Mtamile
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 2,838
- 1,267
Kupitia ukurasa wake facebook Mtatiro amesema hivi
SOURCE: Mtatiro FacebookJulius S. Mtatiro
NCHI HII ITAMALIZWA;
Tunafahamu kuwa kuna njama zinapangwa ili wajumbe wa bunge la
katiba ati waongezewe fedha zaidi.
Hoja hii imetolewa leo hii na mmoja wa wajumbe huku ikionekana
kuwa maarufu na inayoungwa mkono na baadhi ya wajumbe, hasa
wabunge wa CCM.
Binafsi na wenzangu wengi tumepanga kutumia kila uwezo kuzuia
nia hiyo OVU, ifikie wakati tuambiane ukweli vinginevyo nchi hii
watu watakufa masikini.
Shilingi laki tatu tunazopewa kwa siku zinatosha kabisa, ambaye
hazimtoshi aongeze za kwake, na ambaye anaona hawezi kuongeza
zake aondoke Dodoma ili kupisha wanaoweza kutunga katiba kwa
posho ya shs 300,000 waendelee.
Laki tatu tunazopata zinatosha kila kitu na CHENJI inabaki, zinatosha
kula, kulala, kumpa dereva na kuishi Dodoma.
Lazima sisi tunaotunga katiba tufahamu kuwa maisha ya wananchi
ni muhimu na kwamba wana mahitaji yasiyokwisha hata baada ya
bunge hili.
Baadhi yetu tulioko humu bungeni tutakataa jambo hili kwa
maneno na vitendo. Wakipitisha kwa wingi wao tuta-boycott
kuzipokea.
Kenya pale mnakumbuka hoja ya wabunge kujiongezea mapesa
ilipingwa vikali na wananchi waliandamana hadi nje ya ukumbi wa
bunge. Hapa Tanzania hata zikiongezwa milioni kila siku hutaona
mwananchi anachukua hatua kwa vitendo, kuoneshwa
kutoridhishwa kwake.
Tuna tatizo kubwa sana, sisi viongozi na wananchi wetu. Kuna mtu
anasema, viongozi ni zao la jamii hiyohiyo.
Tuungane pamoja kusimamia jambo hili, ninyi mlioko nje na sisi
tulioko ndani.