TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam


Habari za hivi punde ni kuwa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Ndugu Ephraim Kibonde amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 7 Machi 2019.

Kibonde alianza kusumbuliwa na presha akiwa katika msiba wa marehebu Ruge Mutahaba huko Bukoba mkoani Kagera na kuhamishiwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambapo mauti yamemkuta.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa

Mwaka jana Ephraim Kibonde alimpoteza mkewe mama Sara Kibonde. Zaidi soma >TANZIA: Ephraim Kibonde afiwa na Mke wake Sara Kibonde - JamiiForums

View attachment 1039958
Ephraim Kibonde akiwa na mkewe enzi za uhai wao​
R.I.P.Ephraim.Lakini ni nini hasa kinaendelea Clouds?Ni swali ambalo persobally linani-disturb sana.
 
Write your reply...
hapa kuna kitu,mkuu wa ukoo inabidi aitishe kikao cha dharula na wazee wenzake ili kuagua huenda kuna mtu media anatafuna wenzake
 
Clouds inaweza kupitia kipindi kigumu. Hali inayoonekana au inayotokea kwasasa ni hali ya matukio, ambayo inaweza kupelekea Clouds kupita katika kipindi kigumu, kwa kampuni na wafanyakazi wake.

Ifahamike kuwa, Ruge alikuwa kiongozi mkubwa, na alifahamika kama Boss Ruge. Ieleweke vizuri kuwa, hakuna mfanyakazi aliyeko kazini hasiyempenda boss wake. Kila mfanyakazi huwa na tumaini/hisia/mapenzi ya dhati na boss wake, hata kama hawaongei mara kwa mara. Utendaji wa Boss Ruge, ulimgusa kila mfanyakazi wa Clouds, kwa namna moja ama nyingine. Kama watanzania wameguswa kiasi cha juu, inakuwaje kwa wafanyakazi wa clouds?

Ushauri ni huu: Wapate muda wa kupumzika. Katika kipindi hiki cha mapumziko, wapate mtaalamu wa masuala ya Psychology kutokea nje ya kampuni yao ili kuja kuongea na wafanyakazi. Najua kuwa, clouds ina wafanyakazi wenye talent kubwa ya utangazaji, na zaidi wenye uelewa mkubwa sana wa masuala ya kijamii. Ila kwa kipindi hiki, wanahitaji mtu wa nje yao, kuja kuongea nao. Hii itasaidia kuwaongezea kitu kipya ambacho kitawasaidia kuwawezesha kuzidi kuwa na uthubutu wa akili, na uwezo wa mwili kuhimili mikiki ya kazi, hasa kipindi hiki kikiisha. Pia, kuhimili hisia na furaha, hasa kuhamisha mawazo yao kutoka kwa mpendwa wao Ruge, na kujenga upya hisia/furaha zao kwenye maisha yao.

Ruge ameshatangulia mbele za haki, na ameishaimaliza kazi yake hapa duniani.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Clouds. Amen!..

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila shaka wewe ni mhaya maana neno "ameshamaliza" nyie mnaandika/tamka "ameishamaliza"
Btw umeeleweka mkuu....
 
Hata mimi najua,but that might not be all.Kuna nini Clouds nyuma ya pazia?


Hahahaha dah nacheka kama mazuri...............sasa hivi CCTV Camera itaangazia upande wa ile Radio mupya ya wandengereko..... hah

RIP Kibonde, nenda kaka.
 
UMUHIMU WA KUJIWEKA TAYARI


Mahubiri ya Neno la Uzima - Na Mtumishi wa Mungu Askofu Mkuu Zachary Kakobe

Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org
Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries
Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe



SOMO: UMUHIMU WA KUJIWEKA TAYARI

Leo, tunajifunza Biblia zetu katika MATHAYO 24:42-51 na 25:1-13. Katika mistari yote hii, tunajifunza juu ya
kujiweka tayari. Tutayagawa mafundisho tunayojifunza katika mistari hii, katika vipengele vitatu:-

(1) KUKESHA NA KUJIWEKA TAYARI WAKATI WOTE (24:42-44);

(2) MTUMWA MWAMINIFU MWENYE AKILI (24:45-51);

(3) MFANO WA WANAWALI KUMI (25:1-13).


(1) KUKESHA NA KUJIWEKA TAYARI WAKATI WOTE

(24:42-44) – Nyakati za Biblia, wakati wa usiku, uligawanywa katika ZAMU NNE, au vipindi vine. (LUKA 12:38; MATHAYO 14:25). Kila zamu, ilikuwa na muda wa saa tatu kuanzia saa 12 jioni hadi 3 usiku ilikuwa ZAMU YA KWANZA. Kuanzia saa 3
usiku hadi saa 6 usiku ilikuwa ZAMU YA PILI. Kuanzia saa 6 usiku mpaka saa 9 usiku, iliitwa ZAMU YA
TATU; na saa 9 usiku hadi saa 12 asubuhi, iliitwa ZAMU YA NNE. Mwenye nyumba kama anagaliijua ni
zamu ipi ambayo mwivi angekuja, angalikesha na kuwa macho, wala asingeliiacha nyumba yake kuvunjwa.
Kuna mambo kadhaa ya kujifunza hapa:-

1. BWANA ANAYEKUJA – Bwana anayekuja, ni Yesu. Kama alivyochukuliwa kwenda juu mbinguni,
atakuja tena jinsi iyo hiyo (MATENDO 1:10). Yesu, ndiye Mhukumu au Hakimu wa Ulimwengu (YOHANA
5:22; MATENDO 10:40-42). Kuja kwake kunaambatana na HUKUMU. Atakuja kwetu bila taarifa yoyote
kama mwivi.

2. NYUMBA ITAKAYOVUNJWA – Nyumba ni mtu mwenyewe (WAEBRANIA 3:1-3; 2 WAKORINTHO
5:1-2). Ikiwa hatutajiweka tayari, Yesu Kristo atakapokuja kama mwivi, atatuvunja na kutuharibu kwa
hukumu yake. Ikiwa atatukuta tunakesha na kuzilinda nyumba zetu, ndipo nyumba zetu zitakapokuwa
salama yaani ndipo tutakaposalimika.

3. SIKU ATAKAYOKUJA BWANA WETU – Kwetu sisi tulioko duniani, siku atakayokuja kwetu Bwana
wetu Yesu, kama mwivi; itakuwa katika sehemu mbili:-
(a) SIKU YA KUFA – Kwa wengine kati yetu, siku yao ya kufa, ndiyo itakayokuwa siku ambayo Yesu
kama Hakimu atawajia kama mwivi. Baada ya mtu kufa, inafuata hukumu (WAEBRANIA 9:27). Wakati mtu
anapokufa, ndipo Yesu anapomwijia kumhukumu. Kufa siyo ugonjwa wala uzee. Watu waliokuwa wazima
wamekufa kwa ajali na kuwaacha wagonjwa hospitali hawajafa. Watoto wengine wamekufa kabla ya wazee
3/7/2019 UMUHIMU WA KUJIWEKA TAYARI | O-------------------------------------- BAADA YA KUOKOKA,TAFUTA UTAKATIFU
UMUHIMU WA KUJIWEKA TAYARI 2/3
wao (MWANZO 11:28). Hakuna mtu anayeijua siku yake ya kufa (MWANZO 27:2). Kesho, haiko mikononi
mwetu (MITHALI 27:1; YAKOBO 4:13-16). Watu wengine wanaweza kujua kwamba wakati wa kufariki kwao
umefika (2 TIMOTHEO 4:6), hata hivyo ni vigumu kuifahamu siku ya kufa. Watakatifu wamekufa na
kuwaacha waovu wakiishi. Yohana Mbatizaji na Stefano, waliuawa na waovu na wakawaacha wao wanaishi
duniani. Kwa sababu hatujui siku yetu ya kufa, inatupasa kujiweka tayari kuonana na Mungu wakati wote
(AMOSI 4:12). Tusipojiweka tayari kuzilinda nyumba zetu au nafsi zetu, siku ya kufa, Bwana Yesu atazivunja
nyumba zetu pale atakapotutupa kwenye moto wa milele.
(b) SIKU YA KUNYAKULIWA KWA KANISA (1 WATHESALONIKE 4:15-17) – Siku hii ambayo pia
haijulikaniu kwetu, itakuwa siku ya kuja Bwana Yesu kwa wanadamu wengine wote ambao watakuwa
hawajafa. Siku hiyo inaweza kuwa wakati wowote kuanzia sasa.

4. TUNACHOTAKIWA KUFANYA – 1. KUKESHA – Katika lugha ya ki-Biblia, watu wanaotenda maovu
na kuishi kinyume na Neno la Mungu, wanaitwa WATU WALIOLALA USINGIZI (1 WATHESALONIKE 5:4-
8). Watu ambao wanaishi sawa na neno la Mungu na kuwa mbali na uovu, wanaitwa WANA WA MCHANA,
WANA WA NURU au WANA WA KUKESHA. Waovu, ni wana wa giza, waliolala. Mtu aliyelala usingizi,
hana akili, hajui yanayomzunguka, anafikiri ni salama tu. Anapoamka, anaweza akajikuta kwamba alibebwa
na kuhamishwa chumba, pasipo kujijua. Ndivyo walivyo waovu, wanafikiri ni salama, lakini siku moja
watajikuta wamehamishwa na kuwa katika moto wa milele.
2. KUJIWEKA TAYARI – Kukesha kwetu, yaani kuishi sawa na Neno la Mungu, ni lazima kuambatane na
kujiweka tayari WAKATI WOTE na siyo wakati tunapokuwa katika ibada kanisani au katika vikosi vya
maombi. Wakati wote ni lazima tuwe tayari kuonana na Mungu bila mashaka yoyote. Tunapaswa
kuhakikisha kwamba hatuna dhambi yoyote ambayo hatujaitubu au lolote ambalo hatujalirekebisha kwa
Mungu, Watumishi wake, na wanadamu wote (WAKOLOSAI 3:5-10, 12-14; 1 YOHANA 2:1-2; 2 YOHANA
1:8).

(2) MTUMWA MWAMINIFU MWENYE AKILI (24:45-51)
Mtu yeyote aliyeokolewa, ni wajibu wake kufahamu kwamba tumeitwa na Mungu KUMTUMIKIA. Lengo la
juu la kila mtu aliyeokoka, ni kuhakikisha anawapa wengine CHAKULA au kuwalisha wengine Neno la
Mungu. Mtu yeyote ambaye Yesu atamkuta akiwalisha wengine neno la Mungu, ATAMWEKA JUU YA VITU
VYAKE VYOTE. Ni muhimu basi kuona faida ya kushuhudia, kuwafuatilia na kuwalea watoto wachanga
kiroho kwa kuwafundisha Neno la Mungu; na kuitumia vema neema ya kuwa Viongozi wa Makanisa ya
Nyumbani, Viongozi wa Zoni au Wachungaji. Inatupasa kuwalisha kondoo za Mungu kwa sababu
tunampenda Yesu aliyetuokoa na siyo kana kwamba ni wajibu wetu tu! (YOHANA 21:17). Kiwango cha juu
cha udhihirisho wetu wa kumpenda Yesu, ni kuwalisha kondoo zake. Upendo alio nao mama kwa watoto
wake ndiyo unaomfanya aone utumishi wake wa kuwatunza na kuwalisha watoto wake uwe utumishi wa
furaha. Mtendakazi yeyote pia anapaswa kufanya utumishi wa Mungu kutokana na kumpenda Yesu siyo
ilimradi atoe ripoti au ampendeze Kiongozi Fulani. Utumishi unaotokana na kumpenda Yesu, ndiyo
utakaozawadiwa. Mtendakazi yeyote ambaye atadhani Yesu anakawia, na kuanza kuwatesa na kuwaumiza
kondoo wa Mungu, kutokana na tabia yake isiyoonyesha picha ya wokovu; na kuwafanya kondoo kutaka
kurudi nyuma, huyu atatendwa mabaya na Yesu (MATHAYO 24:48-51; LUKA 12:42-48). Ni muhimu
kukumbuka kuwapa chakula kondoo wakati wake ili kukata njaa na kiu yao.
(3) MFANO WA WANAWALI KUMI (25:1-13)
Nyakati za Biblia, katika mila na desturi za Wayahudi, wanawali au mabikira 10 walikuwa wanamlaki Bwana
Arusi kwa niaba ya Bibi Arusi aliyekuwa rafiki yao. Jambo hili lilifanyika usiku, giza tu lilipoanza na
kuonekana kwa nyota. Ilikuwa ni zamu ya kwanza. Katika mfano huu, Bwana Arusi alichelewa kuwasili.
Bwana arusi ni Yesu Kristo (YOHANA 3:28-30). Watu wanaomfuata Mwana Kondoo Yesu Kristo popote
anapokwenda ni Mabikira (UFUNUO 14:4). Leo, tuna watu wengi wanaomfuata Mwana Kondoo Makanisani,
kwa nje wanaonekana kuwa sawasawa lakini kumbe katika 10, watano ni WAPUMBAVU, hawana mafuta ya
TAA. Taa inayotajwa hapa ni Neno la Mungu au KWELI (ZABURI 119:105; YOHANA 17:17). Mafuta ni
NEEMA ya Mungu. Kweli ya Kristo, ilikuja pamoja na Neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu, ni kujaribu
kuokolewa kwa matendo ya sheria; haiwezekani! (TITO 2:11-12, 3:4-8). Bwana arusi atakuja saa tusiyoidhani na ataangalia tu wale waliookolewa kwa neema, na kuishi katika mapenzi yake kwa neema hiyo. Hao tu ndiyo watakaokuwa katika harusi au furaha yake mbinguni. Wengine watafungiwa mlango. Watajaribu kutubu baada ya Dhiki Kuu kuanza, hawatasikilizwa (WAEBRANIA 12:16-17). Vilevile tujilinde na kujiweka tayari wakati wote pamoja na neema tuliyo nayo. Tusije tukalala pamoja na neema hiyo. Wengine walianza vizuri, lakini wameuacha tayari upendo wao wa kwanza, wamelala! Hawa wako pia katika hatari, inawabidi kukumbuka upesi walipoanguka na kutubu (UFUNUO 2:4-5). Tukeshe, maana hatujui siku wala saa!
…………………………………………………………………………………………………………………………………..
Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia
kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda
dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa
dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo
dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya
kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua
uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.
Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa
kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa
kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu
katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa
linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!
Amina barikiwa sana na Bwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom