Mtaani kwetu tunaheshimiana sana

Mtaani kwetu tunaheshimiana sana

basha unguja

Member
Joined
Sep 28, 2016
Posts
83
Reaction score
77
Wasaaaalam,

Yapita miaka miwili kama na nusu hivi nilipokuwa na kigenge pale uswazi kwetu, sasa kwa kuwa mtaji wangu ulikuwa mdogo hivyo genge langu halikuwa limenona kiviiiile, jambo ambalo wateja wangu walikuwa wakija wananidhihaki saaana, wengine hasa wadada wa kitaa wakipita wakawa wananitambia kwa sauti, "heheheeee waaatu na supermarket zaooooo" ilikuwa inaniuma saaana ila sikuwa na jinsi, nikavumilia yoooote japo roho ilikuwa inauma saaana!

Sasa mwaka huu uchumi wangu uko stable kinoma noma kiasi kwamba nina duka-genge limenona kwa level za uswazi kwetu kwa sana tu, mpaka serikali inapotangaza uchumi kukua nahisi kama vile wamenichukua kama sample to evaluate data zao za kiuchumi. Chakushangaza waleeeeee waliokuwa wananibeza kipindi kileee eti sasa, mara nipewe shikamoo, mara niitwe mkuu, Kamanda, Jembe, Ze Don , Mheshimiwa na majina hayo yooote napewa sana sana nyakati wakitaka kukopa na kiungwana tu nimeweka bango kuubwa, "SIKOPESHI" Yaani heshima imerudi kiasi kwamba imefikia hatua naitwa SWEET MANGI wakati mie ni mpemba hatari saaaana. Mtu anakuuliza bei ya kitu unamtajia etii, oohh Mangi you are so funny!! wakati sijatabasam hata kutabasamu yaani ni full uchozi uchokozi, hachokoziki mtu hapa........

NB: SIFURAHII WATU HALI ZAO KUBANA ILA DHARAU ZAO ZILEE NAHISI ZINAWAPONZA SASA SIJUI WALIKUWA WATU WA kitonga sana KIPINDI KILE HATA SIELEWI JEURI ZILE SIJUI WALIKUWA WANATOA WAPI? ILA NOW SHIKAMOO MANGI UKIANGALIA ANAYEKUPA SHIKAMOO UMRI UMEENDA KINOMA DUUH!

Sijui pande za kitaa chenu huko kupoje? Hasa uswazi uswazi flan hv
 
Zam yako mkuu kama umeweza kukuza uchumi wako zama hzi hongera
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom