Mtaji wa 46M faida 540,000, pia mtaji wa 45M faida 576,000

malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
2,780
2,716
Habari wakuu mnaionaje hizi baishara ni za kuendelea kufanya kweli tandam ya gari ya sukari inabeba mifuko 600 ya sukari unaiuza kwa miezi 2 na faida yake ni 540,000 wakati huo gharama za manunuzi 46m faida kwa Kila mfuko jumla jumla ni tsh 900.

Wakati huo huo mtaji wa gari ya ngano 45m hapo gari ya ton 32 sawa na mifuko 1280 kwa Kila mfuko ukiuza jumla faida ni tsh 450 sawa jumla ya 576,000 kwa mifuko yote ambayo unaiuza kwa miezi 2.

Je, wakuu hii biashara inanichanganya sana mtaji mkuwa faida kidogo, tupeane fursa za hela ili tubadilishe biashara tupate faida anagalau inayoendana na mtaji.
 
Biashara small scale isiyoniachia 10% net profit baada ya makato yote ya Serikali, kodi, matumizi na kila kitu hiyo siifanyi!

Ingekuwa mtu amewekeza bilioni 1 na biashara ni very stable inampa 2% faida kwa mwezi hapo angalau. Wewe hufanyi biashara, unazurura ofisini.
 
Habari wakuu mnaionaje hizi baishara ni zakuendelea kufanya kweli tandam ya gari ya sukari inabeba mifuko 600 ya sukar unaiuza kwa miezi2 nafaida yake ni 540000 wakati huo gharama zamanunuzi 46m faida kwa Kila mfuko jumla jumla ni tsh 900.

Wakati huo huo mtaji wa gari ya ngano 45m hapo gari ya ton32 sawa namifuko 1280 kwa Kila mfuko ukiuza jumla faida ni tsh 450 sawa jumla ya 576000 kwa mifuko yote ambayo unaiuza kwa miezi 2.

Je, wakuu hii biashara inanichanganya sana mtaji mkuwa faida kidgo tupeane fursa za hela ili tubadilishe biashara tupate faida anagalau inayoendana na mtaji
Hiyo biashara wanafanya watu wenye mitaji mikubwa mno. Unakuta ana gar 3 au 4..au ni kwamba hiyo gari umeitega mahala sio..mwisho wa siku gari itachoka na faida hujapata...nenda kaitege sehemu yenye uhitaji kweli kweli yaan gari ipige kaz kwa wik ukunje hata 1m.
La hasha ni bora uitie UTT tu ...

Biashara kama huna uzoefu nazo na ndio unaanza ndugu hiyo hela itapotea yote ibaki kumbukumbu tu nilikua na hela fulani.

La hasha tafuta mentor wa biashara anaefanya vizuri kaa nae upite anakopita yeye...awe tayari lakini
 
Biashara small scale isiyoniachia 10% net profit baada ya makato yote ya serikali, kodi, matumizi na kila kitu hiyo siifanyi!

Ingekuwa mtu amewekeza bilioni 1 na biashara ni very stable inampa 2% faida kwa mwezi hapo angalau. Wewe hufanyi biashara, unazurura ofisini.
Kwahiyo mkuu tufanye biashara gani
 
Habari wakuu mnaionaje hizi baishara ni zakuendelea kufanya kweli tandam ya gari ya sukari inabeba mifuko 600 ya sukar unaiuza kwa miezi2 nafaida yake ni 540000 wakati huo gharama zamanunuzi 46m faida kwa Kila mfuko jumla jumla ni tsh 900.

Wakati huo huo mtaji wa gari ya ngano 45m hapo gari ya ton32 sawa namifuko 1280 kwa Kila mfuko ukiuza jumla faida ni tsh 450 sawa jumla ya 576000 kwa mifuko yote ambayo unaiuza kwa miezi 2.

Je, wakuu hii biashara inanichanganya sana mtaji mkuwa faida kidgo tupeane fursa za hela ili tubadilishe biashara tupate faida anagalau inayoendana na mtaji
Loh achana na hyo business mm kuna business nimeanza december mwaka jana faida average kwa mwezi ni almost 600k na nilianza na mtaji wa 3.5m hyo 600k nishatoa matumiz.
 
Back
Top Bottom