Mtaalam asema Watanzania tujiandae kwa Msiba mzito muda wowote Daraja la Mto Wami

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Nikiwa natokea Tanga leo asubuhi huku nikiwa nimebahatika kukaa karibu na Mhandisi mmoja ' maarufu ' sana nchini hasa kwa ' uweledi ' wake katika masuala mazima ya ' Kiuhandisi ' ndani na nje ya Tanzania kama kawaida yangu ya kupenda kuwa ' inquisitive ' pale ninapojua nimekaa na ' Mtaalam ' niliweza kuzungumza nae mawili matatu hasa hasa juu ya lile daraja la Wami ndipo huyu Mhandisi ' akafunguka ' zaidi Kwangu.

Wakati tunakaribia daraja lenyewe la Mto Wami nikamgeukia huyu Mhandisi na kumuuliza kuwa kulikoni hili daraja hadi sasa linazeeka hivi na hakuna kinachofanyika wakati Wao kama ' Wataalam ' wetu wapo?

Huyu Mhandisi katika kunijibu wala hakutaka kupepesa macho, kumung'unya mdomo na kutikisa masikio na akaenda moja kwa moja kunijibu hivi kama ambavyo nayanukuu maneno yake " Bwana mdogo GENTAMYCINE hivi unadhani aliyesema ule msemo wa no hurry in Africa alikosea? Kwa taarifa yako tu tumeshapeleka ushauri wetu wa Kitaalam kabisa huko kunakohusika huu ni mwaka wa 18 sasa lakini tunapuuzwa tu na labda pengine kwakuwa sisi ni Waafrika ndiyo maana ushauri wetu umewekwa Kapuni "

Mhandisi hakuishia tu hapo akaenda mbele na kusema tena na namnukuu " GENTAMYCINE nadhani hata hivi tunavyopita hapa darajani sasa unaweza ukahisi kitu fulani hakijakaa sawa na labda nikuambie tu kuwa nina uzoefu wa masuala mazima ya Kiuhandisi nakuhakikishia kama ndani ya miezi 6 au 9 ijayo hakuna marekebisho makubwa au ujenzi wa daraja jipya utakaofanyika Watanzania tujiandaeni kupokea Msiba mzito sana wa Kitaifa kwani hili daraja hivi sasa halina muda mrefu litaanguka na Watu kupotelea Mtoni ambako Mto wenyewe tu una Kina kirefu na kibaya zaidi ndiyo Mto nadhani ambao kwa Tanzania una Mamba wakubwa mno ukiondoa Mto Ruaha ".

Mnaohusika na suala hili nadhani ' ujumbe ' huu wa Kitaalam kabisa utakuwa umewafikia na nawaomba kupitia ' uzi ' huu huu basi muambiane na haraka haraka mjipange mfanye ujenzi pale Darajani Mto Wami ili muokoe maisha yetu sisi Watanzania ' wanyonge ' wa Kimaisha ambao usafiri wetu mkubwa ni ' Bombardier ' za ardhini tu.

Mwisho nitoe tu RAI kwenu enyi Mamlaka husika acheni hii tabia ya kufungia katika ' Makabrasha ' yenu taarifa muhimu na nyeti zenye maslahi mapana na mazito kwa nchi kama hizi kwani haiwezekani kuwa kumbe mlishawahi kupewa ushauri wa Kitaalam kabisa miaka 18 iliyopita na cha kushangaza kama siyo kutia aibu mpaka leo hakuna kilichofanyika halafu mpo mpo tu. au mnataka mtutoe ' Kafara ' hapo Darajani Mto Wami?

Tunaomba Daraja jipya Mto Wami upesi sana.

Nawasilisha.
 
Lile daraja lilisha ongelewa sana humu! Hamna siku ambayo inapita hapajatokea ajali pale, hata leo ukipita hapo utakuta kuna gari zimeanguka!

Lile daraja siyo la kuliamini sana! Ni suala la mda tu! Prof Mbarawa sijui halioni anaona tu bora wanunue radar
 
Habari za kizushi Enzi za kiwanda cha bia kina milikiwa na serikali Yale nagari Isuzu injection ndio yalikuwa yanabeba bia yalikuwa yanaanguka Sana daraja lilikuwa dogo na la kusubiriana... Baadae miaka ya 1993 nadhani ujenzi Wa daraja jipya ilikuwa unaendelea.. Nadhani kama 1994 au 95 ulikuwa ushaisha sasa tokea miaka hiyo kwa daraja jipya si rahisi kuwa chakavu hadi utishe watu labda kama daraja lilitengenezwa kizembe. Daraja la selander lina miaka ya kutosha na Bado lipo njema.. Maisha ya madaraja ni zaidi ya miaka mia
 
nahisi kweli kuna kitu kinaweza tokea pale, huwa nikianza kuweka Tairi pale naingiwa na woga wa ajabu sana, na hata nikiwa na safari ya huko huwa napafikiria sana pale.

Binafsi ni Mhandisi, na kuna siku nimepita hapo na jamaa yangu nikaanza kumuuliza alternative way ya kufika tanga, Arusha na Moshi kama hilo daraja siku likivunjika, ukiliangalia hilo daraja kwa jicho la kitaalamu utaona namna tunavyoishi bado zama za mawe aka stone age.
 
Nikiwa natokea Tanga leo asubuhi huku nikiwa nimebahatika kukaa karibu na Mhandisi mmoja ' maarufu ' sana nchini hasa kwa ' uweledi ' wake katika masuala mazima ya ' Kiuhandisi ' ndani na nje ya Tanzania kama kawaida yangu ya kupenda kuwa ' inquisitive ' pale ninapojua nimekaa na ' Mtaalam ' niliweza kuzungumza nae mawili matatu hasa hasa juu ya lile daraja la Wami ndipo huyu Mhandisi ' akafunguka ' zaidi Kwangu.

Wakati tunakaribia daraja lenyewe la Mto Wami nikamgeukia huyu Mhandisi na kumuuliza kuwa kulikoni hili daraja hadi sasa linazeeka hivi na hakuna kinachofanyika wakati Wao kama ' Wataalam ' wetu wapo?

Huyu Mhandisi katika kunijibu wala hakutaka kupepesa macho, kumung'unya mdomo na kutikisa masikio na akaenda moja kwa moja kunijibu hivi kama ambavyo nayanukuu maneno yake " Bwana mdogo GENTAMYCINE hivi unadhani aliyesema ule msemo wa no hurry in Africa alikosea? Kwa taarifa yako tu tumeshapeleka ushauri wetu wa Kitaalam kabisa huko kunakohusika huu ni mwaka wa 18 sasa lakini tunapuuzwa tu na labda pengine kwakuwa sisi ni Waafrika ndiyo maana ushauri wetu umewekwa Kapuni "

Mhandisi hakuishia tu hapo akaenda mbele na kusema tena na namnukuu " GENTAMYCINE nadhani hata hivi tunavyopita hapa darajani sasa unaweza ukahisi kitu fulani hakijakaa sawa na labda nikuambie tu kuwa nina uzoefu wa masuala mazima ya Kiuhandisi nakuhakikishia kama ndani ya miezi 6 au 9 ijayo hakuna marekebisho makubwa au ujenzi wa daraja jipya utakaofanyika Watanzania tujiandaeni kupokea Msiba mzito sana wa Kitaifa kwani hili daraja hivi sasa halina muda mrefu litaanguka na Watu kupotelea Mtoni ambako Mto wenyewe tu una Kina kirefu na kibaya zaidi ndiyo Mto nadhani ambao kwa Tanzania una Mamba wakubwa mno ukiondoa Mto Ruaha ".

Mnaohusika na suala hili nadhani ' ujumbe ' huu wa Kitaalam kabisa utakuwa umewafikia na nawaomba kupitia ' uzi ' huu huu basi muambiane na haraka haraka mjipange mfanye ujenzi pale Darajani Mto Wami ili muokoe maisha yetu sisi Watanzania ' wanyonge ' wa Kimaisha ambao usafiri wetu mkubwa ni ' Bombardier ' za ardhini tu.

Mwisho nitoe tu RAI kwenu enyi Mamlaka husika acheni hii tabia ya kufungia katika ' Makabrasha ' yenu taarifa muhimu na nyeti zenye maslahi mapana na mazito kwa nchi kama hizi kwani haiwezekani kuwa kumbe mlishawahi kupewa ushauri wa Kitaalam kabisa miaka 18 iliyopita na cha kushangaza kama siyo kutia aibu mpaka leo hakuna kilichofanyika halafu mpo mpo tu. au mnataka mtutoe ' Kafara ' hapo Darajani Mto Wami?

Tunaomba Daraja jipya Mto Wami upesi sana.

Nawasilisha.
Mkuu vipi hujamuuliza lililopo lilijengwa mwaka gani
 
Kumbe kuna watu wanauchungu na maono ya mbali kama mimi kuhusu hilo daraja la mto wami,kuna siku tulikuwa tunasafiri tukakuta ajali hapo darajani,wahanga wa ile kadhia kila mtu aliongea yake kwa uchungu mkuu! Kwa sababu sikuhiyo tulikaa hapo darajani kwa takribani masaa manane.Nadhani kila mtu anajua umuhimu wa daraja la mto wami hasa watu wanaotokea kaskazini.Ni muda muafaka sasa wa kuwa na daraja la kueleweka.
 
Back
Top Bottom