Mtandao wa WikiLeaks wamlipua Mattaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtandao wa WikiLeaks wamlipua Mattaka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,382
  Likes Received: 414,707
  Trophy Points: 280
  Mtandao wa WikiLeaks wamlipua Mattaka Tuesday, 04 January 2011 10:40

  [​IMG]Mr David Mattaka

  Mwandishi Wetu
  Mtandao wa habari za kiuchunguzi wa WikiLeaks, umeendelea kuanika siri za ufisadi nchini na mara hii umemlipua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka.Taarifa hizo kupitia WikiLeaks zimekuja karibu wiki mbili tangu kutolewa hadharani kwa taarifa nyingine zinazohusu Mkururugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, akidaiwa kufichua siri za Rais Jakaya Kikwete kwamba kiongozi huyo wa nchi asingependa vigogo serikalini kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

  Lakini juzi taarifa zilizoripotiwa na mtandao huo na kunukuliwa na gazeti la New York Times zimedai kuwa Mattaka anatumia mpango wa serikali wa kulifufua upya shirika hilo kwa kununua ndege mpya, kujinufaisha.

  Habari zimeeleza kuwa katika kufanikisha hilo, Mattaka anadaiwa kutaka kumtumia mfanyabiashara wa Kiasia ambaye anajihusisha na biashara za hoteli kuwa wakala wa ununuzi wa ndege hizo baina ya ATCL na Kampuni ya Boeing ya nchini Marekani.

  Tuhuma hizo dhidi ya Mattaka ziko kwenye taarifa za siri za mawasiliano za ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, zilizoripotiwa na mwanadiplomasia wa Marekani, Dk Purnell Delly.

  Delly pia ndiye aliyetajwa katika taarifa za awali na mtandao wa WikiLeaks kwamba alifanya mazungumzo na Dk Hosseah.

  Jana Mattaka alikiri shirika hilo kukubali kununua ndege za kampuni ya AirBus ya nchini Ufaransa, lakini akapuuza madai ya kutumia wakala kwa nia ya kujinufaisha.

  "Huu ni upuuzi. Sikumbuki kufanya jambo hilo na tuhuma hizo hazina mashiko," alisema Mattaka alipokuwa akizungumza na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen.

  Taarifa hiyo inamnukuu Delly akituma taarifa nchini kwake inayoilalamikia Tanzania kwamba ilikuwa na mbinu chafu ziliokuwa zikipangwa kuhakikisha kwamba ATCL inanunua ndege kutoka Kampuni ya Airbus ya Ulaya badala ya Boeing ya Marekani, hasa baada ya uongozi wa Boeing kukataa kutumika kwa mawakala.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Kampuni ya Boeing iliwasilisha mapendekezo yake kwa ATCL sambamba na yale yaliyowasilishwa na kampuni ya Airbus, lakini wanalalamika kwamba kulikuwa na mpango wa makusudi wa upendeleo ambao unaashiria kwamba kulikuwa na “harufu ya rushwa”.

  Taarifa hiyo imedai kuwa ushauri wa Mattaka kumtaka Rob Faye, ambaye ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Kanda ya Afrika wa Boeing kuwasiliana na mfanyabiashara na tajiri wa Kiasia ili aweze kumsaidia kufungua milango ya biashara hiyo kwa serikali ya Tanzania “haukuwa wa kawaida”.

  “Faye aliukataa ushauri huo kwa malezo kwamba kampuni ya Boeing haitumii mawakala katika biashara zake, siyo tu Tanzania, bali katika nchi yoyote duniani,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:

  “Mawakala na malipo ya kamisheni ni kiini cha vitendo kadhaa vya rushwa ikiwemo ile ya rada ambayo Serikali ya Tanzania ililipwa asilimia 31 ya gharama kama kamisheni”.

  Kwa mujibu wa taarifa za mawasiliano baina ya uongiozi wa Boeing, ATCL na Ikulu, Rais Jakaya Kikwete “hakufurahishwa” na taarifa kwamba baadhi ya maafisa wa ATCL walitaka kujinufaisha wenyewe na mpango huo wa ununuzi wa ndege.


  Agosti 9, 2007, Faye alikutana na aliyekuwa Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk Maua Daftari na Mkurugenzi wa Usafirishaji na Mawasiliano, Dk Bartholomew Rufunjo,ambao walimpa matumaini kwamba kusingekuwa na upendeleo katika mchakato wa ununuzi wa ndege hizo.

  Baadaye Agosti 10, Mattaka, alimhakikishia Faye kwamba ATCL haikutumia mawakala katika ununuzi wa ndege zake, kauli ambayo Mattaka aliirudia mara kadhaa wakati wa kikao baina ya Bodi ya Wakurugenzi wa ATCL na Faye.

  Faye alinukuliwa akisema kuwa huenda kumekuwa na mwasiliano baina ya Ikulu na Wizara ya Miundombinu ili kuhakikisha kwamba hakuna “mtu wa kati” katika mchakato huo.

  Hata hivyo, Mattaka anadaiwa kumwambia Faye kwamba kulikuwa na shinikizo kutoka ubalozi wa Marekani nchini ili Boeing wapewe nafasi ya kuuza ndege zake ATCL.

  Wasiwasi kwamba hakukuwa na uwazi katika mchakato huo unatokana na tangazo la aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge la Septemba 2, 2007 lililonukuliwa na vyombo vya habari kwamba Tanzania iko katika mpango wa kununua ndege mpya kutoka kampuni ya Airbus.

  Kauli hiyo ya Chenge ilitolewa saa 48 tangu aliyekuwa balozi wa Marekani nchini, Michael Retzer kuondoka kurejea nchini kwake baada ya muda wake wa kukaa nchini kumalizika.

  Hata hivyo, Chenge anadaiwa kukana kauli yake kwa kusema kwamba alinukuliwa visivyo na vyombo vya habari Septemb 7, 2007 katika kikao chake na Pully pamoja na ofisa wa uchumi katika ubalozi wa Marekani.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Moto ni uleule.
  Mambo hadharani, asante wikileaks, tena iwapo wataweza watume watu wao kwenye kila kona ya nchi.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  We await for more floods if not leaks! Watakoma safari hii! Hivi waziri wa habari ameshindwa kuwafungia hawa wikileak! teh
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,382
  Likes Received: 414,707
  Trophy Points: 280
  W'Leaks: ATCL boss pushed for bribes Monday, 03 January 2011 22:13

  [​IMG]By Tom Mosoba, Weekend News Editor
  Air Tanzania managing director, Mr David Mattaka, allegedly proposed the use of an "agent" to push for a multi-billion shillings fleet modernisation deal with American plane maker – Boeing.

  The claim, in a confidential diplomatic communication from the US embassy in Dar es Salaam, says the ATCL boss implied that the middleman would help to push for the deal that the embassy officials pegged at some $537 million (Sh750 billion) in sales.

  According to the information, Mr Mattaka even dropped the name of "a wealthy South Asian hotelier" as the preferred agent to "open doors" in the deal to purchase 10 planes in a government backed plan to revive the national airline that was then tittering on the brink of collapse.

  However, Mr Mattaka yesterday vehemently dismissed the reports and said he did not at any time do what is being claimed in the memos.

  He told The Citizen in a telephone interview that he did not hold talks with any US officials over the said agent. "That is crap…I don't think I have made such suggestion to anyone and in any case, it doesn't make sense to me," he said. Told of the published dossier leaked from the Embassy, an apparently agitated Mattaka remarked: "I don't know where they got the information."

  The confidential information was filed by the then Deputy Chief of Mission (DCM), Mr Purnell Delly, and was published at the weekend through WikiLeaks, a web based organisation that has released in the Internet over 250,000 secret diplomatic files from US missions around the world.

  WikiLeaks, founded by an Australian national Julian Assange, at the end of last year released another secret file form Dar es Salaam that quoted the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) Dr Edward Hoseah as saying President Kikwete was not willing to prosecute top former and current leaders implicated in corruption. Dr Hoseah has since denied the allegations.

  Succinct details by Mr Delly shows how the former US Ambassadors Mr Michael Retzer, and before him, Mr Mark Green, tried to prevail upon relevant government authorities to facilitates level the playing field for competition between Boeing and another Europe-based plane manufacturer, Airbus, that was also bidding for the same deal.

  The official said other than the push for an agent, the US was also worried that China may have been angling for the ATCL deal by tying its development aid to Dar es Salaam on a settlement of a deal that would be in favour of Airbus. China has a trade agreement with Airbus to assemble some of its parts.

  The suggestion to use an agent was allegedly made in June by Mr Mattaka who put it across to Mr Rob Faye, Regional Director of Sales for Boeing Commercial Airplanes. Mr Faye is quoted as telling the Embassy that "the company's fear of outside influence or corruption might be legitimate."

  "The DCM specifically noted Air Tanzania Managing Director and CEO, David Mattaka's unusual ‘suggestion' that Faye should contact a wealthy South Asian hotelier, who subsequently suggested to Faye that he would need his services to open the right doors in government. Faye flatly refused, responding that Boeing does not use ‘agents' in Tanzania or elsewhere," read the confidential memo.

  Mr Delly makes a footnote of the problem that Tanzania, faced with the use of an agent in the purchase of the $40 million military radar from BAE Systems of UK and reveals how US officials raised the ATCL matter with a close aide to President Kikwete.
  "The presidential advisor later got back to the DCM, telling him that President Kikwete was "incensed" upon learning that senior Air Tanzania officials might be intending to profit personally from the deal," reported Mr Delly.

  The file goes on to recount several meetings with the then minister for Infrastructure Development Mr Andrew Chenge, his deputy Maua Daftari and some senior ATCL officials, who all are said to have noted the importance of a fair and level acquisition process for Air Tanzania's development.
  The US was concerned that any hushed deal could deal a blow to Tanzania's stated commitment to end corruption in government.
  Meanwhile Mr Mattaka yesterday told The Citizen that ATCL finally settled for Airbus to supply the planes. He did not elaborate on the financial details or any other information of the Airbus agreement.

  ATCL has struggled to remain afloat since 2006 when its short-lived marriage to South African Airways (SAA) collapsed.
  The airline largely relied on government subsidy to operate but has seen its Boeing fleet drop to just a single plane as its searches for a business partner.
   
 5. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kwa taarifa yako, wikileaks wanakusanya habari kama anavyokusanya michuzi. kama na wewe una habari basi unaweza watumia kwa kupitia hapa

   
Loading...