Mtandao wa majambazi kutoka Bara wakamatwa Zanzibar. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtandao wa majambazi kutoka Bara wakamatwa Zanzibar.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, Mar 18, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Written by administrator // 18/03/2011 // Kitaifa // 3 Comments

  Salama Said,
  JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja linawashikilia watu 10, wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao walikuwa kwenye maandalizi ya kutaka kupora katika hoteli ya kitalii ya My Blue, iliyoko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini, Henry Mwibambe, alisema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia jana, huko Nungwi ambapo hivi sasa matukio kama hayo yaliaza kupungua lakini sasa ameanza kujitokeza kwa kasi hasa huko Tanzania Bara.
  Kamanda huyo aliwataja watuhumiwa wa ujambazi hao ni Andrew Henry Yussuf (24) mkazi wa Kigamboni Dar es Salaam, Abdullah Khatib Makota (33), mkazi wa Kiembesamaki, Khamis Msoma Masanja (31), mkazi wa Welezo, Faki Makame Faki (40) mkazi wa Kariakoo, Dar es Salaam.
  Wengine ni Salum Seif Roto (30), mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Lelo Michael Ringo (31),mkazi wa Tabata, Dar es Saalam, Said Juma Rashid (35) mkazi wa Magomeni Unguja, Msafiri Ali Mengi (25), mkazi wa Jang’ombe, Jeremia Joseph Michael (31), mkazi wa Dodoma na Khamis Kombo Juma (34) mkazi wa Tomondo Unguja.
  Aidha Kaimu huyo alisema mmoja kati ya watuhumiwa hao alikamatwa akiwa amevaa sare za kamili za jeshi la polisi ambaye alikuwa katika kundi hilo la watuhumiwa hao.
  Alisema mara baada ya majambazi hao kuingia katika hoteli hiyo walijaribu kuwapambana na walinzi wa hoteli hiyo kabla ya kikosi maalum cha kupambana na uhalifu kufika katika eneo hilo na kuanza kuchukua hatua za kupambana nao.
  Kaimu kamanda huyo alisema hata hivyo katika kupambana na walinzi wa hoteli hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa hata mmoja, isipokuwa majambazi hao walitumia mapanga na kuwapiga mabapa walinzi hao kwa lengo la kuwatisha na kutaka watulie ili watimize azma yao hiyo ya uporaji.
  Kaimu huyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Mkoa huo, alisema Polisi walifanikiwa kuwakamata majambazi hao baada ya kupokea habari za uvamizi hu kutoka kwa wasamaria wema na dhana ya polisi jamii kufanya kazi.
  Alisema baada ya polisi kuingia kwenye eneo la hoteli hiyo majambazi hao walijaribu kutoroka kwa kutumia gari yenye namba za uzajili Z 490 AV, Super Custom akuondesha kwa kasi.
  Henry, alisema kukimbia kwao kwa kasi majambazi hao haikufanikiwa kwani waliwekewa kizuizi cha barabarani katika kituo cha polisi Nungwi ambapo kikosi cha kutuliza ghasia cha Mkoa huo kwa kushirikiana na polisi wa kituo hicho walifanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka chini ya ulinzi mkali majambazi hao.
  Alisema watuhumiwa hao wa ujambazi wamekamatwa wakiwa na silaha za jadi kama vile mpanga, ndondo, pamoja na koleo ya kuvunjia milango kwa lengo la kutaka kufanyia uhalifu wao.
  Henry alisema watuhumiwa hao inasadikiwa kuwa ndio walioshiriki kuvamia hoteli ya kitalii ya Waridi iliyoko Pwani Mchangani Machi 17 mwaka huu majira ya usiku wa manane na kufanikiwa kuiba vitu kadhaa baada ya kuwafunga kamba walinzi wa hoteli hiyo na kutimiza azma yao.
  Alisema kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika, huku Kaimu huyo akiwataka wananchi kushirikiana na Jeshi lake ili liweze kuvunja mtandao wa majambazi ambao umeanza kurudi upya hapa Zanzibar.

  3 Comments on "Majambazi wakamatwa visiwani Zanzibar"
  1. [​IMG]
   utomvu 18/03/2011 kwa 7:15 um · Jibu
   Hio ndo faida ya muungano tukisima muungano hauna faida kwa znz tunaonekana aaa tunataka kuvunja udugu, udugu udugu gani huo nakuvamiwa namijitu isiojua hata dini, vunja muungano weka pasport khalass.


  2. [​IMG]
   asumani 18/03/2011 kwa 7:35 um · Jibu
   Nani wa kulaumiwa?


  3. [​IMG]
   makame silima 18/03/2011 kwa 8:45 um · Jibu
   Haya yote yalikuwa hakuna Zanzibar, lakini tulipo ungana na wadudu hawa ndipo walipotuambukiza maradhi haya ya Ujambazi,Uhasharati wakujiuza mili na utapeli ambao udanganyifu huu umo hata ktk Muungano. Waungana na Juma Kecho unambiwa Umeungana na Yussf.
   Na kuhusu Ujambazi mimi nazani hata huyu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini, Henry Mwibambe ni mmoja ktk hawa Majambazi,Zanzibar na Andrew wapi na wapi kama hili si jambazi la Tanganyika?.na nazani huyu Andrew Henry Yussuf nindugu yake wadamu.
   Vunja Muungano turudishe hazi na mila zetu Wzanzibar tukisherewa watatupoteza hawa kitu utamaduni na ustarabu mwiko kwao.
   Vitu tungane na watu matapeli wasio tekeleza makubaliano.

   
 2. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,135
  Likes Received: 2,158
  Trophy Points: 280

  1. [​IMG]
   utomvu 18/03/2011 kwa 7:15 um · Jibu
   Hio ndo faida ya muungano tukisima muungano hauna faida kwa znz tunaonekana aaa tunataka kuvunja udugu, udugu udugu gani huo nakuvamiwa namijitu isioju a hata dini, vunja muungano weka pasport khalass.


   Hapo kwenye Nyekundu Umekosea Wewe Ndio hujui kwani waliokamatwa hawamo wa Dini yako. ulivyokuwa **** hayo majina ni ya Mitume wa Mungu Andrew Yusuph Umekaa kama Kasa Unatoa Povu. Dini inakusaidia nini? ubague au ulaani wengine uwaite majitu? tatizo lenu mna akili za kufundishwa! unaongea mapovu povu tu. Dini Umezikuta hata dini yako ilizikuta na zitaendelea kuwepo hadi utakapo kufa zitaendelea kuwepo hujui maana hata ya dini? imani ya mtu ndio huitwa dini au unaumwa Nenda kwa Babu Loliondo, anatibu na akili pia. Muungano Babu yenu karume na Baba wenu wa Taifa Ndio waliunganisha na hiyo pia umekuta labda hao ndio majitu sie pia tumeukuta twashangaa kwani visiwani ndio wanafaidika bara sijasikia wanachopata huko. iweje uanze kutoa povu
   
 3. K

  Kikambala Senior Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Heading haijakaa vizuri,kwanza hao ni vibaka wa hukohuko unguja,sisi huku jambazi anakuja na smg au bomu maana watu atakao pambana nao wako kamili sio nyie wote mashoga mkipigwa kwenzi tu hoi.mjaribu kuwa na staha mnapoongelea huo muungano ambao unawanufaisha zaidi nyie,siku tukuchukia nakuvunja muungano ndipo mtakapo jua kwamba mlikuwa mna faidi zaidi nyie.
   
 4. aye

  aye JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,987
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  hao wa huko huko wa bara hawavamii na marungu na mapanga tena na sio mchana kweupeeeee
   
 5. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,143
  Likes Received: 871
  Trophy Points: 280
  Kamanda huyo aliwataja watuhumiwa wa ujambazi hao ni Andrew Henry Yussuf (24) mkazi wa Kigamboni Dar es Salaam, Abdullah Khatib Makota (33), mkazi wa Kiembesamaki, Khamis Msoma Masanja (31), mkazi wa Welezo, Faki Makame Faki (40) mkazi wa Kariakoo, Dar es Salaam.
  Wengine ni Salum Seif Roto (30), mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Lelo Michael Ringo (31),mkazi wa Tabata, Dar es Saalam, Said Juma Rashid (35) mkazi wa Magomeni Unguja, Msafiri Ali Mengi (25), mkazi wa Jang'ombe, Jeremia Joseph Michael (31), mkazi wa Dodoma na Khamis Kombo Juma (34) mkazi wa Tomondo Unguja.

  Red: Hao wote yawenyeji wa huko Zenji
  Blue: Wageni ambao walikuwa wakiongozwa na wenyeji wao wa huko.

  My Take:
  Una mtazamo wa kidini
  Wabara tungekuwa na tabia hiyo msingeishi hata kwenye kiti,oto tungewatimua lakini we always share those Good thing pamoja!!!
   
 6. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Heri nguo ziraruke kuliko akili, taabu huisha lakini upumbavu hudumu. Nyie mujahidina mkiongozwa na haka kapumbav abd. mmekuwa mki2tukana sana watanganyika lkn tuko kimya, hao mjahdina wenzenu wanapofanya uhalif huko mnatafta jina la tanganyika na kuendeleza upumbav wenu wa matusi, hv ungekuwa mtandao wa kihalif kutoka bara hako kamkoa kakipigwa bom 1 km lililopigwa bank TMK si mtakufa nyie midebwedo. Hamna akili pimbi nyie, na sis tunaanza 2mia lugha km zenu achen twende jela ya JF. Mullet!
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwahiyo uataka kusema Watanganyika wote ni wakristo sio!.
   
Loading...