Jamaa aliuzoa umaarufu kwa siku moja tu. Lakini bahati mbaya umaarufu mbaya wa kuwa na mdomo mchafu wa mtusi usio na staha mbele ya kina mama, baba, watoto na wanafunzi ambao yeye anapaswa kuwa mwalimu wao!!
Hataweza kuipata heshima hiyo kwa sababu kipimo alichowapimia wenzake, naye atapimiwa hicho hicho.
Alivyo mjinga (na hii ni tabia ya wana CCM wengi), atatafuta platform nyingine na kuwaporomoshea matusi mengine hao watu waliomzomea na maneno mengine ya kejeli kama hawa ni UKAWA tu, wanywa viroba na mengine kibao kana kwamba hawazihitaji kura za wana UKAWA na wanywa viroba!!
Ni vyema akakaa chini na kujiuliza maswali ya msingi ya kwa nini yeye kiongozi mkubwa (M/kiti wa CCM mkoa wa GEITA) afike sehemu badala ya kusikilizwa kwa heshima, anapuuzwa na kuzomewa!!
Ila kama anadhani nafasi aliyo nayo imemlevya na anadhani atakuwa nayo milele, aendelee kutukana watu wengine!!