Aventus
JF-Expert Member
- Mar 8, 2013
- 2,011
- 2,165
.., ndugu mtanzania mwenzangu, wewe hapa unaelewa nini..,!? Tazama kwa makini..,
1. Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameiondoa mahakamani kesi ya Akaunti ya Tegeta ESCROW iliyokuwa ikimkabili Mhandisi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), Theophillo Bwakea ya kupokea Tsh 161,700,000/- kutoka kwa James Rugemalira.
2. Kesi iliyokuwa ikimkabili Ndama Hussein maarufu kwa jina la 'Ndama Mtoto wa Ng'ombe' yaahirishwa hadi 6-1-2017 baada ya upande wa mashtaka kusema hawana jalada la Polisi...,
3. Kassim Salum (mwenye umri wa miaka 18) mkazi wa Dar es Salaam, amehukumiwa kwenda Jela, kifungo cha Maisha kwa kosa la kuiba simu aina ya TECNO (yenye thamani ya Tsh 110,000/-) na kujeruhi..
4. Mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona waliokuwa wakitumikia adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela, wamebadilishiwa adhabu kuwa kifungo cha nje na sasa watakuwa wanafagia Hospitali ya Sinza, Palestina kwa saa nne kila siku.
NB; Mramba na Yona, walitiwa hatiani kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.5 bilioni, kwa kuisamehe kodi Kampuni ya Ukaguzi wa Madini ya M/S. Alex Stewart Government Business Assayers ya Uingereza.
..., mimi naona mapicha-picha ya kiyahudi tu.., au ndiyo tafsiri ya mwenye kuwa nacho, ataongezewa na kuwa na kikubwa zaidi '!?
~ Martin Maranja Masese (MMM)