Mtazamo wangu juu ya tozo za miamala

Wabike kenedy

New Member
Jul 17, 2021
3
0
MTIZAMO

AGIZO LA RAIS, WAZIRI WA FEDHA PAMOJA NA WAZIRI MKUU JUU YA MABADILIKO YA TOZO ZA MIAMALA

Wakati tozo mpya za miamala zinatangazwa, nilikuwa miongoni mwa watu waliounga mkono wazo hilo la Solidaty Fund

Nililiunga mkono kwa kuzingatia lengo lake pamoja na matarajio yake. Miongoni mwa malengo mahususi ilikuwa ni;

1.Ujenzi wa zahanati 900 na vituo vya Afya 114

2. Serikali kutenga Bil.45 zinazotokana na tozo kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma 900 ya zahanati, na ujenzi wa zahanati 1656 ambazo zingegharimu kiasi Cha shillingi Bil. 83.15

3. Billion.322.158 kutoka kwenye tozo zitakazosaidia ukarabati wa barabara za udongo kwenda changalawe.

4. Kuweka mpango wa trillion 5 kwenye mzunguko zitakazotokana na tozo

5. Kwamba Serikali ilipitisha tozo hizo ili kunusuru deni letu la Taifa la kiasi Cha tsh. tril.60.9 libaki kuwa himilivu. Maana yake Serikali isikope fedha kwa ajili ya miradi hiyo ili kubakisha deni lisivuke barline ya kukopa.

Hiyo ndo ilikuwa ni misingi yangu ya kulikubali wazo, na nililisapoti kwa kuwa na uhakika kwamba, wizara imejaa wataalam wa maswala ya uchumi na fedha ambao kazi yao ni kutafuta mitaji, kuwekeza, kujua athari za vyanzo vya Kodi na Mambo mengine yahusuyo fedha na uchumi.

KUHUSU UCHAMBUZI WANGU JUU YA MABADILIKO HAYO
kwanza
si Jambo geni kuona Rais anaingilia Kati juu ya swala ambalo wananchi wanalalamikia, alishafanya hivi Nyerere kipindi wabunge wamepitisha Sheria ya kupanda kwa unga wa sembe na alishawahi kufanya hivi Rais Magufuri kipindi Bunge limepitisha kikokotoo kwa watumishi.

Lakini hebu tuangalie mchakato wa upitishwaji wa muswada kabla haujawa sheria;

a) muswada husomwa mara ya kwanza
b) Muswada hupelekwa kwenye kamati za bunge
c) muswada kusomwa mara ya pili
d) muswada kufanyiwa kazi na kamati ya Bunge zima
e) muswada kusomwa mara ya tatu
f) muswada kupata ridhaa ya rais
g) kuanza kutumika kwa Sheria.

Nimeona niwapitishe hapo juu ili kuona kwamba ili Sheria ipite ni lazima ipitie michakato mingi na Rais ni mhusika mkuu wa kupitisha muswada ili uanze kutumika kama Sheria.

Rais kasema tozo hizi hapana, waziri kasema malalamiko ya wananchi yamepokelewa na yanafanyiwa kazi huku waziri mkuu akiitisha kikao Cha dharula Cha kupitia upya tozo hizi. Sasa nina maswali yafuatayo;

1. Je, Rais alisaini muswada huo bila kusoma?. Kama hakusoma maana yake alidanganywa na washauri wake wa kiuchumi na fedha, Je, kitu gani amefanya kwa washauri wake hao?

2.Bila shaka kujadili huko watakuja na njia mbadala za kupunguza tozo au kuondoa kabisa. Je, miradi iliyopangwa itakamilika?, fedha zilizokuwa zimepangwa zitatoka wapi?.

3. Wakati tunatarajia Mabadiliko mapya sheria hiyo bado inaendelea kutumika na wananchi wanaendelea kukatwa. Je, Serikali itawarudishia wananchi pesa zao na fidia endapo mapendekezo yatakuja na tozo pungufu au kufutwa?.

MAONI YANGU
Kwenye uchumi ukifanya kosa kidogo madhara yake ni makubwa. Kama wizara pamoja na wabunge walijiridhisha na mpango huu na kuona una faida, Serikali ilibidi ishikilie msimamo bila kusikiliza malalamiko ya wananchi mtandaoni maana baadae wananchi hao hao wangekuja kupongeza Kama kweli mfuko huo ungekuwa na faida kwa wananchi.

Alichokuwa anakisisitiza Mwiguru kuwa baadae tutakuja kufurahi huo ndio ungekuwa msimamo. Lakini kitendo Cha kurudi nyuma inaonyesha ni jinsi gani Serikali ilikuwa inawadanganya wananchi na inapunguza hadhi ya uwezo wa viongozi wa wizara, Ofisi ya Rais pamoja na Wabunge.

Haya mazoea ya kusubiri malalamiko ya wananchi wanasemaje si hali nzuri ya kwenda nayo kiuongozi. Nakumbuka Dk. Hassan Abas akiwa katibu wizara ya habari alisema hivi "Wasanii wanatakiwa kutokutumia kiki ili wawe maarufu bali uwezo na ubunifu ndivyo viwe nyenzo", Hii naihusianisha na kitendo Cha viongozi wakuu kusubiri sisi wananchi tunasemaje mitandaoni bila wao kusimamia kile wanachokiamini.

•Makato yasitishwe na Sheria isitishwe wakati Mabadiliko mapya yanajadiliwa ili kuzuia wananchi kuendelea kuathirika kwa kile walichokiona viongozi kuwa malalamiko ya wananchi ni ya msingi.

*KENEDY WABIKE
Phone; 0742272881
Email;wabike.2020@gmail.com
 
Back
Top Bottom