Mtaala mpya elimu ya msingi unaishia darasa la sita, wizara na waziri husika tunataka maelekezo

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,502
6,403
Habari
Hii ipo Tanzania tu duniani

Itakumbukwa serikali ya Tanzania kupitia wizara ya elimu chini ya waziri profesa mwenye ingilishi yake Joyce Ndalichako walifanya mabadiliko ya mtaala wa elimu ya msingi na ukanza kutumika katika kutoa elimu kwa shule zote za msingi hapa nchini

Mtaala huo ulikuja na mabadiliko kadhaa ikiwepo wanafunzi wasome elimu ya msingi kwa miaka sita badala ya miaka saba kama zamani

Miongozo ya kufundisha mtaala mpya ulitolewa ukionesha watoto watasoma mwisho darasa la sita

Mwaka huu wamefika darasa la sita na hakuna mabadiliko yoyote yale katika muongozo wa kuwafundisha wanafunzi

Sylabus inaonesha wanaishia darasa la sita lakini tunajua watasoma mpaka mwakani pia
Je mwakani watafundishwa mambo gani ikiwa sylabus yao imeisha mwaka huu?

Serikali yetu inapenda kushitukiza mambo pasipo kujiandaa, ni vema wizara husika ikatoa muongozo mapema

Ujulikane kama mwakani watoto watapoteza muda wa mwaka mmoja kwa kufanya revision tu au kuna content itaongezwa

Kama content itaongezwa katika kila somo, wao wataitoa wapi ambayo itaendana na uwezo wa watoto na matakwa ya jamii

Ndalichako na watu wako huko wizarani tunataka muongozo katika hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom