Mtazamo wangu kwa Serikali baada ya katibu wa CWT na mweka hazina wake kukutwa na hatia

Singo Batan

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
292
191
Walimu wa Tanzania ni miongoni mwa kundi lisilo na furaha na ajira zao. Hii inatokana na ukweli kwamba pamoja na kulipwa ujira wa utumishi wao kwa mujibu wa viwango vilivyopo kisheria, ujira huo haukidhi mahitaji ya sasa na hautoshelezi kuwafanya watumishi wa kada hii waishi kwa standards zinazotakiwa. Miongoni mwa wanyonyaji wa Walimu ni Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Chama hiki kinawakata Walimu 2% ya mishahara kila mwezi. Makusanyo ya makato hayo kwa mwezi mmoja ni zaidi ya Bilioni 1 (TZS) ukikusanya makato kwa walimu Nchi nzima. Matumizi ya fedha hizi sasa ndio kizungumkuti. Jambo ambalo wakati mwingine walimu hawalifahamu, baadhi ya wanufaika wa fedha hizi ni vyombo vya serikali wanaozipata kwa kukopa au kuchangiwa kama udhamini wa shughuli fulani.

Mwalimu Seif (Katibu Mkuu wa CWT aliyesimamishwa kazi) analifahamu hili kwa uzuri sana.
Fedha hizi zinazovunwa kwa hawa walimu matumizi yake kwa kweli hayana tija kwa wanaokatwa kila mwezi zaidi wanaambulia t-shirt za meimosi, kofia na kurudishiwa 5000 za vocha kila baada ya miezi mitatu (yaani unapigwa 20K plus unarudhishiwa elfu 5 au 6.)

Malalamiko mengi yameandikwa kuhusu hiki chama mfano huyu Mwalimu aliandika makala hii 2018

Adui mkubwa wa walimu ni CWT.

Wana JF mbalimbali wameandika kutoridhishwa kwao na utendaji wa hiki chama pia. Unaweza kupitia link hizi

Kesi iliyowaweka hatiani Deus Seif na Mweka hazina wake ni kujichotea Mil. 13. 9 kwenda kuangalia mechi ya Taifa Stars huko Cape Verde maana yake zipo za kuchezea.

SERIKALI WASAIDIENI WAAJIRIWA WENU KWENYE HILI KWA KUFANYA HAYA:-
1. CWT ina vitega uchumi vingi tu ambavyo vikitumiwa vizuri vinaweza kuhudumia mahitaji ya kichama ya walimu nchi nzima.

2. Kuna Benki iliyoanzishwa na CWT yenye kuiwa Mwalimu Commercial Bank, ni mradi uliolala na umeshindwa kuendelezwa kwa ufasaha. Hapa kwenye Bank iliahidiwa kila mwalimu atapewa sehemu ya umiliki wa hisa za mradi lakini hakuna kilichofanyika zaidi ya ulaghai. Benki ielekezwe kutengeneza faida kwa manufaa ya wamiliki halisi yaani walimu.

3. Sheria ya makato ya 2% ya mshahara wa walimu ibadilishwe na kwa maoni yangu walimu wasikatwe tena. Imetosha sasa.

4. Fedha zilizopo kwenye kapu la CWT zitumike kama mtaji wa kuanzisha miradi ya kimkakati itakayofanya hicho chama kitekeleze majukumu yake (ingawa binafsi sioni execution ya majukumu hayo) zaidi ya vikundi vya walaji.

WALIMU, MSIPOJISIMAMIA WENYEWE MTAISHIA KULALAMIKA NA TOZO ZA CWT ZITAENDELEA KUWANUFAISHA WAJANJA WACHACHE KILA UCHWAO!
 
Walimu wa Tanzania ni miongoni mwa kundi lisilo na furaha na ajira zao. Hii inatokana na ukweli kwamba pamoja na kulipwa ujira wa utumishi wao kwa mujibu wa viwango vilivyopo kisheria, ujira huo haukidhi mahitaji ya sasa na hautoshelezi kuwafanya watumishi wa kada hii waishi kwa standards zinazotakiwa. Miongoni mwa wanyonyaji wa Walimu ni Chama cha Walimu Tanzania (CWT). Chama hiki kinawakata Walimu 2% ya mishahara kila mwezi. Makusanyo ya makato hayo kwa mwezi mmoja ni zaidi ya Bilioni 1 (TZS) ukikusanya makato kwa walimu Nchi nzima. Matumizi ya fedha hizi sasa ndio kizungumkuti. Jambo ambalo wakati mwingine walimu hawalifahamu, baadhi ya wanufaika wa fedha hizi ni vyombo vya serikali wanaozipata kwa kukopa au kuchangiwa kama udhamini wa shughuli fulani.
Mwalimu Seif (Katibu Mkuu wa CWT aliyesimamishwa kazi) analifahamu hili kwa uzuri sana.
Fedha hizi zinazovunwa kwa hawa walimu matumizi yake kwa kweli hayana tija kwa wanaokatwa kila mwezi zaidi wanaambulia t-shirt za meimosi, kofia na kurudishiwa 5000 za vocha kila baada ya miezi mitatu (yaani unapigwa 20K plus unarudhishiwa elfu 5 au 6.)
Malalamiko mengi yameandikwa kuhusu hiki chama mfano huyu Mwalimu aliandika makala hii 2018

[URL Adui mkubwa wa walimu ni CWT.

Wana JF mbalimbali wameandika kutoridhishwa kwao na utendaji wa hiki chama pia. Unaweza kupitia link hizi

Kesi iliyowaweka hatiani Deus Seif na Mweka hazina wake ni kujichotea Mil. 13. 9 kwenda kuangalia mechi ya Taifa Stars huko Cape Verde maana yake zipo za kuchezea.

SERIKALI WASAIDIENI WAAJIRIWA WENU KWENYE HILI KWA KUFANYA HAYA:-
1. CWT ina vitega uchumi vingi tu ambavyo vikitumiwa vizuri vinaweza kuhudumia mahitaji ya kichama ya walimu nchi nzima.

2. Kuna Benki iliyoanzishwa na CWT yenye kuiwa Mwalimu Commercial Bank, ni mradi uliolala na umeshindwa kuendelezwa kwa ufasaha. Hapa kwenye Bank iliahidiwa kila mwalimu atapewa sehemu ya umiliki wa hisa za mradi lakini hakuna kilichofanyika zaidi ya ulaghai. Benki ielekezwe kutengeneza faida kwa manufaa ya wamiliki halisi yaani walimu.

3. Sheria ya makato ya 2% ya mshahara wa walimu ibadilishwe na kwa maoni yangu walimu wasikatwe tena. Imetosha sasa.

4. Fedha zilizopo kwenye kapu la CWT zitumike kama mtaji wa kuanzisha miradi ya kimkakati itakayofanya hicho chama kitekeleze majukumu yake (ingawa binafsi sioni execution ya majukumu hayo) zaidi ya vikundi vya walaji.

WALIMU, MSIPOJISIMAMIA WENYEWE MTAISHIA KULALAMIKA NA TOZO ZA CWT ZITAENDELEA KUWANUFAISHA WAJANJA WACHACHE KILA UCHWAO!

Hii nchi ni ngumu sana. Ni panya road Kila mahali.
 
Chakuhawata unakatwa elfu tano (5000/=) tu.
Cwt imechakaa sana,upigaji mwingi kila eneo,kuanzia Taifa hadi wilayani.
 
Tatizo nikwamba! Kundi la walimu ndio Bwawa la kujifunzia kuogelea! Acha wateseke! Mana wao nikushangilia2, Bola niwe mchoma chips nchi hii , kuliko kuwa mwl.🤣🤣 ukichoma chips Mwl ni wako, awe wa kike au Me..🤣🤣
 
Back
Top Bottom