Mtangazaji ITV uliyehabarisha wizi wa box la kura Magomeni uwe makini, unatafutwa na "kuwindwa" kwa muda mrefu

Kwanza wadhibitishe ...sanduku liliibiwa au laa.....wapunguze ubabe na kufundisha watu kasema uongo... Wengine hawajazoea.
 
Sawa, bbc tutamchukua na kumpa mchongo wa maana...
Huyu dogo tunajua alikuwa anatafutwa hasa kwa jinsi alivyokuwa akiripoti kampeni za cdm na Lowassa 2015
 
Spencer Lameck kuwa makini kuanzia sasa na nyendo zako,kuna watu "wanakuwinda".Sina namna ya kukupata ili nikupe ujumbe huu,lakini napitia JF kukupa "tetesi" kuwa uwe makini,kuna watu "wanakuwinda".

Hawajaanza jana kukuona kama ni "kauzibe" kwao,walianza kuona hauko upande wao toka wakati wa uchaguzi mkuu,team ya kampeni ya "chama dume" kitengo cha Habari na Mawasiliano kilichokuwa kionaongozwa na Mkuu wa Wilaya wa sasa wa Longido,katika majumuisho yao ya kila siku juu ya mwenendo wa kampeni,iliona mtangazaji wa ITV aliyeambatana na Mzee wa Monduli ndio "kikwazo" kwao.

Namna ulivyouhabarisha umma,kwa "mbwembwe" na "bashasha" juu ya kuchanja mbuga katika milima na mabonde kwa mgombea wa chama kingine,ilikuwa kikwazo kwa upande wa pili.

Iliundwa team maalumu kuhakikisha kuwa katika vyombo vya habari vinavyotazamwa sana kama ITV(kwa wakati ule wa 2015),habari za mgombea wao zipate zishereheshwe sana wakati wa taarifa ya habari.

Kwa upande wa "chama dume" mwandishi wa ITV alikuwa Emmanuel Buhohela na upande wa pili alikuwa Spencer Lameck.Huyu Buhohela "alikamatwa" vizuri sana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa CCM wa wakati huo ambaye kwa sasa ni mkuu wa Wilaya ya Longido Mh.Daniel Chongolo.Baada ya uchaguzi,Emanuel Buhohela akapata kazi Ikulu,na sasa yupo kwenye kitengo cha Kurugenzi ya Habari Ikulu iliyo chini ya Msigwa na Jaffari Hanyuu(?) ambaye wakati wa uchaguzi alikuwa anaripoti toka TBC One.

Ahadi kubwa kwa Buhohela ilikuwa ni kuhakikisha anampamba na kumremba vizuri mgombea wao,na baada ya uchaguzi "atafikiriwa",na kweli alifikiriwa.Huyu Spencer Lameck hakutoa ushirikiano kila alipojaribiwa "kuhujumu" taarifa za upande aliokuwepo.Huyu Spencer ndio aliibuka na msamiati wa "mafuriko"...Kila ikifika saa mbili,alitupasha juu ya "mafuriko" ya EL.Mafuriko yalehumtesa mtu fulani mpaka kesho.

Huyu Lameck aliwaudhi watu kwa muda mrefu,walikuwa wanakosa sababu ya haraka(immediate Cause),ila sasa wameipata.

Mkutano wa kwanza wa waandishi wa habari na Raia namba moja,Spencer Lameck alipata nafasi ya kumuuliza Mheshimiwa swali,na swali lake lilikuwa kwamba,ni vigezo vipi Rais ametumia kuchagua mawaziri katika baraza lake la mawaziri??Mheshimiwa akamjibu kuwa; "Vigezo nilivyotumia ndio vilevile ambavyo boss wako na chombo chako cha habari kimekuteua wewe kuja Ikulu kuchukua hii habari"...lakini "off Camera",jamaa akaongezewa jibu kuwa unaniuliza vigezo??ni vilevile vilivyofanya wewe uchaguliwa ku-report habari za UKAWA.

Habari ya ITV siku ya uchaguzi Kinondoni ya kuonyesha jinsi mtu alivyokimbia na kasha la kura kituo cha Idrissa-Magomeni,limewakasirisha sana watu,limewaudhi na wamedhamiria kumuadabisha mtu,hawakuta ukweli ule ujulikane.Wanataka kumshikisha mtu adabu...Bwana mdogo usidharau,kuwa makini na nyendo zako,jilinde,kuwa na tahadhari.Tumeamua kuandika hapa,ili waone aibu kufanya kile walichopanga kufanya.

ITV wameomba radhi kwa mtangazaji wao Spencer Lameck kutangaza habari ya makasha ya kura kuibiwa pale Magomeni.Si kwamba ni habari ya uwongo,ila wanasema ni habari iliyoleta "usumbufu" kwa watu wengine.

Mwanangu na kijana wangu Spencer Lameck,tangu sasa...Chunga mienendo na maeneo unayotembelea.Tupo katika kipindi cha kupeana tahadhari kwa kila tunalolitenda.Ubarikiwe.

Hao washenzi siku zao zinahesabika, ,Nchi sio yao peke yao
 
Wasiojulikana wanamtamani lameck Mungu mlinde lakini kazi bure kutokana na lile tukio chochote kikimpata tutajua ni wao, dawa ya Mchawi mkabidhi mwanao.
 
Hilo la box la kura eti kuibiwa ni uzushi mkubwa mno....Chadema hiki hakikukosi kutunga uongo kila siku...box liibiwe ili iwe nini??? Tanzania hii hatujafikia hukokuiba box la kura....
Hujitambui wewe
 
Back
Top Bottom