ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,622
- 21,689
Ni mara chache sana huwa naandika kuhusu Siasa,na niweke wazi huu ni mtazamo wangu kama ambavyo nawe unaweza kuwa na mtazamo wako
Binafsi naona hii movement ingesubiri kwanza kwasababu moja kubwa,ni hivi majuzi tu Mheshimiwa Tundu Lissu ndio amechukua madaraka ya Uenyekiti wa Chama cha Chadema,hivyo basi angehitaji kwanza kujipanga na kuunganisha nguvu ya chama hasa ukichukua bado kuna majeraha kadhaa baada ya uchaguzi
Hii kwanza ingempa fursa ya kuweka mambo sawa ndani ya Chama pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ambayo yatakuwa rafiki kwa kila mwana chadema ,kuwa familiar na sera na malengo ya Chama pamoja na kuwa na mipango thabiti katika kuchukua dola ya nchi hii
Chama kuwa imara ni pamoja na kutengeneza mifumo mizuri ya kupata pesa ambazo zitawezesha Chama kufanya shughuli zake za siasa bila kikwazo chochote kile,na hii inawezekana tu pale Kiongozi Mkuu atakapo unganisha nguvu ya Viongozi pamoja na Wanachama wake
Sasa kabla hilo halijafanyika tayar Chama kimeingia katika mapambano mengine ambayo yanahitaji nguvu ya pamoja na umakini mkubwa sana
Kuonyesha kwamba bado Chama kingehitaji kujijengea misingi ya kukiimarisha kabla ya kwenda kwenye hatua ya pili ya No Reform No Election,ni kuibuka kwa kundi linalo jiita G55
Hili ni kundi moja ambalo limethubutu kupaza sauti na kujitoa mhanga lakini naamini nyuma yake kuna watu kama hao wengi ambao naamini kabisa wanaunga mkono ajenda ya G55
Kama Chadema kingeweka ajenda ya NRE pembeni kwanza na kujikita kuimarisha chama kwa maana ya kutoa tofauti zote na majeraha baada ya uchaguzi ingekuwa ni move nzuri sana kuelekea katika mapambano makubwa zaidi
Lakini kama Chadema kingeamua kushiriki Uchaguzi pamoja na changamo nyingi,bado kingepata viti kadhaa serikali za mitaa na viti vya ubunge na hivyo kuwa na sauti katika kuchagiza uwepo wake na uhamasishaji wake kisiasa
Lakini kwakupata viti bungeni kungesaidia kwanza kuwa na ushawishi kama Chama kwakuwa sauti yake itasikika zaidi na pili wangepata ruzuku ambayo ingewawezesha kusaidia harakati zake za kuimarisha shughuli za Chama
Nachelea kusema kwamba kwa siasa za nchi hii Chadema haitaweza kuzuia Uchaguzi na badala yake kitakuwa kimejichimbia kaburi lake lenyewe
Na wananchi wa nchi hii sio wajasiri kama wa nchi ya jirani,lau wangekuwa wajasiri wangeweza kuleta mabadiliko ya maandamamo yasiyo na ukomo lakini sio wananchi wa Tanzania hii ninayo ijua
Mda Utaongea
Ni hayo tu!