Mtaji wa milioni moja, naomba wazo la biashara

Habari zenu jamani.

Kwanza nikiri kwamba naandika post hii huku kichwa kinaniuma. Toka nimepata hii pesa (600k nimeuza mali, 400k nimekopa) nimeumiza sana kichwa biashara gani ntafanya ili niendeshe maisha?

Kiukweli sitafuti faida ya haraka haraka, nataka tu nipate chochote ili nilipe kodi na kum-support mzazi mwenzangu maana nimesota sana baada ya kupoteza kazi.

Niliwaza biashara hizi (zifuatazo) lakini nikaacha hayo mawazo kwa sababu zifuatazo.
Saloon - flemu, vifaa, furniture. Nikaona pesa haitoshi.
Mobile money - flemu, leseni, float. Pesa haitoshi.
Mgahawa - flemu, (viti na meza), vyombo. Na nikizangatia hakuna biashara inayolipa ndani ya siku chache za mwanzo nikaona pesa haitoshi. Nitakula msingi.

Biashara ambayo naiwaza sasa hivi ni kunnua simu, hata nikianza na tatu kisha niziuze tu mtaani. Kama kuna mtu ashawai fanya hivi naomba mawazo yenu. Na risk zake ni zipi ?

Lakini kama idea yangu si nzuri, naombeni mnishauri idea nzuri maana kichwa kinauma sana.
Hello ndugu.

Huhitaji mtaji (au mtaji mkubwa) kuanzisha biashara.

Bali unahitaji taaluma ya kusoma matatizo ya soko pamoja na namna ya kutatua matatizo hayo.

Baada ya hapo unatakiwa kuweza ku test soko lako bila ya kupoteza pesa nyingi.

Kama soko linalipa, unajikita katika hilo soko na kujenga biashara. Kama hali lipi unaenda kwenye soko jengine.

Unaweza kuangalia video hii kujifunza zaidi:
View: https://youtu.be/oN9ZQWzAoxk?si=e8zdoasxhitqg6fU

Vile vile tunayo kozi ya bure mtandaoni tunafundiaha yote hayo.

Kama utapenda kujisajili unaweza kwenda hapa Wazo Fasta
 
Wabongo kwenye biashara sisi bado sana. Nimesoma asilimia 90 ya mawazo ya kibiashara hapa wanashauri biashara ya mali kuoza hiyo ni biashara ngumu sana kwa mtu anaeanza.
 
Habari zenu jamani.

Kwanza nikiri kwamba naandika post hii huku kichwa kinaniuma. Toka nimepata hii pesa (600k nimeuza mali, 400k nimekopa) nimeumiza sana kichwa biashara gani ntafanya ili niendeshe maisha?

Kiukweli sitafuti faida ya haraka haraka, nataka tu nipate chochote ili nilipe kodi na kum-support mzazi mwenzangu maana nimesota sana baada ya kupoteza kazi.

Niliwaza biashara hizi (zifuatazo) lakini nikaacha hayo mawazo kwa sababu zifuatazo.
Saloon - flemu, vifaa, furniture. Nikaona pesa haitoshi.
Mobile money - flemu, leseni, float. Pesa haitoshi.
Mgahawa - flemu, (viti na meza), vyombo. Na nikizangatia hakuna biashara inayolipa ndani ya siku chache za mwanzo nikaona pesa haitoshi. Nitakula msingi.

Biashara ambayo naiwaza sasa hivi ni kunnua simu, hata nikianza na tatu kisha niziuze tu mtaani. Kama kuna mtu ashawai fanya hivi naomba mawazo yenu. Na risk zake ni zipi ?

Lakini kama idea yangu si nzuri, naombeni mnishauri idea nzuri maana kichwa kinauma sana.

Kuna mawili tu hapo

1. Soma ka course ka computer security, SAP au Oracle halafu utafute kazi popote mitandaoni
2. Tafuta laini ya kwenda kujiongeza majuu tumia hiyo kama ticket

Maana una pesa ya mboga tu
 
Nunua baro moja la vitenge, java, linauzwa laki 5 hadi 7.5 kutegemea na msimu. Ingia minadani na magulioni huku Handeni, pitia Gairo hadi Manyoni huko.

Baada ya mwaka utakuja kunishukuru kama ni mwenye kushukuru.
 
Vitenge unapata pair ngapi na minadan wanauzaje!
 
Kuna mawili tu hapo

1. Soma ka course ka computer security, SAP au Oracle halafu utafute kazi popote mitandaoni
2. Tafuta laini ya kwenda kujiongeza majuu tumia hiyo kama ticket

Maana una pesa ya mboga tu
Hizi kazi za oracle, cybersecurity, SAp anatafuta kazi za kifanya online, kampuni za nje au ndani, ???
 
Nunua baro moja la vitenge, java, linauzwa laki 5 hadi 7.5 kutegemea na msimu. Ingia minadani na magulioni huku Handeni, pitia Gairo hadi Manyoni huko.

Baada ya mwaka utakuja kunishukuru kama ni mwenye kushukuru.
Uko handeni mkuu?
 
Kwa simu itakuuwa na mawazo tena kama upo Dar. Then kwa biashara ya simu sijui utauza bei kwani upate faida wakati mtu akishakuona na simu mkononi anajuwa used bei inashuka.

Nakupa wazo mkuu, fungua biashara ya vipodozi uswahilini, chukua frame lipa miezi 4 lakini 2 chukua laki 4 ingia kariakoo chukuwa zaga kama zote njoo weka.

Kama utakuta frame ina shelf itakuwa poa sana ila kama hamna tumia laki mbili ya matengenezo then laki moja fanya nauli na chai ukisikilizia mchongo mwaisa.

Pia ukikaa vizuri m1 kwa vipodozi ni mtaji mkubwa sana aisee. Achana na mambo ya leseni ,TRA sijui nini fanya kigumu usifate protocol sana.

Hii biashara ina faida sana hela ya mtaji kwa kipodozi unaweza ukaingiza faida kama ulowekeza.

Ngoja niishie hapa
Na tulioko mkoani?
 
Kama unaroho ngumu Kuna machimbo yanayouza pikipiki used kwa bei nzuri nunuwa ya 800000 kisha upige bolt au kawaida ,pesa iliyobakia utanzia maisha kwenye kazi yako mpya ,hapa jitihada zako na umakini ndio utakao kupatia faida
 
Back
Top Bottom