Mtandao wa Tigo umepatwa na nini?

Mtandao wa Tigo umepatwa na nini?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,347
Reaction score
26,153
Kwa siku tatu sasa, mtandao wa Tigo unakumbwa na changamoto katika jumbe fupi za maandishi na hata kupiga simu kutoka na kwenda kwenye simu yenye mtandao huo. Jumbe hazifiki kwa muda au hazifiki kabisa na hivyo kukwamisha mawasiliano.

Kulikoni?
 
TTCL kwenye matumizi ya bando nimewanyooshea mikono. MB 600 tu nimetumia mpaka nimechoka wakati tigo,Airtel na Voda GB 1 inakwisha kwa kusoma SMS WhatsApp tu.

TCR wawachunguze hawa wengine, kwakweli Nyumbani kumenoga na nimesharudi mazima.
mitandao yote ya njee ni wezi...kuanzia tgo, voda, airtel, halotel and the likes... hamia TTCL mkuu nyumbani kumeshanoga.
 
TTCL kwenye matumizi ya bando nimewanyooshea mikono. MB 600 tu nimetumia mpaka nimechoka wakati tigo,Airtel na Voda GB 1 inakwisha kwa kusoma SMS WhatsApp tu.
TCR wawachunguze hawa wengine, kwakweli Nyumbani kumenoga na nimesharudi mazima.
TTCL kupata vocha zao hadi upande gari uende ukazitafute mjini, naskia ukitumia laini zao kuna baada ya vitu huwezi kuvifanya mitandaoni.. Kama kudownload vitabu na video
 
Jamani vp kuhusu hizi meseji za nitumie kwenye no hii jina litatokea kidubwashika chandombwa hivi hawa wezi wanapata wapi no hizi wajuzi embu nielewesheni
 
mie ilinigomea kuingia apps zote za google nikaona huu upumbavu. Simu inaingia whatsapp tu na facebook.
TTCL kupata vocha zao hadi upande gari uende ukazitafute mjini, naskia ukitumia laini zao kuna baada ya vitu huwezi kuvifanya mitandaoni.. Kama kudownload vitabu na video
 
Back
Top Bottom