pilimichuma
Member
- Apr 8, 2011
- 42
- 21
Nadhani kila mtu hasa wasomi (wahitimu) wanandoto za kuoa na kuolewa labda na msomi mwenza au raia mwingine tu wa kitaa (BIG UP). Napenda kutoa mtazamo tu juu ya hili, usikurupuke na kufuata mkumbo wa wengine, itakula kwako. Fanya hili
.tenga kipindi labda 2-3 years au zaidi ukiweza na fanya yafuatayo ukiwa na mchumba ama single (Ukiweza fanya
.yakikushinda mh! Mwachie Ngoswe):
Wengi wetu huko majumbani kuna mashimo ya kufukia hasa yaliyosabishwa na sisi wahitimu au ndugu, jamaa na marafiki. Tafuta kazi kwanza au hata temp. jobs ,utakachokipata kiasi rudisha maskani kwa madogo na wanajeshi wengine (FUKIA MASHIMO NA NYUFA ).Mfano: Kama waliuza mbuzi usome, nunua hata bata basi ku replace. Hili ni rahisi zaidi ukiwa nje ya ndoa.
Huu ndio muda wako kama kijana msomi, have fun! Pata kazi, pata mshahara wako kuwa huru kufanya jambo lolote (bila kuvunja sheria). Sote ni vijana, hakuna asiependa bata mingi mingi. Panga na marafiki zako nini cha kufanya pamoja and have fun (popote ndani au nje ya nchi).Ni kipindi muafaka kwako,sitegemei kukuona 50 yrs unakwenda disco. Fanya kitu utakuja simulia miaka 20 ijayo(majaaliwa). Nje ya ndoa ni rahisi zaidi.
Kwa muda utakao tenga (at least 2 yrs) ni muda wako kama kijana kuanza ku experience the real life la mtaa hasa kiuchumi na kijamii. Hili litakusaidia kutengeneza principle zako za kimaisha juu ya matumizi ya mapato, urafiki, nidhamu kazini na mengine meengi! Kuishi campus, mabibo au hata mtaani ukiwa unategemea boom kama kipato its totally deferent na kuishi mtaa ukitegemea mshahara (payslip). Nje ya ndoa ni rahisi zaidi kutengeneza mfumo wako kama msomi.
Tumemaliza sote lakini kuna kuongeza elimu (hasa Masters).Ni rahisi sana kulitimiza hili ukiwa single au na mchumba (si ndoa).Maswala ya kwenda ulaya alafu watoto wanalia njaa bongo sio mpango. Ingia kwenye ndoa ukiwa umeridhika na elimu ulionayo. Kumbuka, short course hazina madhara katika hili.
La mwisho, ni rahisi zaidi kuweka msingi mzuri wa uwekezaji ndani ya huo muda utakao jitengea, ambao utekelezaji wake utakuwa ni rahisi ukija kuingia kwenye ndoa (endapo hutafanikisha mapema). Usije ingia kwenye ndoa peku peku.
NB: KUMBUKA MAISHA NI KUBALANCE
(mfano: usije tenga miaka miiingi mpaka ukawa KABABU au KIBIBI ...ooh!)
HUU NI MTAZAMO FLANI, KAMA TAYARI UPO NDANI YA NDOA USIHOFU PIA YANAWEZEKANA JAPO INAHITAJI NGUVU KIASI.