Mtaalam wa Saikolojia asema kwamba ukiona upo katika Mahusiano halafu hunenepi na unakondeana tu jua upo kwa Mtu siyo sahihi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,177
Amesema kwenye Mahusiano ya kweli na ya dhati kabisa lazima wote wawili mtakuwa na afya njema na hata Miili yenu itakiwa ' inanawiri ' kwa Kunenepa ama Kiasi au Sana ila ukiona hali ni tofauti jua haupo kwa Mtu sahihi hivyo fanya maamuzi ya haraka ya Kuachana nae na umtafute yule aliye sahihi na chaguo lako la kweli / dhati.

Haya siyo maneno yangu GENTAMYCINE bali ni maneno ya Kiutaalam na Kisaikolojia kabisa kutoka Mtu mmoja maarufu kwa Elimu ya Saikolojia nchini ( jina Kapuni / nalihifadhi ) ambapo aliweza ' Kunidokezea ' na Mimi baada ya kuambiwa hili nilianza kuwaangalia Marafiki zangu wawili watatu ambapo kuna mmoja kabla hajaoa alikuwa ni SIMTANK lakini alipooa tu sasa amekuwa FIDODIDO na anazidi tu ' Kukongoroka ' huku kuna mwingine kabla ya Kuoa Yeye na Mwenzake wote walikuwa ' mbaumbau ' lakini tokea waishi pamoja sasa ' wamenenepeana ' mno halafu wanapendana Kunakotukuka hadi Sisi wengine ambao bado ni ' Waoga / Manyali ' wa Kuoa tunawaonea Wivu.

Kazi ipo!

Nawasilisha.
 
Kwenye huu uzi nilichogundua ni kwamba aliekuwa mnene kabla ya kuoa amekonda baada ya kuoa.

Na waliokuwa wembamba kabla ya kuoa wamekuwa wanene.

Hivyo wanaotaka kunenepa ama kupungua wakiwa ndoani wazingatie vigezo.
 
Kwenye huu uzi nilichogundua ni kwamba aliekuwa mnene kabla ya kuoa amekonda baada ya kuoa.

Na waliokuwa wembamba kabla ya kuoa wamekuwa wanene.

Hivyo wanaotaka kunenepa ama kupungua wakiwa ndoani wazingatie vigezo.
We kweli ni Great thinker...upo sahihi kabisaa
 
Back
Top Bottom