Mtandao wa NBC sport wamtaja Samatta kama ni raia wa Tunisia

olele

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
1,305
1,569
Huu ni mtandao unaomilikiwa na NBC TV network na ni unaoheshimika duniani kwa habari zao za uhakika,
lakini nimeshindwa kuyaamini macho yangu wakati nasoma habari zao kuhusu African player of the year, walipomtaja SAMMATA kuwa ni raia wa TUNISIA

" Pierre Emerick-Aubameyang of Borussia Dortmund and Gabon was named the African Player of the Year, while the African-based honor of the same name went to 24-year-old Tunisian striker Mbwana Aly Samatta of TP Mazembe."

Je ni uzembe wa waandishi wao (siamini kama wanaweza kuwa wazemmbe kiasi hiki) Je ni makusudi?? au ni kwa sababu Nchi yetu sio maarufu

Aubameyang, Samatta named African Players of the Year; Arsenal to bid big for the former?
 
Kuna wakati miaka ya nyuma barua na vifurushi vingi vya kwenda Gambia vilikuwa viinapelekwa Zambia.
 
Kuna wakati miaka ya nyuma barua na vifurushi vingi vya kwenda Gambia vilikuwa viinapelekwa Zambia.

Lakini Tanzania na Tunisia ni vitu viwili tofauti mkuu
 
Lakini Tanzania na Tunisia ni vitu viwili tofauti mkuu
Tatizo letu ni kutokuwa na ubunifu katika kujitangaza kimataifa. Kwa hao NBC Tanzania ni kama Tunisia. Ni sawa wamechemsha lakini ndio hivyo. Ingekuwa ni nchi nyingine (kwa mfano Kenya) tayari makelele yangekuwa yameshaanza kwenye mitandao ya kijamii hadi NBC kulazimika kufanya masahihisho au kuwa makini na Tanzania hapo mbeleni. Angalizo: Nimetaja Kenya kama mfano lakini hawa nyan'gau huwa siwafagilii kabisa.
 
hicho ndo nachojaribu kufikiria, tuko nyuma sana labda pia hawaamini kama kuna mtanzania anaweza kuwa mchezaji
bora wa Afirica (wa ndani)

pia umesema vizuri kuwa ingekua nchi nyingine wangeshapiga kelele mpaka jamaa wangeomba radhi na kurekebisha,
lakini sisi hata kujua tu kuwa kuna makosa itakua ni ishu.. au tutaona na kupuuzia tu
 
Mi nadhani walijichanganya wenyewe wakati MC anatangaza majina wao Tanzanian waliisikia kama Tunisian na hii yote ni kwa sababu jina la nchi yetu bado halijakaa masikion mwa watu wengi wa nje kwenye issues za michezo
 
Post moja inatosha. Tatu za nini?
 
Wala Hakuna Cha Ajabu Hapo, Kwasababu Hata Mlima Kilimanjaro Kuna Baadi Ya Nchi Zinajua Kama Upo Kenya.
 
Hawataki Tanzania ijulikane kuwa ina vipaji.Watu mnalaumu si tukatae tu mitandaoni?au hili li english linasumbua.
 
...ninachowashangaa mmekaa kujibizana na comments hapa...tetea nchi yako nenda NBC jisajili then watupie comments pale so far ziko 5 tu. Acheni kulalamika POWER 2 U, mtaweza kweli mabadiliko nyie??? By the way registration kule ni bure!!!
 
Mwisho wa siku wao ndio wataonekana Wana waandishi vilaza. !
 
Na mimi nilishinikiza
 
Attachments

  • 1452264196933.jpg
    1452264196933.jpg
    52 KB · Views: 29
Back
Top Bottom