Mtazamo wangu kuhusu Pro Baregu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtazamo wangu kuhusu Pro Baregu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by cilla, Apr 14, 2012.

 1. c

  cilla JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 249
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Kitendo cha professor Baregu kutokutumia biblia au Quran wakati wa kuapishwa sioni kama ni tafsiri ya kuwa mpagani.
  1,Naona fasihi yakutokuwa upande wowote wa dini wakati wa mchakato. wa katiba ilakusimamia usawa.
  2.Kuapa kwa kutumia vitabu vya Mungu hakumaanishi atakuwa sahihi wakati wote kwa hiyo kwa upande mwingine utakuwa unamkufuru Mungu.
  3,WAKRISTO HAWA RUHUSIWI KUAPA KWA KITU CHOCHOTE KAMA NDIO SEMA NDIO KAMA HAPANA SEMA HAPANA.MATHAYO 5;33-37.Kuna ushahidi. wa baadhi ya wachungaji wamewahi kuzigomea hata mahakama na kutumia njia nyingine kisheria lakini haikuwa tafsiri ya kuwa mpagani.Lkn kwa baadhi ya wachungaji wamasilahi hilo nikama hawalioni kama ni kosa.
  4,mafisadi waliapa kwa vitabu hivyo hivyo lakini wakatuibia.
  Chamsingi uwajibikaji,utu, haki na usawa bila kuegemea upande wowote kwa masilahi ya taifa.
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kwa kifupi ni kwamba, Profesa Baregu kaweka Misingi ya Namna gani Imani za Kidini zinatakiwa kuwa approached kwenye Katiba Yetu.

  Kama Ndugu Cilla ulivyo quote kifungu cha Biblia, kwamba Biblia imewaelekeza wote wanaojitambulisha kama Wakiristo kwamba wasiape kwa kitu chochote kile including Biblia, Basi Katiba inatakiwa kuhishimu maelekezo hayo, Mtu akiishasema yeye ni dini Fulani basi, Maelekezo ya Imani yake juu ya mchakato wa kuapa yafuatwe.

  Na isiishie kwenye Kuapa tu bali kwenye Mambo mengine yote ya Kiimani, Maelekezo ya dini husika juu ya Mambo husika yaheshimiwe.

  Ili kujenga Jamii zenye watu wenye Imani zinazoeleweka, uwepo michakato ya kisheria ya kuauthorize Imani fulani za kidini kusambazwa kwa mujibu ya maelekezo ya vitabu vinavyoongoza dini hizo, Kwa maana ya kwamba Imani zote ni lazima maelekezo yake yawe katika Maandiko ama sivyo imani hizo zinabaki kuwa personal issues na haziruhusiwi kusambazwa kwenye Jamii kwa namna yoyote.

  Ninaamini kwamba hii itasaidia kuondoa confusion kubwa ya mambo ya kiimani iliyotapakaa nchini kwetu na duniani kwa ujumla kiasi cha kupelekea mifarakano yenye maafa makubwa sana.

  Hivi sasa kuna imani inaitwa ya kifreemanson, hakuna vitabu vinavyoilezea authoritatively, imani hii inasababisha hofu kubwa sana kwa wananchi hasa wamijini na inaleta instability kubwa sana kuanzia ngazi za kifamilia.

  Bila kuwa na wananchi wenye Imani imara na zisizobadirika badirika kutokana na interpretations za vitabu hivyo zinazoibuliwa na kila namna ya watu, kila kukicha.

  Angalia imani ya Kikirsto, ni mparanganyiko mkubwa sana, wakina kakobe, Gwanyima mfufua watu, na kuna mwingine kule Mwanza anaitwa Father God, sikia mambo ya kina mwingira Mama Lwakatare, na wakatoriki na Rais wao chaguo la Mungu, ni rehema za Mungu tu zinazozuia umwagaji damu.

  Na apa ifikie sehemu tuweke ukomo wa Malalamiko ya Waislamu ambayo yamekuwa yakileta hofu kila wakati bila sababu za msingi, Nasikia wamechaguliwa kwa wingi kwenye tume hii, Waislamu watumie nafasi hii kuhakikisha kwamba Jamii za kiislamu popote zilipo katika Mipaka ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zinaendesha Mambo yake kwa Mujibu wa Kitabu chao/Sharia, na waifinyange katiba katika namna itakayowawezesha kufaidika na Jumuiya za OIC lakini pia tutumie fursa hii katika kuhakikisha kwamba, Kwa mujibu wa katiba yetu, haitawezekana hata kidogo makundi ya kihuni yanayotoa roho za watu kwa visingizio vya imani za kidini, kupata nafasi ya kujiinua katika Taifa letu.Kama tunavyoona Nigeria na the Famous Alkaida Movement.
  Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu katika Jina la Yesu Kiristo kwa Ujasiri aliompatia Profesa Baregu na kuapa katika namna ambayo leo inaleta mjadala kwenye Jamii yetu.

  Tanzania, Nakuombea Rehema na Amani.
   
 3. w

  wenyajr Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF mi nafkiri na hilo liwe wazi kwenye katiba mtu akiapa au kuapishwa atatumia Bible, Quran au Katiba kama kuna issue nyingine iwe wazi isije ikawa jamaa ni ........ there are minor things but Senstive tusiaminiane saana hasa kwenye mambo ya Imani.
   
 4. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  We koma kabisa! Tamko la jk ni chaguo ka Mung lilitolewa na askofu kilaini na hakuwakilisha all catholics! Catholic church hutoa matamko kupitia TEC yaan Tanzania Episcopal Conferene na at tht tym kilain hakua katibu wa Tec aliongea ku eveal mahaba yake kwa ccm and thts y we demoted him!
   
 5. K-killer

  K-killer Senior Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi naomba nije upande mwingine wa sarafu!
  Je inawezekana kua Prof. Ameamua kutokutumia kitabu cha dini kuapa akijua kua he is making a deal with a devil(Mkuu wa Nchi) hivyo itakua dhambi sana uki make deal with a devil and yet uka swear kwakutumia kitabu cha Mungu,yu halikua unajua kabisa kua hamna la maana unaenda kubadilisha kwenye katiba kwani baadhi ya vitu vitakua sio haki na pia baadhi ya vitu watashinikizwa na Bwana mkuu.

  Hivyo kaona ni dhambi kubwa akiapa kwakutumia kitabu cha Mungu wakati anajua hawataachwa huru kwa manufaa ya kutengeneza Katiba inayowafaa watanzania wote,hivyo kwakuapa kwa Biblia ni dhambi kubwa sana wakati unajua unaloenda kulitenda.
  Nawakilisha
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani una-assume kuna dini mbili tu: Uislama na Ukristo.
  Vipi kama Prof Beregu ni Zorostian? au Buddhist? Hizi dini nilizotaja ziko hapa Tanzania. Na pia itakuwaje kwa mmsai asifuata imani yake ya asili?
   
 7. d

  dundula JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 541
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Acha kutudanganya tamko la chaguo la mungu lilitolewa kabla ya uchaguzi kwanini TEC hawakukanusha wakati huo ili lisiwe na effect wakati wa uchaguzi wakakaa kimya mpaka uchaguzi ukaisha?silent means yes
   
 8. a

  african2010 Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Chezea Wapuuzi wenzako wote ila sio Kanisa Katoliki, System za Dunia zitakupoteza, kwa taarifa yako kila Raisi hadi Obama ukishaapioshwa lazima ukapewe baraka Roma, chunga maneno yako.
   
 9. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Duh, mkuu hii ni hoja nzito. Natamani iwe na independent discussion wakati mwingine. Ukishajipanga hebu njoo na data zenye mashiko tupate knowledge pana hapa.
   
 10. The Eagle2012

  The Eagle2012 Senior Member

  #10
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  and so u think that Makes Catholic distinguished?? Catholic is just an anti-christ institution!!
   
 11. The Eagle2012

  The Eagle2012 Senior Member

  #11
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Naunga Mkono hoja yako Mkuu,isipokuwa Ukisoma hilo andiko linasema USIAPE KABISA,yaani hairuhusiwi kuapa kwa namna yeyote ile haijalishi utatumia nn kula kiapo hicho,sasa hapa natatizwa,inakuwaje mtu ambaye amechaguliwa kuwa Kiongozi?
   
 12. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mpaka leo sijajua mantiki ya kuapa umeshika kitabu cha dini, hata mzee Ngombale Mwilu hakuwahi kushika kitabu chochote katika viapo vyake. Kwa viongozi wa serikali labda ashike katiba ambayo ataisimamia
   
 13. G

  Godlv Member

  #13
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wote pale ni devil worshipr, wanapretender, natamani ka wote mngeweza ona katika ulimwengu wa roho ka mie nionavyo..then mngejua kila kitu kinachofanyika na kila jambo linalofanywa dumia hapa nikama marudio, ktk ulimwengu wa roho yalishapangwa siku nyingi!
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Haya mambo ya kuapa yamekuwa usanii tuu siku izi.
  Watu wanaapa kwa katiba na do hao hao wanaivunja the same to Bible na Quraani sijui nimekosea mnisamehe
  Heri mtu yule ambaye hakuapa kwa chochote kile na akatenda haki atahesabiwa haki mbele za bwana
   
 15. grndossy

  grndossy JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Angeapa kwa vitabu vya dini hiyo au taratibu za kimasai ambazo angezisema. Kukataa kuapa kwa kitabu cha dini anyoabudu kunaonyesha uoga kushika hicho kitabu kwa sababu zake au anatupa mashaka kwamba hayuko pale kutenda haki hivyo anaogopa kuhukumiwa na kiapo chake. Tusimsemee sana ajitokeze aseme ukweli wake.
   
 16. N

  Noboka JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,144
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  "I would not want to be hypocritebecause I believe God is there , not in the house of Bibles or Quran's" hiyo ni kauli ya Pr. Baregu. Kimsingi Pr. Baregu ameutendea haki kabisa Uprofesa wake, ni lazima kufikiri. Wengi wetu tuko kwenye haya madhehebu kwa sababu tu ya historia ya familia zetu na hakuna anayetaka kujishughulisha. Ukiangalia wezi/mafisadi wote Tanzania wameapa kwa hivyo tunavyokariri kama vitabu vitakatifu, je mbona mpaka sasa hivi wanaendelea kupeta? laana iko wapi. Binafsi nampongeza Baregu na laiti tungezama kwenye misingi yetu ya asili huenda hata huu ufisadi labda usingekuwa mkubwa kiasi hiki. Turejea historia tu hivi ukristo na uislamu uliletwa na nani, halafu tulinganishe na namna ukoloni ulivyoletwa. Ni vema kutafakari sana kwa kina.
  Kwa vyovyote iwavyo, wengi wetu tunaamini Mungu yupo, ni kwa namna gani tunafika kwake hapo ndipo wazungu na waarabu walipotupiga bao
   
Loading...