Mtaje mchezaji ambaye hujawahi kumuona akicheza ili wakongwe wakuchambulie sifa zake

Watu wa zamani wanajisifiaga tu ila kiukweli hawakujua mpira
 
Huu ni uzi maalum wa kutaja wachezaji wa zamani ambao hukuwahi kuwaona wakicheza. Ukishawataja subiria wakongwe waliomuona akicheza waje wakuoe sifa zake.

Mimi sijawahi kumuona George Magere Masatu akicheza, naombeni mnitajie uwezo wake maana yupi hyped sana
Alikuwa balaa, alikuwa anatisha, alikuqa jembe sana, alikuwa mwamba.
 
Watu wa zamani wanajisifiaga tu ila kiukweli hawakujua mpira
Zamani ni Zipi ?

Na Taifa Stars ipi ilishawahi kupata mafanikio kuliko nyingine achana na hii iliyokwenda AFCON baada ya AFCON kuongezewa Timu....

Unamjua Hussein Amani Masha na alivyocheza kwa akili, yaani kwa Madaha na kutanua huku pasi zake zikiwa na macho (angekuwa Ulaya ungekuwa unaongelea kina Patrick Viera aliyechanganyikana na Pirlo)

Mpira wa zamani ulikuwa mpira kweli unahitaji na nguvu na ubabe ndani sio sasa hivi imekuwa non contact sport hata mtu mwenye kifafa unaweza kucheza.... , yaani zamani kwenye ammunition yako sio ujuzi tu bali ulihitaji nguvu pia
 
Natamani kuwajua hawa jamaa (Gerd Muller),(Alan Shearer),na Robert Carlos
Allan Shearer mchovu tu zaidi ya kufunga alikuwa hana cha zaidi ila ndio hivyo kipenzi cha Magpies (Newcastle) Gullit alijifanya kumuweka mkeka kilichotokea ni kupoteza kibarua chake......
 
Natamani kuwajua hawa jamaa (Gerd Muller),(Alan Shearer),na Robert Carlos
Alan Shearer alivunja rekodi mara mbili ya usajili enzi hizo. Kwanza kabisa alipotoka Southampton kwenda Blackburn ambapo alitwaa ubingwa huku magoli yake yakichangia ubingwa.

Mara ya pili alivunja rekodi alipotoka Blackburn kwenda Newcastle. Jamaa alikuwa analijua sana goli.

Kilichomfanya afunge magoli mengi kwenye EPL ni kwakuwa alicheza timu ambazo hazina presha kubwa. Ni kama ilivyo kwa Harry Kane kwa zama hizi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom