As Salafiyyu91
JF-Expert Member
- Jan 11, 2014
- 2,537
- 2,530
Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha na Mipango, mwaka 2015, Tanzania ilikadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 47.4. Hii ina maana kwamba katika deni la taifa la sasa la Sh. trilioni 43.5, kila Mtanzania atatakiwa kulipa Sh. 915,937 ili kulimaliza.
Akiwasilisha mapendekezo ya kiwango cha ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17 katika mkutano wa wabunge jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema deni la taifa limepanda kutoka Dola za Marekani bilioni 19.69 (Sh. trilioni 43) ilivyokuwa Juni 2015 hadi dola bilioni 19.93 (Sh. trilioni 43.5) Februari mwaka huu.
Dk. Mpango alisema katika ongezeko hilo la asilimia nne, deni la serikali ni Dola bilioni 17.594 (Sh. trilioni 38.4) wakati Dola bilioni 2.336 (Sh. trilioni tano) ni deni la sekta binafsi.
"Kuongezeka kwa deni kulitokana na mikopo mipya hususan yenye masharti ya kibiashara ndani na nje kwa ajili ya kugharimia miradi mbalimbali ya maendeleo," Dk. Mpango alisema na kuongeza:
"Mikopo ya kibiashara ina gharama kubwa na inaongeza mzigo mkubwa kwa serikali katika kulipa riba na mtaji."
Licha ya deni la taifa kuzidi kukua, waziri huyo alisema serikali itaendelea kukopa, lakini itakopa kwa uangalifu."
"Tathmini ya uhimilivu wa deni la taifa (Dept Sustainability Assessment) iliyofanyika Septemba 2015, ilionyesha kuwa deni la taifa ni himilivu kwa kutumia vigezo vya kimataifa," alisema na kuongeza:
"Hata hivyo, serikali itaendelea kukopa kwa uangalifu ili kuhakikisha kuwa gharama za kulipia mikopo haziongezeki kwa kasi na hivyo kutoathiri Bajeti ya Serikali."
Chanzo: NIPASHE