Mtatiro afichua kilichomfanya ajiunge na CUF

Mtatiro afichua kilichomfanya ajiunge na CUF

Mzito Kabwela

Platinum Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,908
Reaction score
7,751
Naibu katibu mkuu wa CUF chama cha wanachi Mh.Julius Mtatiro,amebainisha kwamba nchi inakuwa na viongozi mafisadi wengi kwa kuwa wengi hawana nia ya kuongoza ili kumkomboa mtanzanaia bali kukomboa matumbo yao.

Mh. Mtatiro aliamua kuweka wazi kile alichokiweka moyoni kwa muda mrefu kwamba kabla ya kujiunga na chama chochote cha siasa alifuatwa na vyama vyote vikubwa vya siasa hapa nchini wakimsahawishi ajiunge kwenye vyama vyao,lakini alivutiwa sana na ilani/itikadi , sera ya CUF kama alivyo tanabaishawa na Prof.Lipumba (mwanyekiti wa CUF ) ambaye ambaye alifanya mazungumzo nae, amabaye Mtatiro ansema yeye alikuwa tofauti na viongozi wa vyama vingine ambao walimuahidi,nyumba,gari,fedha na vyeo."Hii haikuwa interest yangu mimi niliangalia chama gani chenye siasa za kweli na kinawatetea watanzania bila fix" alieleza Mtatiro.

mtatiro.jpg
Naibu Katibu mkuu wa CUF mh.Mtatiro akihutumia wananchi Ndungumbi,Makanya,Kinondoni

Mtatiro pia ameonya tabia ya viongozi wa Chadema ya kununua viongozi wa CUF kwa fedha nyingi kama wanavyofanya CCM.Mtatiro alisema kwamba tabia hii ianjenga viongozi wachumia tumbo na wasio na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi ambao wengi wanakuwa mafisadi na wachumia matumbo."Prof.Lipumba aliniambia -karibu CUF, hili ndilo neno ninalolikumbuka kwa kweli yeye ndiye aliyekuwa kiongozi pekee wa chama cha siasa ambaye hakujinadi kwa kutumia fedha.Kiufupi mimi huwezi kuninunua kama inavyofanyika kwa wengine kwani najitambua"aliongeza mh.Mtatiro

Naibu katibu mkuu huyo wa CUF aliendelea kutanabisha kwamba wanaushahidi wa sauti wa namna viongozi hao wa Chadema walivyokuwa wakihangaika kuwarubuni viongozi wa CUF mikoa ya kusuni kwa kutumia ahadi za kuwapatia fedha pale watakapohama CUF na kuhamia Chadema wakati wa ziara yao ya mikoa ya kusini hivi karibuni.

Mh.Mtatiro alitanabaisha hayo juzi kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika uliofanyika kata ya Ndugumbi Kinondoni ambapo kada muhimu wa CCM alihamia CUF na kushusaha bendera ya CCM kwenye tawi lake na kupandisha bendera ya CUF na kuunda tawi la CUF Mkombozi.
 
Janatu Firdaus
Hapa nadhani ajadiliwe Mtatiro kama mtu kwa kuwa KAFU kama chama hakuna .Namuonea huruma dogo kachukua ukanjanja wa wazee wa vikofia ila nadhani he is smart anawala sana mapesa yako na siku anaondoka huko sijui atarudi CCM ? Maana chama makini hawawezi kumtaka.
 
Last edited by a moderator:
Eh aliahidiwa ukuu wa wilaya na ccm akagoma, CUF walimwahidi UENYEKITI sasa anausubiri!..
 
cuf hakuna jipya sera za maji taka! wewe mtu na akil unakuwa na hoja za kusema cdm kwan nch iko mikonon mwa cdm!
 
Alikurupuka CDM haiwezi kununua mtu kutoka CUF labda aamue kujiunga nayo kwa ridhaa yake mwenyewe, maana muungano wa chama hiki na magamba huko zenji kimeiua hapa bara, rejea hata matokeo ya uchaguzi mdogo wa Igunga CDM haikusimamisha mtu mara ya kwanza, lakini kwenye by-election moto wake ulionekana, na mpaka sasa unaendelea maana ushindi wa kufoji wa Kafumu ulitenguliwa na mahakama.
 
Mbona tunasikia yupo mguu ndani mguu nje kwenda ADC?
Siku akihama atafichua kitakachomhamisha? Kweli siasa ni
si hasa, kwa maisha gani aliyonayo ya kukataa pesa?!...
 
Atuambie ile Noah na kile cheo cha haraka haraka ndani ya Cuf alitunukiwa au ilikuwa takrima?
 
cdm kunnua viongozi wa cuf!!!aweke huo ushahidi wa kupikwa na usalama wa taifa(ccm)..tokea ccm waingize mtambo wa kufoji sms imekuwa tabu kila mwana ccm anasema ana ushahidi..
 
Mtatiro aliambiwa na chadema kuwa kama yuko tayari kuwatumikia wananchi ajiunge chadema lakini hatuna mishahara minono na vyeo vya kugawa, kwahiyo akaamua kwenda cuf kuwa naibu katibu mkuu na kulipwa mshahara mnono! Aache unafiki!
 
Mtatiro nimesoma nae Ifakara High school namtambua vema kama kilanja wa chakula alivyokuwa na roho mbaya, tukaenda nae UDSM namfahamu uwezo wake mdogo sana anaweza lopoka kama hapa ka-print kadi ya CDM hii inaonekana ni mpya kabisa yaani huyo mwanachama wa chadema alijiunga asubuhi... tena hata hakuikuja kadi jioni akairudisha CUF... shame on you Mtatiro, na nimemuona mdogo wako Malima CUF umempa shavu gani?
 
Wanasiasa wajifunze kwenda na wakati. Siasa chafu kwa siku hizi ni kitanzi kwa yule asiyejilewa. Kazi kuropoka wanapotafuta kuungwa mkono. Enzi hizi za sayansi na teknologia kinachoweza kudhihirisha uweli ni vielelezo asilia. Angeonesha video tumuone alivyokuwa ndani ya mazungumzo au arushe hewani kwenye redio mazungumzo hayo. Poor politics kila wakati kutuzuga tu!!!!!
 
hii kutoka CDM ukaenda CUF ni sawa na kutupa bunduki ukanunua fimbo[/QUOTE
Kweli kabisa uanze tu kuhama cdm nakuenda ccm b ! Angalia kadi ya cdm ilivyompya ?angalia za ccm A ZILIVYOCHAKAA hIZO NDO ZILIZORUDISHWA LKN SI ZA CDM

]
 
Naibu katibu mkuu wa CUF chama cha wanachi Mh.Julius Mtatiro,amebainisha kwamba nchi inakuwa na viongozi mafisadi wengi kwa kuwa wengi hawana nia ya kuongoza ili kumkomboa mtanzanaia bali kukomboa matumbo yao.

Mh. Mtatiro aliamua kuweka wazi kile alichokiweka moyoni kwa muda mrefu kwamba kabla ya kujiunga na chama chochote cha siasa alifuatwa na vyama vyote vikubwa vya siasa hapa nchini wakimsahawishi ajiunge kwenye vyama vyao,lakini alivutiwa sana na ilani/itikadi , sera ya CUF kama alivyo tanabaishawa na Prof.Lipumba (mwanyekiti wa CUF ) ambaye ambaye alifanya mazungumzo nae, amabaye Mtatiro ansema yeye alikuwa tofauti na viongozi wa vyama vingine ambao walimuahidi,nyumba,gari,fedha na vyeo."Hii haikuwa interest yangu mimi niliangalia chama gani chenye siasa za kweli na kinawatetea watanzania bila fix" alieleza Mtatiro.

mtatiro.jpg
Naibu Katibu mkuu wa CUF mh.Mtatiro akihutumia wananchi Ndungumbi,Makanya,Kinondoni

Mtatiro pia ameonya tabia ya viongozi wa Chadema ya kununua viongozi wa CUF kwa fedha nyingi kama wanavyofanya CCM.Mtatiro alisema kwamba tabia hii ianjenga viongozi wachumia tumbo na wasio na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi ambao wengi wanakuwa mafisadi na wachumia matumbo."Prof.Lipumba aliniambia -karibu CUF, hili ndilo neno ninalolikumbuka kwa kweli yeye ndiye aliyekuwa kiongozi pekee wa chama cha siasa ambaye hakujinadi kwa kutumia fedha.Kiufupi mimi huwezi kuninunua kama inavyofanyika kwa wengine kwani najitambua"aliongeza mh.Mtatiro

Naibu katibu mkuu huyo wa CUF aliendelea kutanabisha kwamba wanaushahidi wa sauti wa namna viongozi hao wa Chadema walivyokuwa wakihangaika kuwarubuni viongozi wa CUF mikoa ya kusuni kwa kutumia ahadi za kuwapatia fedha pale watakapohama CUF na kuhamia Chadema wakati wa ziara yao ya mikoa ya kusini hivi karibuni.

Mh.Mtatiro alitanabaisha hayo juzi kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika uliofanyika kata ya Ndugumbi Kinondoni ambapo kada muhimu wa CCM alihamia CUF na kushusaha bendera ya CCM kwenye tawi lake na kupandisha bendera ya CUF na kuunda tawi la CUF Mkombozi.

Mtatiro hana uzito wowote kwa siasa za Tanzania. Level yake ni Nape wote waropokaji
 
ndoa ya mkeka ya zanzibar imeifanya cuf kikawa chama ambacho siyo makini badala ya kueleza madudu ya mumewe ccm anahangaika na CDM wanapoteza muda tu.
 
Kujifanya unarudisha kadi ya SISIEM na kuchukua kadi ya SISIEM B kuna tofauti gani
 
Back
Top Bottom