...Msuya atupa mzigo kwa Mkapa

Mniwie radhi ila huyu mzee naona kama anakaribia kufa kwa hizi kauli zake. Hata mzee kawawa alianza hivi hivi. Kaniudhi sana kwa kutomheshimu dr phD. Kwetu vijana ambao hatukuushuhudia uongozi wa mwalhmu huwa tunafarijika sana na uwepo wa Slaa kuliko anavodhani huyu mzee na magamba wenziea
 
Huyu mzee analeta mbinu za kijinga na kipumbavu kweli. Kama yeye hajaona viongozi wazalendo anatushauri nini??? Wananchi wadanganyike na kukata tamaa kuwa hawa waliopo waendelee kwa sababu hakuna wanaofaa?! Hajaona wanaofaa lkn hapohapo anategemea walio madarakani watatue matatizo yanayotukabili!!! Kwanza nani alimdanganya kuwa anaaminika kwa watanganyika?
 
Tukitaka kurudi kinyume nyume huyu Mzee Msuya itabidi aunganishwe na akina Gray Mgonja na Yona kwani katika uongozi wake alifanya makosa makubwa mengi hususan; kuelekeza raslimali za Taifa kwa ajili ya kujenga miundombinu ya wilaya ya Mwanga anakotoka ambayo haina uzalishaji wowote Wa maana unaochangia kwenye mfuko Taifa. Pili kuendeleza ukabila Wa wazi wazi kwa kupendelea jamii ya watu Wa eneo anakotoka, tatu kuingiza migogoro ya kidini kwa ajili ya kuwagawanya wapare, tatu kushiriki katika kupanga mauaji ya Edward Sokoine.

Kwa wale vijana wadogo humu jamvini nawasihi mumuogope huyu Mzee Msuya kama Ukoma
 
Msuya naye anasema watu wanamsikiliza ? Mpuuzi huyu mkuu wa migogoro kila kukicha .Ana nini cha kutuelezea huyu sasa na shida zentu ? Majira nao lakini ni wale wale badala ya kuafuata mtu wa maaana wanaenda kwa Msuya .Msuya mkongwe wa Siasa za umimi na CCM yake hana habari na Dunia iko vipi sasa atasema nini ?
 
Msuya amesema sawa!!! Amekosoa viongozi wote tu, wenye dola na wapinzani!!!

Lakini na yeye asisahau, na pia hatujasahau machafu yake!!! Huyu mzee alikuwa mbinafsi sana!! Hakuweza ku-accumulate mali kwa kuwa Mzee Nyerere (RIP) alikuwapo!!! Nyani halioni kundule...waswahili walisema.

Yeye atulie azeeke vizuri tu...
 
Quote"Tuchukue mfano kwa Mwalimu, watoto wake na Mzee Kawawa utagundua kuwa licha ya kukaa madarakani kwa muda mrefu maisha yao ni ya kwaida kama watanzania wengine tofauti na sasa tunavyoshuhudia watu wameenda kujilimbikizia mabilioni nje ya nchi huku wakiyaita vijisenti...,"

Hii quote hapo juu sijaelewa vizuri Msuya alichomaanisha. Kwa mtizamo wake yeye watoto wa Kawawa wanafanya nini cha maana CCM tofauti na wengine? Yeye Msuya watoto wake karibia wote wanaishi nje ya nchi, kwenye nyumba za kifahari na kazi nzuri. Sisemi kwamba ni ufisadi kwasababu inawezekana ikawa juhudi zao binafsi, lakini kwa mwananchi wa kawaida huu ni sawa na utajiri huo huo anaouzungumzia. Au kwavile yeye hajatumia neno vijisenti ndio tatizo? Kwani kwa mtu anayeishi kwenye nyumba za kifahari nje ya nchi na yule anayeishi Tanzania kifahari tofauti zao ni nini hasa? Unless anataka kutuambia anaowasema yeye hawajapata fedha zao kihalali ila watoto wake wamepata zao kihalali. Haya mahojiano ya Msuya kwangu mimi yanaonekana kama alitaka kufikisha ujumbe kwa watu fulani hivi. Either way naamini bado ana-power ya kushawishi CCM ijisafishe otherwise itaishia tu kuwa mipasho kwenye magazeti.
 
*Asema ndiye ametufikisha tulipo

Na Godfrey Ismaely

MAKAMU wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu katika Serikali ya awamu ya Kwanza Bw. Cleopa Msuya ameishauri serikali kufanya uchunguzi wa kutosha juu ya viongozi
wanaovuliwa au kujivua gamba wenyewe ili wakibainika kwamba walijipatia mali walizonazo kinyume na taratibu wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Mwito huo aliutoa jana nyumbani kwake Dar es Salaam, wakati akifanya mahojiano maalum na Majira lengo likiwa ni kufahamu hatima na mwelekeo wa Taifa na tathimini yake juu ya mwenendo wa mambo ya siasa likiwamo suala la upatikanaji wa nishati ya umeme ambalo kwa sasa limeonekana kuwa kero kwa uchumi na hata uzalishaji.

"Lazima kila mmoja awajibike katika kutoa ufafanuzi awe amevuliwa au amejivua gamba mwenyewe kwa kuwa sisi wananchi tunachoitaji zaidi ni kuona hatua za kisheria zinachukuliwa dhidhi yao na ikiwezekana wawajibishwe," alisema Bw. Msuya na kuongeza.

"Zingatia kuna hatua za aina mbili ambazo zinaweza kuzaa matunda kwanza ni juu ya Chama kuwachukulia hatua za kuwapima watendaji wake na hata viongozi wanaotuhumiwa na vitendo vya ubadirifu kwa kuwavua wote madarakani.Hatua ya pili ni serikali kupitia vyombo vya dola hasa mahakama inapaswa kutumia vigezo vyake kwa kuzingatia kuwawajibisha wahusika na katika ili tunapaswa kuwa na 'Zero tolerance wakati wa kuwachukulia hatua'," aliongeza

Pia alisema kuwa suala la kuwafumbia macho viongozi wabadirifu madarakani ndiyo chanzo kinachochangia baadhi ya mipango ya maendeleo ya wananchi kutofanikiwa mapema.

"Ukienda katika Halmashauri utagundua kuwa hali ni mbaya kweli kutokana na watendaji ambao wanajihusisha na suala la hongo hasa katika mpango wa kilimo kwanza katika hatua za kuagiza na kuwapatia wakulima powertiller hivyo hali kama hii haipaswi kufumbiwa macho bali hatua zinapaswa kuchukuliwa dhidhi yao mara baada ya uchunguzi," alisema Bw. Msuya.

"Ukifanya uchunguzi utagundua kuwa viongozi wengi wanaoingia madarakani siyo kwa dhumuni la kuwatumikia wananchi kama awali bali kujilimbikizia mali na hata kutekeleza mipango yao.Tuchukue mfano kwa Mwalimu, watoto wake na Mzee Kawawa utagundua kuwa licha ya kukaa madarakani kwa muda mrefu maisha yao ni ya kwaida kama watanzania wengine tofauti na sasa tunavyoshuhudia watu wameenda kujilimbikizia mabilioni nje ya nchi huku wakiyaita vijisenti, wengine wakijenga majengo na kuendesha magari ya thamani kubwa bila kujali maslahi ya wananchi," alisema Bw. Msuya.

UMEME

Bw. Msuya alisema kuwa suala la umeme hata kama litaendelea kupigiwa kelele kwa namna gani nchini kama serikali na hata vyama vya upinzani havitakaa kwa pamoja wakiwemo wataalam ili kuandaa michanganuo inayoeleza namna ya kutumia rasilimali zilizopo hapa nchini zitakuwa kelele ambazo hazina tija.

"Hata misimamo iwekwe ya namna gani ya kutaka kuwashinikiza vingozi walioko madarakani wakiwamo wale wa Wizara ya Nishati na Madini wajiuzulu, ufumbuzi juu ya tatizo la kudhibiti mgawo wa umeme hauwezi kupatikana kwa kuwa kinachoitajika kwa sasa ni uwekezaji na michanganuo inayoonesha namna ambavyo rasilimali zilizopo hapa nchini kama makaa ya mawe, gesi,upepo na nishati ya jua inavyoweza kutumika kuzalisha umeme," alisema Bw. Msuya.

Alisema imefikia hatua kwa serikali kuwekeza zaidi katika nishati ya umeme kupitia mipango ambayo walikuwa wanatumia awali ya miaka mitano kwa madai kwamba rasilimali zilizopo hapa nchini zinaweza kuzalisha umeme wa kutosheleza kwa matumizi ya ndani na hata kwa ajili ya kuuza nje.

"Tatizo hili tunaloshuhudia la nishati linatokana na utaratibu usioridhisha katika serikali ya awamu ya tatu, kwa kuwekeza fedha vibaya na wala siyo awamu ya nne hawa walibebeshwa mzigo tu' kutoka kwa EPA, RICHMOND lakini kwa mtazamo wangu ninaona waliohusika wote wakati wakiendelea kuchukuliwa hatua za kisheria serikali inaweza kuajiri na hata kuwatumia wataalam wa ndani na nje ili kuandaa michanganuo ya kutuondoa hapa tulipo sasa," alisema Bw. Msuya.


MALUMBANO BUNGENI

Bw. Msuya alisema kuwa viongozi wengi wanaoingia madarakani kwa sasa siyo kwa lengo la kuwasiadia ama kutatua kero za wananchi bali wamelenga maslahi binafsi.

"Ninakiri hadi leo hapa tangu 1992 mara baada ya serikali kufikia uamuzi wa kujiunga na mfumo wa vyama vingi sijamuona kiongozi mwenye uthabiti na mwelekeo wa kumsaidia mwananchi na hata kelele wanazopiga bungeni kwa sasa wala hazilengi kumsaidia mwananchi bali wanalenga maslahi yao tu.Kiongozi mwenye nia ya dhati kwa ajili ya kumsaidia mwananchi huwa anaadaa mchangunuo mzuri unaoelekeza jinsi ya kuzikabili kero za wananchi wala siyo kusema tu,"alisema Bw. Msuya.

UCHUMI

Kwa upande wa uchumi alisema kuwa uwezekano wa Tanzania kuipita Kenya katika ukuaji wa uchumi wake kupitia kipimo cha GDP upo wazi kwa kuwa hali ilivyo kwa sasa mwelekeo huo upo ila kinachoitajika ni jitihada na uwajibikali kwa kila mtendaji na wananchi kwa kuzingatia matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo hasa madini, vivutio vya ukalii, mbuga, gesi na mito.

"Uchumi wetu umeendelea kukua siku hadi siku kwa asilimia saba hadi kumi tofauti na Kenya ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia tatu hadi tano lakini kwa kupiga hatua zaidi. Tatizo ni kwamba ukuaji huo wala hauonekani kutokana na kutotumia vyema rasilimali zetu lakini ninaamini zikitumika vyema siku si nyingi tutaipita hata Kenya kiuchumi," alisema Bw. Msuya.
 
Mimi naona watu waliokuwa kwenye serikali ya awamu ya tatu bado wako kwenye awamu ya nne isipokuwa to Mkapa... kwahiyo Awamu zote zinayajua haya Ya Pili, Ya tatu na Ya Nne.
 
Atoke zake huko Wakiwa Kwenye Madaraka hawasikii wala hawaoni wakitoka wanajifanya kukosoa, Si alikuwa kwenye Serikali ya Fisadi Mkapa.
Tunachokita Watanzania kuiondoa CCM na Majambazi wake, ili tujipange upya

Kuna ukweli. Kuna siku JK aliuliza wanamlaumu yeye lakini wao walifanya nini walipokuwa madarakani. It may sound stupid but it make some sense.

Msuyua bado anaweza kuinfluence mambo, hwy has he been so quiet for long time, wakati mambo yanaenda hovyo kwa miaka 7 sasa? unaweza kuona kuwa kuna unafiki fulani.
 

Nadhani huyu mzee anashinda muda mwingi amelala kama hajaona dr slaa anafanya vitu hivyo kwa vitendo basi hatuko naye tanzania labda kaja jana au yupo lakini amelala muda wote Bajeti ya chadema nimchanganuo tosha wa namna wananchi watakavyo letewa maendeleo sio blabla za ngeleja na wana magamba wenzake nadhani ifikie pahala maoni ya wazee walio choka kama huyu yasitiliwe maanani kwani yatakua yanapotosha wananchi hasa kuhusu wamwamini nani mwenye mlengo wa kujari maslai ya umma kwa dhati. Nashukuruu kumuona dr slaa akiwa hai kila siku.



Na mimi nashawishika kuamini kwamba wengi wa wale wanaoongoza upinzani ni wanaharakati zaidi kuliko kuwa viongozi. Kuwa kiongozi ni zaidi ya kuwa mwanaharakati.
 
Back
Top Bottom