wapo??yaani Mkapa na Kikwete wana ccm wenziwe waliotufikisha hapa si awaulize??au ndio kutaka kuonekana wewe ndio bora katika kapu la samaki waliooza??zote hizo ni kiki tu hamna kipya.
 
Weka mkataba wa madini hapa tuusome humo ndani kama mchanga haujasemwa basi ubaki

Kumtuma CAG na tume invisible tutatoa mapesa kibao lakini kamkataba kadogo hata kama ni soft copy itagharimu bundle la sh 500 tu
 
Na haya ndio madhara yake waswahili husema mficha ficha maradhi kilio kitamfichua wanasaini mikataba mibovu halafu wanaficha hawataki kuipeleka bungeni maji yamewafika shingoni wanaanza kutoka hadharani kuunda tume lukuki na hata kamati za bunge wakati bunge lenyewe hata mikataba yenyewe hawaijui eti wanachunguza kwa hadidu lejea mmm!!acha ikulu ihangaike nayo maana hakuna namna kwani hayo ni mambo ya kujitakia kujifanya wao wanajua kila kazi tu lakini mwisho wa siku hawataki kuangalia pale walipojikwaa.
 
aaminike amekuwa MUNGU nadhani sisi wenyewe kumuamini MUNGU ni ngumu sasa iweje sembuse umuamini binadamu mwenzako aliye na madhaifu na hajakamilika, eti haaminiki aaminike amekuwa malaika au msaidizi wa mnyaazi Mungu
k
 
Wewe unajuwa zaidi ya wabunge wote?
Hao wabunge wa Tanzania hata wakijua zaidi yangu wamefungwa na mfumo wa kifashisti unaowafanya wamuabudu mtu mmoja hata kama anapeleka nchi kuanguka katika korongo.

Ndiyo maana unaona mawaziri wasomi wanapelekwa pelekwa wanashindwa hata kujiuzulu.

Na hata wanaotoka serikalini bado wanajishaua shaua kwa Faru John.

Isitoshe, wabunge wengi tu wanasema haya haya ninayosema mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…