Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,475
Mkuu shukran kwa kuscan hii habari, nimeisoma yote neno kwa neno. A lot of parliamentary boilerplate, but a lot of meaningful heated debate too.
1. Ndugai kwa kwenda kwenye kimjadala kisicho mizani na kujibishana na Tundu Lissu kama Naibu Spika, bila ya kuwa na uwakilishi rasmi wa CCM, na hivyo kutoa picha kwamba anawakilisha CCM, amedhalilisha bunge kuliko gazeti lolote linavyoweza kufanya.
2.Ndugai anajichanganya kwa kusema bunge linadhalilishwa, halafu hapo hapo kusema anajua kuna uhuru wa vyombo vya habari. Hivi huyu mwanasheria? Kama unajua kuna uhuru wa vyombo vya habari, na bado unasema bunge limedhalilishwa, inabidi uonyeshe kwamba bunge limedhalilishwa kwa kadiri ya kupita kiwango cha kawaida cha kubanwa na vyombo vya habari ili kulihasibu, hakuonyesha hili.
3. Habari nzima haionyeshi Ndugai kutaja specifics za udhalilishaji wa gazeti na kuzikanusha. Bunge si dini kusema haliwezi kusemwa. Hata hizo dini zinasemwa, mitume wanasemwa.
4. Kuna some very serious allegations ambazo nchi yoyote makini zingefanyiwa kazi. Mbunge amesema bungeni kwamba wabunge wa CCM wanawaambia wabunge wa upinzani kwamba wanapigiwa simu za vitisho kupitisha bajeti. Hili ilikuwa si suala la kusema tu, hili lilikuwa suala la kuliforce bunge kufanya uchunguzi na kuandika ripoti, nani anatoa vitisho hivi? Kwa maslahi ya nani? Kama kuna mtu anadhalilisha bunge basi ni huyu anayetoa vitisho kwa wabunge, lakini mbona hatusikii huyu kufuatiliwa ? Ndugai anabaki kutoa kanuni rejareja kushutumu magazeti tu?