Mtangazaji Khalid Gangana wa TBC aonyesha Ukengeukaji mkubwa mbele ya Makonda Studioni

Halafu nikija kuwasema humu JF mnaanza kukasirika na hadi kuninunia wakati kumbe ukweli ni kwamba mnafanya makosa makubwa sana ya Kitaalauma na Kiueledi hasa katika suala zima la Utangazaji na niwaahidi tu kuwa sitowanyamazia hadi pale mtakapobadilika.

Leo asubuhi kuanzia Saa 12 na nusu hadi Saa 1 na nusu hivi TBC1 walikuwa wakifanya mahojiano na Paul Makonda ( nachelea kumwita Mkuu wa Mkoa kwakuwa bado hajatupa uthibitisho kamili wa Cheti chake ) na Mtangazaji aliyepewa jukumu la kumhoji alikuwa anaitwa Khalid Gangana.

Binafsi kabisa leo nilitegemea kuona very hot and critical interview kutoka TBC1 na badala yake niliishia tu Kukasirishwa na aina ya Kipuuzi ya jinsi Mtangazaji wa TBC1 Khalid Gangana alivyokuwa anamhoji Paul Makonda.

Hivi Mtangazaji mahiri kweli wa TBC1 anaweza kumhoji Mtu ambaye tayari nchi na pengine hata dunia kama siyo hata Mbinguni wanajua kuwa ana matatizo makubwa na matendo ya ajabu ajabu yanayotia doa utendaji wake maswali kama haya yafuatayo?

  • Paul Makonda hivi huwa unalala Saa ngapi?
  • Naona mwili wako umejengeka sana Kimazoezi.
  • Nasikia unapenda mno mchezo wa Ndondi je ni kweli?
Nilipokuja kumuona huyu Mtangazaji Khalid Gangana kweli nae ni wa hovyo hovyo na amekengeuka tena kwa Kutukuka kabisa ni pale alipoyakubali matango pori ya Paul Makonda kuwa kwa Afrika ya Mashariki Tanzania ndiyo nchi ya Kwanza inayoongoza kwa kukua kwa Uchumi wakati ukweli ni kwamba kwa takwimu za sasa ni Rwanda ndiyo inaongoza ikifuatiwa na Kenya.

Mtangazaji huyu Khalid Gangana hakuishia tu hapo kukubali rasmi kujitolea Kwake kulishwa matango pori ( Kudanganywa ) pale ambapo tena Paul Makonda alimwambia kuwa Kidunia Tanzania ni nchi ya Tisa ( 9 ) inayokuwa Kiuchumi wakati kwa data za hivi karibuni ni nchi ya Angola ndiyo inayokuwa kwa Kasi sana Kiuchumi na Tanzania hata katika 20 bado hatupo.

Kitaaluma Mwandishi wa Habari hatakiwi Kudanganywa ( kulishwa tango pori ) na Source wake na inaruhusiwa pia kama akiona Source wake anakengeuka / anakosea basi anatakiwa kufanya kupinga na kukubali Watazamaji wake walishwe Sumu ya Uwongo uliotukuka.

Na kilichonikera zaidi huyu Mtangazaji Khalid Gangana Yeye muda wote wa Interview yake na Paul Makonda alikuwa akicheka cheka bila hata sababu ya msingi na niseme tu ukweli huwa natizama sana Interviews mbalimbali za Waandishi Nguli kabisa wa BBC, CNN na SKYNEWS na sijawahi kuona wakiwa na Characteristics kama za Mtangazaji Khalid Gangana.

Ningekuwa Mimi ndiyo Mtangazaji Khalid Gangana leo ningemuuliza Paul Makonda maswali haya yafuatayo:

  1. Ni kwanini hutulii Mkoani Kwako na muda wote unazunguka zunguka tu Mikoani?
  2. Je unazikumbuka ahadi zako ulizozitoa kwa Mkoa? Je kuna ambayo imeshafanikiwa?
  3. Nini kinakufanya usimalize huu Utata wako wa Cheti Feki?
  4. Mbona mwanzoni ulikuwa hutujali TBC na ulikuwa karibu sana na Clouds Tv na Radio?
  5. Je ile kamata kamata yako ya Dawa za Kulevya unaona imesaidia kumaliza kama siyo kupunguza tatizo au ndiyo umesaidia kuleta Ubunifu wa matumizi na uingizwaji wa dawa za Kulevya nchini?
  6. Je unadhani nafasi hii uliyonayo iliwahishwa Kwako au labda bado ulipashwa kubakia pale ulipokuwa ili uendelee kujifunza zaidi masuala ya Uongozi na Utawala?
  7. Kila mara unasikika ukipenda kulitaja mno jina la Mungu je Ndugu Paul Makonda unadhani matendo yako unayoyafanya kwa Wenzako au Wana Dar es Salaam au Watanzania yanamfurahisha Mungu na kwamba pengine unavyomtaja na Yeye huko alipo anafurahi?
Tanzania ya sasa inahitaji kuwa na Critical Journalists na siyo PR Journalists ambao kwa mtazamo wangu ndiyo wengi na wamejazana karibu katika kila Media Outlet hapa nchini. Na nyie Wakufunzi wa haya masuala ya Habari na Utangazaji hebu tafadhalini tupikieni Competent Journalists ili wasaidie kusukuma maendeleo ya nchi hii.
Hmm, ulitaka mwandishi hbr anune,sio? Je,wewe unaamini kuwa wauza sembe wamebadili mbinu ya kuingiza dawa hzo nchini? Je,tangu lini RC mkoa wowote Tz analazimika kutulia mkoani kwake?
 
Tabu ni nyie kupenda udaku, sasa cha ajabu nini hapo. Alienda kuongelea ya mji wake na pia sio mbaya wananchi wote nchini tukamjua.

Ilikuwa safi sana, ulitaka aongeleeeee nini!? au aulizwe nini tena...ha ha ha haaaaa tupo karne ya ishirini na....(malizia)

Ushamba umekujaaaaa

Kipindi lilikuwa kizuri wa Dar wamemuelewa na wananchi wengine.

Acha wivu, ni Mkuu wa Mkoa hata iweje n Mkuu wa Mkoa...sali usubiri zamu yako.

Makonda oyeeeeeeeeee
Naona ni mtu mmoja tu ndio ka like comment yako
 
Tabu ni nyie kupenda udaku, sasa cha ajabu nini hapo. Alienda kuongelea ya mji wake na pia sio mbaya wananchi wote nchini tukamjua.

Ilikuwa safi sana, ulitaka aongeleeeee nini!? au aulizwe nini tena...ha ha ha haaaaa tupo karne ya ishirini na....(malizia)

Ushamba umekujaaaaa

Kipindi lilikuwa kizuri wa Dar wamemuelewa na wananchi wengine.

Acha wivu, ni Mkuu wa Mkoa hata iweje n Mkuu wa Mkoa...sali usubiri zamu yako.

Makonda oyeeeeeeeeee
bila shaka ww mwenyewe unajishtukia ulichoandika ni pumba pumbafu. hizo kaz za kupewa unajinyea mwenyewe na huku unajicheka
 
Ukipimwa mkojo halafu majibu yakasoma negative, naenda kukivunja kifaa kilichotumika kukupimia. Na hiyo mimba ikikutwa si ya msukuma, I do the same kwa mashine ya DNA
Mkuuu nimekuelewa vizuri ulicho mjibu huyu demu mwenye asili ya kwa kagame.Anatetea kitumbua cha mumewe tu.Kuhusu mimba sidhani kama kwa laana anazoendelea nazo itanasa.Jamaa ataenda mazoezi mpaka misuli ipasuke lakini laaana yakukana ubini(ukoo) pamoja na kumkana mzee Bashite itamtafuna na mwisho wake utakuwa mbaya
 
Nadhani watangazaji wa Tbc wanafanana kwa tabia, kuna yule dada alimuuliza Sizonje swali wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari eti raisi anapendelea nini,kwa hyo hata sio ajabu kwa huyu wa leo na yy kuhoji maswali ya kijinga
 
Mkuuu nimekuelewa vizuri ulicho mjibu huyu demu mwenye asili ya kwa kagame.Anatetea kitumbua cha mumewe tu.Kuhusu mimba sidhani kama kwa laana anazoendelea nazo itanasa.Jamaa ataenda mazoezi mpaka misuli ipasuke lakini laaana yakukana ubini(ukoo) pamoja na kumkana mzee Bashite itamtafuna na mwisho wake utakuwa mbaya
Kumbe ni mkewe!
 
Mtangazaji ukisimamia taaluma yako unakua vizur na heshima utajijengea sio kujipendekeza huwa inakua kwa muda tu mwisjowe utalia na kuuaga meno
 
Kuna maswali hapo kama ya darasa la kwanza ambayo hayakuwa na umuhimu wowote. bado kuna tatizo kwenye hizi Tathinia ya habari
 
Tabu ni nyie kupenda udaku, sasa cha ajabu nini hapo. Alienda kuongelea ya mji wake na pia sio mbaya wananchi wote nchini tukamjua.

Ilikuwa safi sana, ulitaka aongeleeeee nini!? au aulizwe nini tena...ha ha ha haaaaa tupo karne ya ishirini na....(malizia)

Ushamba umekujaaaaa

Kipindi lilikuwa kizuri wa Dar wamemuelewa na wananchi wengine.

Acha wivu, ni Mkuu wa Mkoa hata iweje n Mkuu wa Mkoa...sali usubiri zamu yako.

Makonda oyeeeeeeeeee
Ahahaha!!!! Yaani hawapati usingizi kuhusu Makonda, wamesema na kumtusi matusi ya nguoni, Jamaa anapeta tuu!!! Nimeamini awamu ya Tano ni Mwiba mkali na Sumu mbaya kwa wadudu wote wa nchi Hiii.... Bila Makonda na JPM haiwezekani.. Te te te te te te te te te te
 
Mzee Albert Bashite yupo naye mumhoji. Je unaweza kutupa full history ya Paul Christian Makonda pamoja na wazazi wake wajitokeze na tumfahamu mzee Christian Makonda. Uwe mkweli usitumike

Ipo youtube.
 
Ukipimwa mkojo halafu majibu yakasoma negative, naenda kukivunja kifaa kilichotumika kukupimia. Na hiyo mimba ikikutwa si ya msukuma, I do the same kwa mashine ya DNA

Duh

Hii nayo kali... nink tena. Eeeeeeeeeh

RC ni family man, ana mke anampenda sana sana.

Acha wivu, fanya kazi
 
Back
Top Bottom