msukumo unaosababisha mtu afanye tendo la ndoa.

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,274
20,673
Wanajamvi poleni sana kwa majukumu ya kujenga taifa.

Leo kama kawaida baada ya kukagua jukwaa hili pendwa nimeona nije na huu uzi. Kila mwana MMU akiulizwa swali kwamba nini kinachomsukuma kufanya tendo la ndoa naamini atakuja na jibu kati ya haya hapa. Na ndio maana nikaona niiweke bayana hapa.

1) HAKI YA MSINGI KATIKA NDOA.
Katika ndoa swala la ufanyaji tendo la ndoa limehalalishwa na likawekwa kama sehemu ya kustareheshana na pia kama njia ya kuendeleza vizazi. Wanandoa wafanyapo kamwe hawahesabiwi kuwa wadhambi ama wakosa kwani ndio msingi wa umoja wao.

2) RUSHWA
Baadhi ya watu hufanya ngono kwasababua ya kutaka kununua huduma fulani ama kulipa fadhila fulani. Hii hutokana na ugumu ambao muhusika anao katika jambo husika. ugumu huo waweza kukuta ni wa kifedha, ugumu wa maisha, kazi, cheo, nk. Vijana wengi wa kike kwa wa kiume huanguka katika mtego huu na kujikuta wale wa kiume wakiwa na ma sugar mamy na wakike wakiwa na mabuzi.

3) TABIA

Kuna baadhi ya watu hufanya ngono kwasababu ya tabia tu. Hawa huwakuti na shida ama hitaji lolote lakin bado wanaanguka katika mtego wa kufanya ngono hovyo. wengi wao ni watu walioko kenye ndoa ambao kwao haijalisha kama ana mke ama mume basi lazima tu atakuwa mtu wa kutembea nje ya ndoa yake.

4) BIASHARA

Wapo watu ambao wameamua kuuza miili yao ili kuweza kukidhi haja za kimaisha. wengi wa hawa wawe wakike ama wakiume wapo kwenye uzinzi ili waweze kupata pesa za kujikimu kimaisha. Haijalisha anauza mwili wapi na kwa gharama gani ila wote ni wafanya biashara wa miili yao.

5) STAREHE

Kuna baadhi ya watu ambao hufanya ngono kama moja ya starehe zao. mara nyingi sana hawa ni wale ambao wakoa katika uchumba ama urafiki ambao hujikuta wanahitaji kuliwazana hivyo huliwazana kwa namna ya kufanya ngono.

6) UDADISI

Vijana wadogo wengi hasa school childrens huanguka katika kundi hili. Hawa hutaka kudadisi inafanywaje, inaraha kiasi gani na ikoje. kwao hakuna commitment zaid ya kugundua what is inside it.

HITIMISHO

Tendo la ndoa iwe limefanywa kwa msukumo gani nyuma yake laweza kuishia kupata mimba ama kupata ukimwi. Ingawa wengi husema heri mimba utazaa mtoto kuliko ukimwi, mimi huwa nasema heri ukimwi utakuwa ndani yako wewe uliyeutafuta kuliko mimba ambayo utazaa watoto ambao huwatarajii na hivyo kuongeza idadi ya watoto wanaokosa malezi stahiki.

alwayz
Mwl-gfsonwin
 
You have done your homework teacher!!! Well reseached!! Natoa hitimisho BINAFSI!! Uwe umefanya kwa kusukumwa na hivo vigezo au kwa kuamua mwenyewe. the End Point ni kuwa uhakikishe una ENJOY every bit of it! Jst remember ALWAYS USE A CONDOM, n safe sex is the best!!! NANI KANUNA?????? LOLEST
 
thanks LARA. ila kuna wengine wanakutana na unyanyasaji wa kutokutumia condom hasa wakiwa kwenye biashara and real that pains me a lot. ukiwauliza wanaojiuza utaskitika sana unyanyasaji wanaofanyiwa na wateja wao.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin UNGETUMIA NENO NGONO INGEPENDEZA ZAIDI KULIKO TENDO LA NDOA, HILO TENDO HUFANYWA NA WANANDOA PEKEE WENGINE WOOTE WANANGONOKA

nilitamani kutumia neno hili ila kwa jinsi ambavyo tendo hili limebarikiwa nkashindwa kuliita hivyo. ukisoma pako mahali ambapo nimeonyesha ngono.
 
Wanajamvi poleni sana kwa majukumu ya kujenga taifa.

Leo kama kawaida baada ya kukagua jukwaa hili pendwa nimeona nije na huu uzi. Kila mwana MMU akiulizwa swali kwamba nini kinachomsukuma kufanya tendo la ndoa naamini atakuja na jibu kati ya haya hapa. Na ndio maana nikaona niiweke bayana hapa.

1) HAKI YA MSINGI KATIKA NDOA.
Katika ndoa swala la ufanyaji tendo la ndoa limehalalishwa na likawekwa kama sehemu ya kustareheshana na pia kama njia ya kuendeleza vizazi. Wanandoa wafanyapo kamwe hawahesabiwi kuwa wadhambi ama wakosa kwani ndio msingi wa umoja wao.

2) RUSHWA
Baadhi ya watu hufanya ngono kwasababua ya kutaka kununua huduma fulani ama kulipa fadhila fulani. Hii hutokana na ugumu ambao muhusika anao katika jambo husika. ugumu huo waweza kukuta ni wa kifedha, ugumu wa maisha, kazi, cheo, nk. Vijana wengi wa kike kwa wa kiume huanguka katika mtego huu na kujikuta wale wa kiume wakiwa na ma sugar mamy na wakike wakiwa na mabuzi.

3) TABIA

Kuna baadhi ya watu hufanya ngono kwasababu ya tabia tu. Hawa huwakuti na shida ama hitaji lolote lakin bado wanaanguka katika mtego wa kufanya ngono hovyo. wengi wao ni watu walioko kenye ndoa ambao kwao haijalisha kama ana mke ama mume basi lazima tu atakuwa mtu wa kutembea nje ya ndoa yake.

4) BIASHARA

Wapo watu ambao wameamua kuuza miili yao ili kuweza kukidhi haja za kimaisha. wengi wa hawa wawe wakike ama wakiume wapo kwenye uzinzi ili waweze kupata pesa za kujikimu kimaisha. Haijalisha anauza mwili wapi na kwa gharama gani ila wote ni wafanya biashara wa miili yao.

5) STAREHE

Kuna baadhi ya watu ambao hufanya ngono kama moja ya starehe zao. mara nyingi sana hawa ni wale ambao wakoa katika uchumba ama urafiki ambao hujikuta wanahitaji kuliwazana hivyo huliwazana kwa namna ya kufanya ngono.

6) UDADISI

Vijana wadogo wengi hasa school childrens huanguka katika kundi hili. Hawa hutaka kudadisi inafanywaje, inaraha kiasi gani na ikoje. kwao hakuna commitment zaid ya kugundua what is inside it.

HITIMISHO

Tendo la ndoa iwe limefanywa kwa msukumo gani nyuma yake laweza kuishia kupata mimba ama kupata ukimwi. Ingawa wengi husema heri mimba utazaa mtoto kuliko ukimwi, mimi huwa nasema heri ukimwi utakuwa ndani yako wewe uliyeutafuta kuliko mimba ambayo utazaa watoto ambao huwatarajii na hivyo kuongeza idadi ya watoto wanaokosa malezi stahiki.

alwayz
Mwl-gfsonwin
AISEE... UMESAHAU VISHAWISHI: Unaweza kuwa hujatamani ila ukashawishiwa ukajikuta unatoa au unapiga.
TAMAA: Kuna watu sio tabia, sio haki ya ndoa, sion vishawishi, starehe... yaani wasione kichaka...watataka kujisaidia
 
vishawish vinaanguka katika makundi karibia yote, manake mwenye rushwa atasema ameshawishiwa na tamaa ya hela, mwenye kudadisi atasema kashawishiwa na kutaka kujua, nk. sijui kama kuna mtu anafanya ngono bila msukumo wa ndani.
 
Wanifurahisha sana,

Ni mjuzi wa mengi, uwe unamwaga data tujifunze na sisi

nafurahi sana kusikia kwamba nakufurahisha. jf bana ndo mpango mzima hapa utajifunza hadi basi. kuna wataalm kama dad yangu AshaDii na mzee wangu Dark City watakufunza mengi sana.
 
Last edited by a moderator:
nilitamani kutumia neno hili ila kwa jinsi ambavyo tendo hili limebarikiwa nkashindwa kuliita hivyo. ukisoma pako mahali ambapo nimeonyesha ngono.

tendo hili limebarikiwa kwa wanandoa tuu na si kwa kila mtu, Huwezi kuita wanayofanya machangudoa limebalikiwa hapo inakuwa ni laana!
 
ni kweli limebarikiwa na Mungu aliliumba ni takatifu sasa kasheshe ni kwamba Mungu alishalibariki sisi wanadamu ndio tunaoliharibu, je tuendelee kukataa uhalisia Mungu alioueka kwenye baraka zake kwasababu ya matendo yetu maovu? sisem kwamba wanaofanya biashara ni wanafanya tendo la ndoa la hasha hawa wanazini na mimi naiita ni ngono.

heading yangu ilitumika kwasababu nilitaka kuanza na utakatifu wa tendo husika na ndio maana nikaanza na category iliyoruhusiwa nayo ni ndoa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom