Mtaalamu wa kilimo;uliza ujibiwe.

Ni zao gani la kibiashara ambalo linakubali kwenye ardhi ya morogoro ambalo lina stable prices na soko ni la uhakika??
 
Okay, asante sana je wanatoa mafunzo ya hydroponic pekee ake kaa mtu unataka kusoma hydroponic tuu
 
Ni zao gani la kibiashara ambalo linakubali kwenye ardhi ya morogoro ambalo lina stable prices na soko ni la uhakika??
ardhi ya morogoro imegawanyika katika kanda..
kuna nyanda zilizopo juu,kati na chini.katika nyanda zilizopo juu ndizo hulima kahawa kwa kiwango fulani( zao hili lina bei isiyoyumba sana)
nyanda za chini hulima mpunga ambao kwa kweli hutegemea sana mvua ya mwaka husika,kwani mvua ikiwa ndogo bei huwa juu na kinyume chake.
hivyo swali lako ni zuri ila je unataka kulima wilaya ipi ya mkoa wa morogoro?
 
Wilaya ya Mvomero
 
Okay, asante sana je wanatoa mafunzo ya hydroponic pekee ake kaa mtu unataka kusoma hydroponic tuu
SUA huwa kuna kozi za muda mfupi ambazo hutolewa kwa wahitaji wa kozi husika,hivyo kama unahitaji kozi hiyo unaweza kwenda moja kwa moja SUA au mbadala wake unaweza kujifunza wataalamu wengine ambao wamebobea juu ya kilimo hicho cha kisasa kisicho hitaji ardhi.
 
Dawa gani hutibu kinyaushi katika nyanya ugonjwa ambao hufanya mmea kusinyaa na badae kunyauka na kukauka kabisa .ikiwezekana na njia za kuuzuia
 
Wilaya ya Mvomero
Wilaya ya mvomero inafanya kilimo cha kokoa,ufuta,mpunga,ndizi,Kahawa,Maharage,mbaazi,nazi,choroko,nyanya,njegere,Mahindi,Mitiki.
katika hivyo vyoote ni mpunga na kahawa ndio vyenye soko la kueleweka.katika hivyo viwili kahawa huchukua zaidi ya miaka mitatu kupata faida inayoonekana.
hivyo kama mvumilivu kalime kahawa na kama unataka pesa kwa haraka kalime mpunga hutajuta kabisa ila jiandae uhudumiaji.
 
Shukrani sana
 
Dawa gani hutibu kinyaushi katika nyanya ugonjwa ambao hufanya mmea kusinyaa na badae kunyauka na kukauka kabisa .ikiwezekana na njia za kuuzuia
ugonjwa wa mnyauko wa nyanya huweza kusababishwa na wadudu wengi sana na mmoja wao hujulikana kama Ralstonia solanacearum ambao kibongo bongo wamekuwa ni tatizo kubwa sana kuwaangamiza lakini njia zifuatazo huweza kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la mnyauko wa nyanya.
Kwa kutumia bleaching powders ambao huwa ni mchanganyiko wa soil disinfectants na chokaa ambayo huweza kutumika kwa kiasi cha kilo 30 kwa hekta na huwa mbolea kwa namna moja na kiua vinyaushi kwa upande mwengine.
lakini muda mwingine mnyauko huweza kusababishwa na fungi/kuvu waitwao Phytophthora infestans hawa huweza kuuliwa kwa kutumia dawa kama ivory72,success n.k.
asante
 
Mazao yanayozalishwa ktk teknolojia ya hydroponic ni lazima yakuzwe ndani ya greenhouse
si razima,ila kwa ubora wa mazao yako kwa wanunuzi na pia njia rahisi kukinga wadudu hatari hewani(air borne microbes) na wadudu wengine unashauriwa ulime ndani ya kitalu nyumba (green house).
 
Au yanakuzwa ktk mazingira gani?
Teknologia ya hydroponics inakuza mazao hasa mbogamboga bila uwepo wa ardhi na hiyo virutubisho huweza kuwekwa kwenye maji ambamo mizizi ya mmea husika imepandikizwa au kushikizwa na mazingira stahiki huwa ni kwenye kitaru nyumba(green house) na ikifanyike nje ya hapo huwa kunakuwa na changamoto nyingi hasa wadudu na magonjwa.
asante.
 
Kuna tofauti gani kati ya green house na net house?

Je, kunakuwa na tofauti ya ubora wa mazao ya mbogamboga kutegemea mfumo uliotumika (gh au net house)?
 
Naomba kujua mahtaji ya kuzalisha viazi ulaya.
kabla hujaanza kulima angalia hali ya hewa kama inaruhusu kilimo viazi hali ya 10-22c
uwe umeandaa shamba lako,mbegu,mbolea(DAP+CAN) kwa ratio ya 2:1,madawa ya wadudu na ukungu(early and late blight diseases),pesa za kupalilia na taslimu kwa ajili ya dharula.ila kumbuka kuwa baadhi ya mbegu kama alika ni lazima uwe na muda wa kutosha kwani huwa ni rahisi kushambuliwa na ukungu ukilinganisha na meru au red almasi.
 
Kuna tofauti gani kati ya green house na net house?

Je, kunakuwa na tofauti ya ubora wa mazao ya mbogamboga kutegemea mfumo uliotumika (gh au net house)?
Labda nianze kwa kusema kuwa watu wengi hushindwa kutofautisha kati ya green house na net house.
kwa kawaida neno green house hutumika kuelezea nyumba kitalu inayotumia hali ya hewa inayokuwa controlled na mara nyingi huweza kuitwa screen house ambamo hali ya hewa huweza kuwekwa kulingana na mahitaji ya mimea mfano kiasi cha mwanga,hewa.joto na pia kudhibiti wadudu wahalibifu.
kwa upande wa net house huwa ni nyumba kitalu iliyojengwa kwa kutumia karatasi ya plastiki kwa juu na net ngumu na maalumu kwa pembeni nahii ni kuwa hali ya hewa huwa ya kawaida ila tu hukinga wadudu wahalibifu tofauti na kupanda nje ya net house..
lakini vyote kwa sasa zote watu huziita green house.
 
Nahitaji msaada kidogo kuhusu kilimo cha mpunga, aina ya mbegu, upandaji, usimamizi mpaka uvunaji pamoja na gharama yake kwa heka. Hata kama utasuggest machapisho, video au vyanzo vingine navyoweza kupata taarifa hizi utakuwa msaada mkubwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom