Ndiyo hivyo ndugu yangu,huwa ninawashangaa sana watu ktk nchi hii,utakuta mtu yupo kwenye system anakula Mshahara mkubwa halafu anamshauri mhitimu wa chuo kikuu kuwa ajiajiri mwenyewe, wakati huo unakuta mwingine ni Mzee na hataki kustaafu lkn akisimama jukwaani Anawaambia vijana kuwa wajiajiri,sasa unajiuliza swali hivi Mbona yeye hajaachia ngazi ili akajiajiri maana anao mtaji?!!!.Ishu ya kujiajiri ni nzuri lkn vijana wetu hawana mitaji na kwa Bahati mbaya Serikali yetu Haina mifumo mizuri ya kuwawezesha wahitimu wa vyuo kujiajiri.Km wenye mitaji wenyewe, yaani Watumishi waliokwisha kuajiriwa wanashindwa kujiajiri unadhani mhitimu wa chuo ataweza??.