Mtazamo juu ya vijana wa sasa

Ni kweli kabsa mkuu lakini unahisi nini kifanyike ili kuondoa hilo tatzo miongoni mwetu vijana maana changamoto ni nyingi sana
Issue ninayo ona inafaa hapa kwa yale niliyoyaona basi vijana wanatakiwa wapewe kipaimbele sana katika jamii zao, wasikilizwe, kwenye kuwasikiliza utapata cha kuwashauri, ninalosema nimeliona mataifa 18 ya ulaya ikiwemo Uingereza, nimekuja Tanzania nimeliona kwa ukubwa, hapa Marekani ndio habari kuu yani vijana wamekuwa tishio kwa siku za usoni..
 
Ningekuwa raisi na power ningemtafuta a man behind the compaign of KATAA NDOA nimsweke ndani ndo chanzo cha yote haya
Sikubaliani na hilo, nimeona ni mfumo wa maisha ndio umeleta haya, kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye mfumo wa maisha ya sasa, kuanzia malezi ya nyumbani, elimu, gharama za maisha, utamaduni mpya, na zaidi Umaskini.
 
Umasikini ukizidi unamfanya mtu kuwa fukara na ufukara ukizidi unampelekea mtu kuwa na matatizo ya akili
Matatizo ya afya ya akili yanachukuliwa kama suala la kawaida ila ni janga kubwa na haribifu siku za usoni, tuna kila sababu ya kusimama kupunguza hili katika jamii zetu.. mauaji yataongezeka kutokana na hili, watu kujidhuru wenyewe,watu kuishi maisha mabaya zaidi kwa sababu ya kukata tamaa, yote haya tutayaona siku sii nyingi
 
Ninawaza ni jinsi gani maisha yamebadilika na kwa jinsi ninavyokaa na vijana kuwasikiliza mawazo yao, ninapata majibu kuwa miaka 10 ijayo kutakuwa na ongezeko kubwa la watoto wa mitaani na vifo kutokana na changamoto ya Afya ya akili vitaongezeka sana.
Kweli tunaelekea pabaya sana siku hizi. Itabidi wazazi wafanye kitu kabla mambo hayajaharibika zaidi.
 
Kwani vijana wenyewe wanasemaje? Tuwasikilize kama ulivyoshauri.
 
Kuna ule utafiti ulifanywa kuhusu Vijana embu utafute unamajibu ya Uzi wako wote huu
Kati ya Vijana 10 ni mmoja tu ndo ana adabu au heshima inayostahili
 
Back
Top Bottom