Elections 2010 Mtatiro na mogendi wako live ndani ya mlimani tv

Caren

JF-Expert Member
Feb 12, 2010
278
91
Niko kwenye kochi nimetulia nawaangalia wagombea ubunge wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CHADEMA Philip Mogendi na Juliuus Mtatiro wa CUF na mgombea jimbo la Ubungo wakijadili mada ya keki ya Taifa. Hawa vijana kwa kweli wamejiandaa kuchukua majimbo yao. Wanajua mambo kwa kweli.
 
Mtatiro sasa anaongelea tatizo la kukosa priority. Anasema priority ya serikali inatofautina na priority za wananchi
 
Mtatiro anaishukuru CCM kwa kuleta uhuru lakini anasema inalazimu sasa kuiondoa kuleta mabadiliko
 
Usalama wa Taifa wameiondoa signal ya Mlimani TV. Walikuwa wanaongelea namna madini yanavyoibiwa huko Nyamongo. hawa wanajua sana mambo ya kule maana wote wamezaliwa kule.
 
mtatiro amesema kuwa namna ya kumtawala masikini ni kumnyima elimu na fedha.
 
Duh huyu dogo anayemoderate hiki kipindi lazima ni mpinzani. Ila yuko bright. Ana info nyingi na siyo average journalist kwa umri wake.
 
Mogendi sasa anaongelea namna serikali ya CCM ilivyosahau wananchi na kuweka mikataba ya ovyo. Anasema ili nchi hii iendelee inahitaji kiongozi wa aina ya slaa.
 
Kipindi kimeisha. My take both Mogendi and mtatiro wanstahili kwa kweli kuwa wabunge wetu wa ubungo na kinondoni. Ni vijana na wanajua kila wanachokisema na natumaini watasimamia kile wanachokiamini.
 
Kipindi kimeisha. My take both Mogendi and mtatiro wanstahili kwa kweli kuwa wabunge wetu wa ubungo na kinondoni. Ni vijana na wanajua kila wanachokisema na natumaini watasimamia kile wanachokiamini.

jimbo la mnyika hilo, kinondoni sina uhakika sana.
 
Niko kwenye kochi nimetulia nawaangalia wagombea ubunge wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CHADEMA Philip Mogendi na Juliuus Mtatiro wa CUF na mgombea jimbo la Ubungo wakijadili mada ya keki ya Taifa. Hawa vijana kwa kweli wamejiandaa kuchukua majimbo yao. Wanajua mambo kwa kweli.

Akina Mtatiro na wengineo ni wasindikizaji tu. Mbunge mtarajiwa ni Bw John Mnyika yu tele kitini anasubiri kula kiapo aanze kuleta mageuzi.
 
akina mtatiro na wengineo ni wasindikizaji tu. Mbunge mtarajiwa ni bw john mnyika yu tele kitini anasubiri kula kiapo aanze kuleta mageuzi.

Anaechagua ni mpiga kura na si haki kudai mgombea tayari kashachaguliwa anangojea kuapishwa!! Hii inatutia wasiwasi labda huwenda huyo munaedai anangoja kuapishwa anafanya kazi na usalama wa taifa? Jee hapa si kuna harufu ya kuiba kura!! Maana nilisikia kuna mgombea mmoja wa urais toka kambi ya upinzani aliedai kuwa nusu ya usalama wataifa huripoti kwake!!!

Sasa hii maana yake nini kututangazia kuwa mbunge wa ubungo tayari ameshachaguliwa anangoja kuapishwa? Inamaana hana mpinzani? Alipitishwa na tume ya uchaguzi kuwa mgombea pekee?

Wacheni propaganda zilizopitwa na wakati na waacheni wananchi wampigie kura mgombea wanaemtaka ili nchi iweze kuendeshwa ki demokrasia!!!
 
Back
Top Bottom