msukumo unaosababisha mtu afanye tendo la ndoa.

gfsonwin duh kweli umeongea
Na asante sana
Ila kumbuka kuwa fanya utakavyofanya na kwa msukumo wa aina yoyote ila upate kile ambacho umekitaka maana kuna kwingine unaweza ishia pata maumivu na la muhimu cheza salama kwa popote pale utakapokuwa kama hujahalilishwa
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi poleni sana kwa majukumu ya kujenga taifa.

Leo kama kawaida baada ya kukagua jukwaa hili pendwa nimeona nije na huu uzi. Kila mwana MMU akiulizwa swali kwamba nini kinachomsukuma kufanya tendo la ndoa naamini atakuja na jibu kati ya haya hapa. Na ndio maana nikaona niiweke bayana hapa.

1) HAKI YA MSINGI KATIKA NDOA.
Katika ndoa swala la ufanyaji tendo la ndoa limehalalishwa na likawekwa kama sehemu ya kustareheshana na pia kama njia ya kuendeleza vizazi. Wanandoa wafanyapo kamwe hawahesabiwi kuwa wadhambi ama wakosa kwani ndio msingi wa umoja wao.

2) RUSHWA
Baadhi ya watu hufanya ngono kwasababua ya kutaka kununua huduma fulani ama kulipa fadhila fulani. Hii hutokana na ugumu ambao muhusika anao katika jambo husika. ugumu huo waweza kukuta ni wa kifedha, ugumu wa maisha, kazi, cheo, nk. Vijana wengi wa kike kwa wa kiume huanguka katika mtego huu na kujikuta wale wa kiume wakiwa na ma sugar mamy na wakike wakiwa na mabuzi.

3) TABIA

Kuna baadhi ya watu hufanya ngono kwasababu ya tabia tu. Hawa huwakuti na shida ama hitaji lolote lakin bado wanaanguka katika mtego wa kufanya ngono hovyo. wengi wao ni watu walioko kenye ndoa ambao kwao haijalisha kama ana mke ama mume basi lazima tu atakuwa mtu wa kutembea nje ya ndoa yake.

4) BIASHARA

Wapo watu ambao wameamua kuuza miili yao ili kuweza kukidhi haja za kimaisha. wengi wa hawa wawe wakike ama wakiume wapo kwenye uzinzi ili waweze kupata pesa za kujikimu kimaisha. Haijalisha anauza mwili wapi na kwa gharama gani ila wote ni wafanya biashara wa miili yao.

5) STAREHE

Kuna baadhi ya watu ambao hufanya ngono kama moja ya starehe zao. mara nyingi sana hawa ni wale ambao wakoa katika uchumba ama urafiki ambao hujikuta wanahitaji kuliwazana hivyo huliwazana kwa namna ya kufanya ngono.

6) UDADISI

Vijana wadogo wengi hasa school childrens huanguka katika kundi hili. Hawa hutaka kudadisi inafanywaje, inaraha kiasi gani na ikoje. kwao hakuna commitment zaid ya kugundua what is inside it.

HITIMISHO

Tendo la ndoa iwe limefanywa kwa msukumo gani nyuma yake laweza kuishia kupata mimba ama kupata ukimwi. Ingawa wengi husema heri mimba utazaa mtoto kuliko ukimwi, mimi huwa nasema heri ukimwi utakuwa ndani yako wewe uliyeutafuta kuliko mimba ambayo utazaa watoto ambao huwatarajii na hivyo kuongeza idadi ya watoto wanaokosa malezi stahiki.

hapo kwenye red mwana nakubaliana na wewe asilimia mia.
 
Mwalimu gfsonwin nakubaliana na wewe kwenye baadhi ya sababu ila i beg to differ kwenye sehemu moja tu. Nayo ni ile ya kusema STAREHE ni msukumo unaojitegemea. Binafsi naamini ngono/tendo la ndoa kwa ujumla wake aidha limefanywa kwa msukumo upi lina tabia mbili nazo ni STAREHE na UCHUNGU/KARAHA. Maana yangu ni kwamba unaweza kufanya ngono ukiwa kwenye ndoa na usipate starehe badala yake ukapata karaha na pia unaweza kufanya ngono kwa msukumo wa pesa ukapata starehe na sio karaha. So, inategemea.

Kikubwa kinachoweza kutofautisha hapa ni nani anapata nini kwa sababu tendo lenyewe linahusisha watu wawili. Ni kawaida sana wote kupata starehe, mmoja kupata starehe mwingine karaha wakati mwingine inatokea wote mnaliona tendo kama ni karaha..lakini inakuwa ngumu kidogo kwa wote kupata karaha kwa sababu lazima mtoa mada ajione amefurahi
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom