Kwa muda mrefu CCM imekuwa ikitumia 'ujinga' kama tatizo la kimkakati la kuendelea kubaki madarakani. Ni ukweli usiopingika kuwa sababu ya ujinga unaotokana na umasikini kukithiri katika sehemu kubwa ya jamii, hata wakati wa kampeni za uchaguzi CCM imekuwa ikifanya jitihada za makusudi kutengeneza ajenda na propaganda ambazo ni wajinga tu wanaoweza kumeza. CCM imekuwa ikinufaika sana na hali ya ujinga na umasikini uliokithiri katika jamii. CCM imekuwa ikikwepa kwa juhudi zote kampeni kuongozwa na hoja (issues based), ndio maana inakataa mijadala katika kushindanisha wagombea.
Sasa CCM imekuja na mpango wa kusafirisha gas kutoka mtwara kwenda DSM, wapinzani wamewalisha wananchi propaganda za aina ileile kama ambazo CCM huwa wanazitumia. Ukisikiliza hoja zinazotolewa na wananchi huko mtwara ndio utajuwa kweli kazi ipo. Mtu anasema kwanini hawakusafirisha maji kutoka kidatu hadi DSM halafu hiyo mitambo ya umeme ikajengwa DSM, Kwa mjinga hii ina mantiki sana. Sasa eti CCM saa hizi ndio inataka wananchi wa mtwara watumie akili kufikiri ili waone mantiki ya serikali katika kusafirisha gas,too late subirini watu wafe tu kwa sababu ni mbegu mliyoipanda. kama mngetaka jamii ambayo inayoweza kujenga hoja mngeitengeneza.
Kama CCM wangejishugulisha kutoa ujinga katika jamii, hili bomba la gas wala tusingebishana kuhusu kulijenga labda tungebishania mikataba yake imekaaje na itawanufaishaje wananchi