Mtazamo wangu: Mashine za EFD ni uonevu

Mtazamo wangu: Mashine za EFD ni uonevu

illegal migrant

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2013
Posts
1,277
Reaction score
1,121
Leo nimepita kwa ma supplier wengi kufanya malipo kwani tulikuwa na shughuli muhimu wiki iliyopita hivyo kutulazimu kukodi huduma mbali mbali kama vile ulinzi, vyombo vya habari, mahoteli, makampuni ya kukodisha magari na mengine mengi sasa siku ya leo nilikuwa na enda kufanya malipo kwa haraka haraka ni ofisi takriban arobaini hivi hakuna hata moja waliyonipa risiti ya kielektronoki, ikumbukwe haya ni maofisi makubwa, hoteli za nyota tano hakuna hata moja inayotoa risiti hizi, makampuni ya simu, makampuni ya ulinzi haya makubwa makubwa unayoyajua wewe lakini mjasiriamali akifungua duka lake la spea watoza ushuru lazima wamletee zengwe au ni mimi sielewi anayepaswa kutoa risiti hizi ni nani? cc Mwigulu Nchemba
 
Last edited by a moderator:
Kwa mfumo wetu, wa ukusanyaji kodi ni mgumu sana, kwanza kwenye suala la kodi haliitaji nguvu nyingi na sheria kali sana, ili watu walipe kodi bali ni elimu tu, na hao walipaji kodi waone umuhimu wa kodi pale wanapoona mrejesho wa matunda yake, sasa hapa Tz we unakamuliwa kodi kila siku unasikia bilioni kadhaa zimeliwa huo si ujinga, ukienda hospital hata panadol tu hamna, masokoni huko kila lro ni ushuru takataka tu kuziondoa ni shida. Tofauti na wazungu, wao nawaona ufahali kulipa kodi kwani wanaona matokeo yake. Hapa kodi mnakusanyia WAHUNI tu, na wafanya biashara wakubwa nchi hii hawalipi kodi inavyotakiwa, mlipaji kodi ni yule anayetafuta pesa ya kula tu. Na hasa kariakoo kuna polisi wengi na wafanyakazi wa TRA, Wao ni kuvizia watu ambao hawajapewa risiti na wauzaji, ili wawakamue, hata kama umenunua kwa mhindi flat screen ya sumsung inchi 40,na kwenye risiti imeandikwa laki moja, wao wanakubali tu!!!
 
Ni nini kinachosababisha system tax idara nyeti kama hii kushindwa kufanya kazi, ni siku ya tatu leo nimeshindwa kupata makadirio ya ushuru wa gari kisa eti system haifanyi kazi, inakera sana jamani. Tuoneeni huruma sisi walala hoi.
 
usikute wanataka gari lichelewe kutoka ili ulipe zaidi bandarini
 
Yani ni shida kwa kweli nchi yetu hii, huduma kama hii inakuwaje eti systen haifanyi kazi? Na sio kwamba ni tatizo la jana hizi habari nimeanza kuzisikia siku nyingi sana kulikoni?
 
Kila mwaka selikali inavuka lengo la ukusanyaji wa kodi, pamoja na misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa ya wajanja wachache. Nashindwa kuelewa mfumo huu ambao hata tafiti haikufanywa kama utaleta mafanikio au katika nchi gani ulileta mafanikio,? ''TRA WAKAJIBU KUWA TANZANIA NDIO NCHI YA KWANZA DUNIA'' Lakini yatupasa mashine hizi zinachangamoto nyingi za kimfumo, mfumo wa TRA ni mbovu mno kwahio hizi mashine hazifai, na kama kuna mkubwa ambae alichukua TENDA ya kuiuzia selikali mashine hz kwa maslahi yk ajue biashara yk imedoda. BY CHILUNDULU
 
TRA wanapaswa kujipanga mm binafsi nililipia roadrecense ya gari yangu kwa njia ya simu lakini kuchukua stika ilinichukua siku sita nilikua nafika saa nne mpaka saa tisa kwa siku zote hizo TRA mjilekebishe bhana
 
leteni habari zenye uhakika, msituletee story za maajent wenu makanjanja wanawaongopea eti system hakuna mnashauriwa kutembelea ofisi za tra/customs kuthibitisha mnayoambiwa na maajent wenu ili kupata ukweli kabla ya kuropoka.
 
Wacha watu wapige hela, kukusanya kodi sio muhimu kwa nchi kama Tanzania, hela unayoilipa kama kodi haifiki sehemu inayotakiwa. Watu wanakula na kuzichezea.

So far nasapoti zoezi zima la ukwepaji kodi hadi tupate serikali inayojua nini wananchi wake wanataka.

Kwanza ukipewa hiyo risiti itakupeleka wapi zaidi ya kukujazia mikaratasi home.
 
illegal migrant
mkuu kama ukienda kulipia kodi ya aridhi unapewa risti ya mkono na hiyo ndio serekali kwanini hao wa hotel wasikupe ya mkono?

_na kama trafiki anakuandikia ya mkono wakati hzo efd wanaweza kukaa nazo kwa barabara huu si wizi tu??
 
Last edited by a moderator:
illegal migrant
mkuu kama ukienda kulipia kodi ya aridhi unapewa risti ya mkono na hiyo ndio serekali kwanini hao wa hotel wasikupe ya mkono?

_na kama trafiki anakuandikia ya mkono wakati hzo efd wanaweza kukaa nazo kwa barabara huu si wizi tu??

Kwa kiswahili chako naona kama si mwenzetu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom