Mtafaruku mkubwa CCM Mkuranga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtafaruku mkubwa CCM Mkuranga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dedam, Apr 30, 2012.

 1. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mtafaruku mkubwa unafukutu ndani ya CCM Mkuranga baada ya madiwani 18 wa halmashauri ya Mkuranga kumpinga mbunge wao pamoja na mkurungenzi wa halmashauri ndugu Sipora Liana na m/kiti wa halmashauri ndugu Magaila kutokana na ubadhirifu wanaofanya.

  Taarifa zinadai kuwa viongozi hao watatu wanashirikiana kwa pamoja kufuja mali za umma kwa maslahi yao binafsi.

  Duru za siasa wilayani Mkuranga zinadai kuwa wananchi wengi hawana imani na viongozi hawa na taarifa kuna wazee wapatao 500 wamejiandikisha na wanafanya utaratibu na moja chama cha cha upinzani ili waweze kuhamia huko.

  Wananchi wengi hawaridhishwi na uongozi wa mbunge wao adamu malima kuwa hajafanya cha maana tangu achaguliwe zaidi kumwaga nguzo za umeme chini bila kufanyiwa kazi kwa muda mrefu sasa pia mbunge huyo inadaiwa ana dharau na visasi kwa wananchi kwa wale ambao hawakumpa kura.

  Adam Malima inasemekana haelewani na swahiba wake mkubwa diwani wa kata ya mkamba ndugu HASANI DUNDA, Malima inadaiwa hataki kabisa kumuona diwani.
   
 2. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huo ni uongo mtupu.
  1. Laptop tatu
  2. Bunduki 2
  3. Passport 2
  4. US$4,000
  5. TZS 1,500,000
  6. Mikufu ya dhahabu
  7. Shoe shining yake London
  8. Mfadhili NRA

  Watu hamna shukrani.
   
 3. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Huu mvutano wa madiwani na mkurugenzi Mkuranga ulianza pindi ambapo mkurugenzi wa sasa alipopelekwa. Kwa wale wenye kufuatilia mambo ya serikali za mitaa watamtambua huyu mama kuwa ni mtendaji wenye rekodi ya kutokudumu katika halmashauri ukianzia na Moshi Vijijini na baadae Monduli kutokana na kutokuogopa wanasiasa mafisadi. Ana rekodi nzuri ya kuboresha mapato ya halmashauri ila pia ni ngangari kweli kweli. Halmashauri ya Mkuranga imebadilika sana katika miaka 3 iliyopita kutokana na dira ya huyu mama na usimamizi wake, ujenzi wa jengo la ofisi umeshakamilika huku yale ya kituo cha kitega uchumi, machinjio, soko na stendi yakiwa katika mchakato mzuri.

  Mkuranga ni wilaya kichaa iliyojaa wanasiasa wenye kuweka mbele maslahi binafsi na utete wa hali hii unajulikana hata TAMISEMI.
   
 4. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Mh!!! haya
   
 5. k

  kansiana Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nakubaliana nawe na namkubali Mkurugenzi SIPORA LIANA kuwa ni Mwadilifu na anazingatia
   
 6. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dhambi ya uzinzi inamtafuna mzee wa kunyonya chuchu a.k.a mzee wa mapete na mabunduki.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Kuongoza uswahilini kaaazi.....
   
 8. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,201
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Sina shaka na utendaji kazi wa yule DED ila ana tatizo la kukosa washauri wazuri, anasikiliza sana majungu, ana visasi dhidi ya watendaji wake na imefika hatua sasa madiwani wanajiorodhesha ili kumkataa. Sina data za kutosha kuhusu hali ya CCM ila walau najua kuwa Malima na DED hawakubaliki kabisa na madiwani wakiongozwa na Bw KUBENEA
   
 9. Falcon

  Falcon JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wampeleke mzee Ali Hassan mwinyi akasawazishe
   
 10. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  kweli kabisa sipora aliingia na moto mkali sana mkuranga lakini sasa ameshikwa masikio na wajanja. Kuhusu mgogoro kati ya malima na baadhi ya madiwani hususani mh. Hassani dunda juzi waliitwa na wazee wa kata ya mkamba ili waaeleze chanzo cha wao kutoelewana hali iliyosababisha barabara ya kimanzichana -mkamba kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu kwenye kikao hicho inadaiwa kama kawaida malima alikacha kikao hicho na kutuma wawakilishi ambao waligawa pesa tsh 4000 kwa kila mzee aliyefika. Kutokana na malima kupoteza mvuto inasemekana mpinzani wake kisiasa ndugu mtembei ameanza kujipanga kisiasa.
   
 11. m

  matawi JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Zoezi la wafu kuzikana naona linaenda vizuri. Asante mungu baba kuruhusu haya kutokea maana bila wewe magamba wangetumaliza
   
 12. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeennnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnn
   
 13. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  madiwani hao wana njaa kali. ndio maana wanampiga vita huyo mama ambaye huhesabu mpaka vifusi barabarani kabla ya kupitisha malipo.
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kila Mtanzania alikua anshangaa kwa mtaji wa ANASA YA KUTISHA kwa huyu Mbunge wa Mkuranga na kujilinda na zana za kivita mikoani hivi kweli Wana-Mkuranga safu yao ya maendeleo itakua ni salama kweli.

  JF, ni jukumu letu kutuma ujumbe mzito Mkuranga ili kuhakikisha kwamba SAUTI YA WANYONGE pale inasikika kama ambavyo krimu ya uongozi wao mashinani ukiongozwa na jopo kubwa la madiwa 18 walivyokwishatia shaka mwenendo mzima wa mambo huko jimboni.

  Eti watu kama huyu Malima ndio kati ya watu wanaoitwa MAWAZIRI na kukaa kuamua hatima ya taifa letu; ni kero na huruma kweli!!!


   
 15. w

  wamwala Senior Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu mama sio wala nini kamfukuza jamaa yangu kazi kisa alimtaka kimapenzi na jamaaa akamtosa. Anajifanya anajua kubana watu bt ndio type za kina Blandina Nyoni. CDM waende waweke nguvu ya kutosha pale 2015 tuchukue jimbo hilo
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  swahiba wake mkubwa alafu haelewani nae. Swaiba kivipi tena hapo sasa!
   
 17. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  Huyu Malima ni yupi? Yule aliyetapeliwa na Malaya baada ya uchovu?
   
 18. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  ndiyo huyo huyo mzee wa totoz
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jimbo la Mkuranga kuzaa 'DHAHABU' CHADEMA hivi karibuni. Habari ndio hiyo.
   
 20. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hivi mbunge, mkuu wa wilaya au watu kwenye halmashauri yupi ndio bosi wa wote...nani ana say zaidi katika jimbo..??
   
Loading...