nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
na Janet Josiah
WAZIRI Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (83), amepata rufaa ya kupelekwa nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kabla ya hapo, Msuya alilazwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) Februari 4 mwaka huu, na kushughulikiwa na jopo la madaktari bingwa wa hospitalini hapo.
Msemaji wa Moi, Almas Jumaa, aliiambia Tanzania Daima jana kuwa Msuya alitoka hospitalini hapo juzi saa tatu usiku baada ya kuthibitishiwa safari yake.
Hata hivyo, Almas alisema hana taarifa rasmi ya siku ambayo mwanasiasa huyo mkongwe ataelekea Uingereza kwa sababu safari yake inashughulikiwa na madaktari wa Moi kwa kushirikiana na mtoto wake aliyemtaja kwa jina moja la Dk. Msuya.
Maandalizi ya safari yake yanafanywa na baadhi ya madaktari wa Moi kwa kushirikiana na mtoto wake Dk. Msuya hivyo ikishakamilika tutawaeleza alioambatana nao, alisema.
Viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa walifika hospitalini hapo kumjulia hali kwa nyakati tofauti akiwemo Rais Jakaya Kikwete aliyekwenda juzi.
Msuya amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za kisiasa ukiwemo ubunge wa Jimbo la Mwanga, Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri Mkuu kwa vipindi viwili tofauti na Katibu Mkuu wa Wizara za Ardhi, Fedha, Maji na Utamaduni na Ustawi wa Jamii.